Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 576
- 1,626
Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku 'Musukuma'
Vikao vya bunge vimefunguliwa rasmi leo tarehe 4/4/2023. Katika kikao cha leo, shughuli za Bunge zilisimamishwa kwa ajili ya Azimio la kumpogeza Rais, ambapo Wabunge walipata nafasi ya kutoa pongezi zao.
Kwa upande wa Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku 'Musukuma' amesema kwenye madudu yaliyoibuliwa na CAG, kuna viongozi wanaiba sehemu moja na kuhamishwa sehemu nyingine wanaenda kuendeleza wizi sehemu nyingine
Akisema kuwa TAKUKURU ina mrundikano wa kesi kutoka CAG na kama TAKUKURU kuna madudu pia basi waundiwe tume ya kuwachunguza. Akisema haiwezakani watu hao watajwe mwaka jana na mwaka huu pia bila kushughulikiwa.
Akasema Rais alisema kama wanakula basi wale kwa urefu wa kamba zao lakini hao hananunui kamba za katani, wananunua manati likijaa linatanuka.
Msukuma pia amesema hawataki tena kupiga swaga kwani kila CAG wanaongea lakini watu hawachukuliwi hatua. Amedai mwaka jana wameyajadili na mwaka huu watu hao hao wamepata hati chafu.