Mbunge Ole Sendeka awasha Moto bungeni kuhusu ripoti ya CAG

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,232
6,479
Ktk Azimio Maalum la Kumpongeza Rais Samia kwa uongozi mzuri, kupitia Bunge la 12 mkutano wa 11 kikao cha Kwanza, Ole Sendeka awasha Moto.

Alianza kwa kumsifia Sana Rais Samia lakini mwishoni akaanza kwa kulaumu waliotajwa Ubadharifu Ripoti ya CAG kuenedelea ofisini hadi Sasa.

Kadai wasipojiuzulu na kujisalimisha, Basi kupitia Mkutano huu Bunge lifanye maamuzi dhidi ya wenye viburi na jeuri hao.

Amemtaka Rais achukue hatua vinginevyo yeye kwa kutumia Bunge hili atashawishi wabunge wachukue hatua juu ya watumishi mafisadi.

Wabunge wengine pia wamekuwa na mawazo Kama ya Sendeka na kudai Tanzania hakuna mtu wa kujiuzulu hadi tu aoneshwe mlango wa kutokea. Wamedai wakati wa Bunge kuonesha Meno yake ni Sasa.

Waliounga miongoni mwao ni kitila Mkumbo aliyechangia baada ya Sendeka, Saashisha Mafue, Mwakasaka na wengine wengi.
 
Back
Top Bottom