Mbunge Santiel Kirumba Katika Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Kahama

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MBUNGE SANTIEL KIRUMBA KATIKA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU KAHAMA-SHINYANGA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Eric Kirumba akiwa na viongozi mbalimbali na wananchi wamejitokeza kuupokea Mwenge wa Uhuru leo 30 Julai, 2023 katika viwanja vya Kituo cha Afya Kagongwa Wilaya ya Kahawa.

Mwenge wa Uhuru Kahama-Shinyanga umepokelewa na kukimbizwa katika Miradi Sita (06) ya Maendeleo Kahama Mjini ikiwemo kupanda miti 500 katika Bwawa la Maji Nyihogo lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Kahama ili kutunza mazingira

Mradi wa Barabara za Manispaa ya Kahama wenye jumla ya Kilomita 1.39 zinazojengwa kwa kiwango cha lami, umezinduliwa leo na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Abdalla Shaib.

Akizungumza baada ya ukaguzi, Shaib amesema ameridhishwa na mradi huo wa barabara ambao unakwenda kuondoa changamoto ya vumbi na kuendana na ukuaji wa mji wa Kahama.​


Aidha, Mwenge wa Uhuru umezindua Klabu ya Kupinga Rushwa katika Shule ya Sekondari Kagongwa, Manispaa ya Kahama ambapo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2023, Abdalla Shaibu ameongoza shughuli zote.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-07-30 at 21.24.00.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-30 at 21.24.00.jpeg
    85.9 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2023-07-30 at 21.24.02.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-30 at 21.24.02.jpeg
    105.7 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2023-07-30 at 21.24.01.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-30 at 21.24.01.jpeg
    103.1 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2023-07-30 at 21.22.08(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-30 at 21.22.08(1).jpeg
    158.9 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2023-07-30 at 21.22.08.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-30 at 21.22.08.jpeg
    154 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2023-07-30 at 21.22.07.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-30 at 21.22.07.jpeg
    102.8 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2023-07-30 at 21.24.02(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-30 at 21.24.02(1).jpeg
    110.9 KB · Views: 7
Back
Top Bottom