Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,902
- 945
MHESHIMIWA OLIVER ATATUA TATIZO LA UKOSEFU WA MAJI SHULENI
🏷️Leo Tar 22 September, 2023 Mhe Oliver Daniel Semuguruka (Mbunge Viti maalum Mkoa wa Kagera) alikuwa Mgeni rasmi katika mahafali ya shule ya Msingi Mgeza Mseto Bukoba Mjini, ambayo shule hiyo ni ya watoto wenye MAHITAJI MAALUMU.
🏷️ Pia Mhe. Oliver Amewakumbusha wazazi kutowatenga watoto wenye mahitaji maalumu. Badara yake wawakumbatie na kuwapa Elimu Bora na Kuwapa haki zote za mtoto za Msingi.
🏷️ Zaidi ya yote hayo Mheshimiwa Oliver ametatua tatizo la ukosefu wa maji shuleni hapo kwa kutoa Tank mbili zenye ujazo wa Lita 5000 kila moja.
🏷️Ikumbukwe Leo hii hii Mbunge huyu ameshiriki matukio mawili Kwa siku Moja (Mgeni Rasmi Mahafari na Kushiriki kikao cha Halmashauri kuu ya Mkoa ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mhe. Kassim Majaliwa Waziri Mkuu Tanzania) Hii ndio maana sahihi ya Neno "TUKUTANE SITE"
UNAPIGWA MWINGI HADI UNAMWAGIKA
#KaziIendelee......