Mbunge: Serikali iwekeze katika elimu badala ya mabweni ili kukwepa mimba za utotoni

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Mbunge wa Viti Maalumu, Hawa Mwaifunga ameitaka Serikali kuongeza nguvu ya kutoa elimu kwa jamii ili kupunguza tatizo la mimba za utotoni huku akieleza moja ya sababu ni wanafunzi kufuata shule mbali na makazi yao.

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Jijini Dodoma leo.

“Tabora unakuta kuna watoto wana miaka 12 au 13 ni wajawazito, tunaposema kuongeza mabweni badala ya kutoa elimu tunakuwa hatusaidiii, tufanye hivyo ili kuokoa kizazi,” alisema Hawa Mwaifunga

Serikali imepanga kuongeza ujenzi wa mabweni katika Bajeti Kuu ya mwaka wa fedha 2022/2023 ili kupunguza tatizo hilo.
 
Atleast wapewe elimu ya kutosha, kuhusiana na mimba za utotoni. Lakini kushikilia mabweni tuuu, ata mabwenini mimba zinapatikana.
 
Shule za bweni watoto Wanapigwa miti sana na Walimu wao. Binafsi naamini collective responsibility Kama msingi wa kutatua tatizo hili .
 
Mbunge wa Viti Maalumu, Hawa Mwaifunga ameitaka Serikali kuongeza nguvu ya kutoa elimu kwa jamii ili kupunguza tatizo la mimba za utotoni huku akieleza moja ya sababu ni wanafunzi kufuata shule mbali na makazi yao.

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Jijini Dodoma leo.

“Tabora unakuta kuna watoto wana miaka 12 au 13 ni wajawazito, tunaposema kuongeza mabweni badala ya kutoa elimu tunakuwa hatusaidiii, tufanye hivyo ili kuokoa kizazi,” alisema Hawa Mwaifunga

Serikali imepanga kuongeza ujenzi wa mabweni katika Bajeti Kuu ya mwaka wa fedha 2022/2023 ili kupunguza tatizo hilo.
Huu ni wimbo wa miaka yote
 
Back
Top Bottom