Mbunge Rose Busiga awataka Wanawake Nyang'wale kuendelea kuwa Jeshi la Rais Samia

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945
Mbunge wa Viti maalum mkoani Geita Mhe Rose Busiga amewataka wanawake wa Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita kuendelea kuwa jeshi la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema kuwa wanawake wanapaswa kujivunia kuwa na Rais mwanamke kwani hiyo ni hatua nzuri katika kuelekea ajenda ya 50 kwa 50 katika nchi ya Tanzania.

Mhe Busiga ameyasema hayo jana wakati wa hafla ya chakula cha jioni na kuzungumza na viongozi wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) wa kata zote za Wilaya ya Nyang'wale wakiwa Jijini Dodoma mara baada ya kutembelea Bungeni.

Mhe Busiga amewataka wanawake hao kuhakikisha kuwa wanaendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa ba Rais Samia nchini.

Kadhalika amewataka wanawake hao kujitokeza kwa wingi na kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwakani 2024 pamoja na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2025 kote nchini.

"Nawasihi kinamama wemzangu Tusitolewe kwenye reli tufanye kazi kwa bidii ili CCM iendelee kuaminiwa na kupata ushindi wa kishindo na hakikisheni Rais Samia anapata kura za kutosha katika uchaguzi mkuu 2025" Amesisitiza Mhe Busiga

Mhe Busiga amesema kuwa ujio wa viongozi wa UWT Nyang'wale bungeni Jijini Dodoma ni mwanzo wa ziara za wanawake wa UWT mkoani Geita ambapo kwa sasa ameanza na wilaya ya Nyang'wale huku akijipanga kwa wilaya zingine za Geita, Chato, Bukombe na Mbogwe.

MWISHO

1694012978223157-2.jpg
1694013132498773-0.jpg
1694013127973543-1.jpg
1694012964763902-5.jpg
1694012959815307-6.jpg
1694012954581414-7.jpg
 
MBUNGE ROSE BUSIGA AWATAKA WANAWAKE NYANG'WALE KUENDELEA KUWA JESHI LA RAIS SAMIA

Mbunge wa Viti maalum mkoani Geita Mhe Rose Busiga amewataka wanawake wa Wilaya ya Nyang'wale Mkoani Geita kuendelea kuwa jeshi la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema kuwa wanawake wanapaswa kujivunia kuwa na Rais mwanamke kwani hiyo ni hatua nzuri katika kuelekea ajenda ya 50 kwa 50 katika nchi ya Tanzania.

Mhe Busiga ameyasema hayo jana wakati wa hafla ya chakula cha jioni na kuzungumza na viongozi wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) wa kata zote za Wilaya ya Nyang'wale wakiwa Jijini Dodoma mara baada ya kutembelea Bungeni.

Mhe Busiga amewataka wanawake hao kuhakikisha kuwa wanaendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa ba Rais Samia nchini.

Kadhalika amewataka wanawake hao kujitokeza kwa wingi na kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwakani 2024 pamoja na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2025 kote nchini.

"Nawasihi kinamama wemzangu Tusitolewe kwenye reli tufanye kazi kwa bidii ili CCM iendelee kuaminiwa na kupata ushindi wa kishindo na hakikisheni Rais Samia anapata kura za kutosha katika uchaguzi mkuu 2025" Amesisitiza Mhe Busiga

Mhe Busiga amesema kuwa ujio wa viongozi wa UWT Nyang'wale bungeni Jijini Dodoma ni mwanzo wa ziara za wanawake wa UWT mkoani Geita ambapo kwa sasa ameanza na wilaya ya Nyang'wale huku akijipanga kwa wilaya zingine za Geita, Chato, Bukombe na Mbogwe.

MWISHO
Isaya 3:12
Katika habari za watu wangu, watoto ndio wanaowaonea, na wanawake ndio wanaowatawala. Enyi watu wangu, wakuongozao wakukosesha, waiharibu njia ya mapito yako.
 
Back
Top Bottom