Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 576
- 1,625
Mbunge Ndaisaba Ruhoro akiwa anachangia hoja amesema; Mkaguzi mkuu wa ndani wa serikali anapewa fedha kutoka wizara ya fedha na anapewa fedha na katibu Mkuu Wizara ya fedha, na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ndiye anaetoa fedha kwenye halmashauri na mamlaka zote za serikali za mitaa na kwenye taaisisi za serikali.
Lakini Wakaguzi wa ndani ambao wapo kwenye taasisi wanaripoti kwa maafisa Masuuli ambao na wenyewe wanapewa fedha kutoka kwa katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, hili linafanya Wakaguzi wa Ndani wafungwe kamba.
Akiendelea kufafanua amesema, hakuna siku hata moja wakaguzi hawa wa ndani watakuja kufanya ukaguzi ambao hauiliwe na mtu na kuibua madudu yaweze kushughulikiwa, kwa sababu ya jinsi mfumo wa Ukaguzi wa Ndani ulivyotengenezwa nchini, na kupendekeza kuwa iundwe taasisi ya ukaguzi wa ndani inayojitegemea ambayo haiingiliani na afisa masuuli, akisema huu ndio mwarobaini pekee utakaowezesha ofisi ya wakaguzi wa ndani kuweza kufanya kazi kwa uhuru bila kuingiliwa na watu.
Kitendo cha kutofanya hivyo kimesababisha mpaka wakaguzi hao wa ndani kushiriki kwenye dili za kuiba. Akisema haiwezekani mkaguzi wa ndani yupo Halmashauri anaripoti kwa Mkurugenzi watu wanacheza dili halafu yeye wakamtoa mswaki, lazima na yeye apewe mgao!
Hivyo lazima taasisi hii ya Wakaguzi wa ndani ihuishwe, ifumuliwe na kutengenezwa upya, iwe huru na iweze kufanya kazi yake ya ukaguzi kisawasawa, vinginevyo wizi utaendelea!