Mbunge Jafari Chege Aitaka Serikali Kufanya Maboresho ya Sera ya Ardhi Mwaka 1995

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

MBUNGE JAFARI CHEGE AITAKA SERIKALI KUFANYA MABORESHO YA SERA YA ARDHI MWAKA 1995

"Je, ni lini Serikali itafanya maboresho ya Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Rasimu ya Sera ya Taifa ya mwaka 1995 toleo la mwaka 2023 liliwasilishwa katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri tarehe 18 Agosti, 2023. Wizara imekamilisha maboresho ya Rasimu ya Sera kwa kuzingatia maoni ya Baraza la Mawaziri, hatua inayofuata ni Rasimu ya Sera kujadiliwa katika Mkutano wa kazi wa Baraza la Mawaziri kwa tarehe itakayopangwa" - Mhe. Geofrey Pinda

"Ni lini kama Wizara ya Ardhi mtaridhia kuhamisha Mabaraza ya Ardhi kutoka kwenye Wizara kwenda kwenye mfumo wa Kimahakama? Je, lini Serikali utaridhia na kuhamisha Mamlaka ya Maendeleo ya Ardhi nchini ili kuendelea kuimarisha usimamizi na uimara katika kutatua migogoro nchini" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Wizara ipo kwenye mchakato wa kuanzisha Tume (Commission) ya Ardhi ambayo itasimamia Mamlaka ya Ardhi kwa Maendeleo ya Watanzania" - Mhe. Geofrey Pinda
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2023-11-12 at 09.07.56.mp4
    25.5 MB
Back
Top Bottom