Mbunge Amandus Chinguile: Ni lini Serikali Italigawa Jimbo la Nachingwea.

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943

Mbunge Amandus Chinguile: Ni lini Serikali Italigawa Jimbo la Nachingwea.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kutangaza utaratibu na sifa za kugawa majimbo mbalimbali nchini, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga amesema kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, NEC imepewa mamlaka ya kuchunguza mara kwa mara maeneo ili kugawa mipaka ya majimbo ya uchaguzi angalau kila baada ya miaka 10 baada ya kupata kibali kutoka kwa Rais.

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Nachingwea, Amandus Chinguile aliyetaka kufahamu ni lini Serikali italigawa jimbo la hilo.

Chinguile ameshauriwa kuwasilisha maombi ya kugawa jimbo hilo mara tu NEC itakapotangaza kugawa au kubadili majina ya majimbo ya uchaguzi.
 
Attachments

  • IMG-20210508-WA0131.jpg
    IMG-20210508-WA0131.jpg
    228.4 KB · Views: 3
  • 04952d74-b7b6-4308-9e42-a5fb25d9c05f-1024x847.jpg
    04952d74-b7b6-4308-9e42-a5fb25d9c05f-1024x847.jpg
    97.5 KB · Views: 3
Hakuna hapa..... akomae,bilashaka kanusa hali ya kutokurudi tena bungeni,endapo jimbo lisipogawanywa.
 
wapinzani wakionekana kutaka majimbo ,na CCM wanaona kushindwa ndio huu uhuni unaanza utasikia kugawa,kugawa
 
Wakigawa hayo majimbo yaitwe majina yalipo, na sio nachingwea mashariki, kusini, magharibi, mashariki. Mfano jimbo la manyoni magharibi liitwe jimbo la itigi, jimbo la singida magharibi liitwe sepuka, jimbo la ikungi, jimbo la ilongero itapendeza sana majimbo yaitwe yaliko makao makuu ya halmashauri yake. Kama halmashauri ina majimbo zaidi ya moja basi jimbo jingine liitwa jina la kata mojawapo iliyochangamka. Pia jimbo linaweza kuitwa jina la kijiografia liliko kama jimbo la bonde la ufa, jimbo la mlima kitonka, jimbo la mto malagasi, mto ruvu, jimbo la ruaha, jimbo la meru, nyumba ya mungu, tarangire, jimbo la nyanza nk.
 
Wazo jema munyampaa.
 
yale majimbo ya iramba magharibi na iramba mashariki yaitwe jimbo la kiomboi na jimbo la mkalama
Wanaogawa majimbo sidhani kama huwa wanaenda fizikale na kuchukua hata maoni tu kwa wakazi husika.Wanajumlisha/generalise tu eti mashariki au magharibi!Kwani maeneo hayo hayana majina maarufu au pendekezwa?Waache uvivu,ubinafsi na mahovyohovyo yao.
 
Mkuranga nayo kubwa sana asee,watoe majimbo mawili ulega kazidiwa kazi na kasi ya ukuaji wa wilaya ya mkuranga.
 
Back
Top Bottom