Ripoti ya Uwajibikaji wa Vyombo vya Usimamizi kwa Taasisi za Umma 2021|22

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Hali ya Utekelezaji wa Mapendekezo ya CAG kwa Miaka 3 hairidhishi

1689077120507.png

Ripoti ya Uwajibikaji ya Taasisi ya Wajibu Institute imebainisha kuwa kwa kipindi cha Miaka Mitatu, (2018/19-2020/21), utekelezaji wa mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kikamilifu bado upo chini ya asilimia 50

Swali la msingi ni, kwa nini hakuna msukumo wa kutekeleza mapendekezo ya CAG?

1689142986449.png

Mapendekezo yanayotolewa na CAG yanalenga kuboresha mifumo ya usimamizi/
uwajibikaji na utendaji wa Serikali. Kutotekelezwa kwa mapendekezo ya CAG kwa
wakati, kunafanya madhaifu yaliyobainishwa kuendelea kuwepo na wakati mwingine
kuisababishia Serikali hasara.

1689230057140.png

Matokeo ya ukaguzi wa CAG kwa kipindi cha Miaka mitatu (2019/20 – 2021/22) yanaonesha maboresho katika uandaaji wa hesabu kwa Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa

Hii imepelekea kuongezeka kwa idadi ya Taasisi, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mashirika ya Umma yaliyopata hati safi kutoka 87% mwaka 2019/20 hadi kufikia 96% mwaka 2021/22

Hata hivyo bado kuna mapungufu kama, kutozingatiwa matakwa ya Sheria, kanuni na taratibu za utendaji kazi yaliyopelekea uwepo wa viashiria vya upotevu wa fedha na rasilimali za umma

Mapendekezo:

WAJIBU inaendelea kushauri yafuatayo;
a. Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ipendekeze kufanyika kwa marekebisho kwenye Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya mwaka 2008 ili kuweka kifungu kitakacho weka adhabu zikiwemo hatua za kinidhamu kwa Maafisa Masuuli ambao hawajatekeleza mapendekezo yanayotolewa na CAG katika kaguzi za fedha ambayo hayahitaji mabadiliko ya kisheria au mapendekezo yaliyo ndani ya uwezo wa maafisa masuuli.

Hii itawaongezea wakaguliwa msukumo, hamasa na ari ya kutekeleza mapendekezo ya CAG.

b. Serikali kupitia Taasisi ya Serikali Mtandao (eGA) iunganishe mfumo wa GARI- ITS na IFT - MIS ambayo inatumika sasa kufuatilia utekelezaji wa mapendekezoya CAG katika mashirika ya umma na Mamlaka ya Serikali za Mitaa.

Mifumo hii miwili iunganishwe ili kuwe na mfumo mmoja ulio wazi na madhubuti utakaotumika kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo ya CAG.

c. WAJIBU inashauri, Ofisi ya CAG itoe mapendekezo yake kwa mchanganuo wa mapendekezo ya muda mfupi, kati na mrefu ili kurahisisha utekelezaji na ufuatiliaji.

d. WAJIBU inashauri CAG kutoa mchanganuo wa mapendekezo yaliyo ndani ya uwezo wa maafisa masuuli na yale yanayohitaji mabadiliko mapana ya kisera, kisheria na miongozo mbalimbali. Mchanganuo huu ubainishe muhusika mkuu katika kutekeleza mapendekezo maususi na namna ya kumuwajibisha.
 

Attachments

  • Ripoti_ya_Uwajibikaji_Usimamizi_wa_rasilimali_za_umma_Final.pdf
    3.9 MB · Views: 4
View attachment 2684915

Ripoti ya Uwajibikaji ya Taasisi ya Wajibu Institute imebainisha kuwa kwa kipindi cha Miaka Mitatu, (2018/19-2020/21), utekelezaji wa mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kikamilifu bado upo chini ya asilimia 50

Swali la msingi ni, kwa nini hakuna msukumo wa kutekeleza mapendekezo ya CAG?
Hakuna msukumo kwa sababu hakuna wa kusukuma mwingine.
 
Back
Top Bottom