Mbunge Mkundi: Serikali iwekeze kwenye huduma za Kijamii

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

F-aPKWva8AAc-J3.jpg

Mbunge wa jimbo la Ukerewe (CCM), Mhe. Joseph Mkundi ameishauri serikali kuwekeza katika huduma za kijamii ili kukuza uchumi wa taifa.

Mhe. Joseph Mkundi ameyasema hayo Novemba 7,2023 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mapendekezo ya mwongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

"Tukiwekeza kwenye huduma za kijamii, uchumi wetu utaendelea kukuwa kwa kiwango kikubwa sana ,na hili ndio maana nitumie nafasi hii kumpongeza Mhe. Rais kwa uwekezaji mkubwa sana alioufanya kwenye sekta ya huduma za kijamii kwenye elimu, afya, maji kazi kubwa imeafanyika" - Mhe. Joseph Mkundi

"Lakini bado kuna maeneo ambayo miundombinu yetu hasa ya usafirishaji kuna changamoto kubwa sana mfano eneo la Ukerewe" - Mhe. Joseph Mkundi

"Kuna vikwanzo vingi sana kwa watu wetu kule chini wanapokuwa wanafanyabiasahara, wanapokuwa wanafanya shughuli za uzalishaji vilevile, sekta ya uvuvi ni sekta muhimu kwenye taifa hili katika kuimarisha uchumi wa wetu" - Mhe. Joseph Mkundi

Hata hivyo amesema ipo haja ya kuwepo kwa sera ya taifa ya ufuatiliaji na tathimini ili mipango yote inayopangwa iweze kutekelezwa kwa wakati na kwa usahihi.

"Tukiwa na sera hii itasaidia kwanza kuongeza uwajibikaji, itasaidia miradi kufanyika katika kiwango bora na thamani ya pesa tuliyowekeza kwenye miradi ile kuonekana" - Mhe. Joseph Mkundi
 
Back
Top Bottom