Kitila Mkumbo: Bunge liwaoneshe Mlango wa Kutokea wote waliotajwa kwenye Ripoti ya CAG

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Fuatilia yanayojiri Bungeni leo Aprili 4, 2023 kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 1.


MABASI KUTEMBEA KWA SAA 24

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tulia Ackson ameishauri Wizara ya Mambo ya Ndani kuangalia upya amri inayokataza mabasi ya abiria kutembea barabarani baada ya saa 6 usiku.

"Nafikiri hili jambo nimewahi kulisemea mahali pengine, ni muhimu Serikali ilitazame kwa ujumla wake. Tunazuia magari saa 6 kwa sababu ipi? Kwa sababu madereva ni walewale wanaotuendesha sisi na wanao endesha hayo magari mengine, madereva wanapitia masomo yaleyale. Kama kuna mahali pana mapungufu tuyafanyie kazi hayo mapungufu"

Ameongeza, "Lakini kuzuia abiria halafu anakaa hapo halafu gari inaondoka baada ya saa 4 labda saa 10 inaondoka au saa 11 inaondoka, sasa sijui tunakuwa tumezuia nini, hasa katika kapindi hiki ambacho Serikali inafanya juhudi kubwa sana ya kuboresha miundombinu ya barabara."

Dr._Tulia_Ackson.jpg

Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Spika amehoji nini maana ya kutengeneza hizo barabara kwa sababu abiria hao wangekuwa na gari binafsi wasingezuiwa kutembea usiku, huko ni kuchelewesha abiria.

Ametoa wito kwa Serikali, maeneo yenye miundombinu mizuri na ulinzi w kutosha mabasi ya abiria yaruhusiwe kutembea kwa saa 24.

TANESCO YATAKIWA KURUDIA TATHMINI YA MAENEO YANAYOSTAHILI UMEME WA TSH. 27,000
Mbunge Kilombero, Abubakar Damian Asenga Asenga ameuliza swali Bungeni kuwa ni lini Wizara itatekeleza maelekezo ya Waziri wa Nishati, Januari Makamba ya kurejesha punguzo la bei ya kuunganisha umeme kwa Tsh. 27,000 maeneo ya Vijijini katika Tarafa ya Ifakara.

Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato amesema utaratibu wa kubaini maeneo ya kuunganisha umeme kwa gharama ndogo hakufanyika kwa umakini, hivyo wameelekeza TANESCO kurudia zoezi hilo kwa kuwashirikisha Wabunge wote ili wapate maeneo sahihi.

Serikali imesema Mkandarasi anayepeleka umeme katika Wilaya ya korongwe Mkoani Tanga na maeneo mengine anafanya uzembe kukamilisha kazi.

Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato amesema tumekubaliana achukuliwe haua na itakapofika katikati ya mwezi huu (Aprili 2023) ikiwa hatafikia hatua waliyokubaliana watavunja mkataba.

KUWAJIBISHA VIONGOZI WALIOTAJWA NA CAG
Mbunge wa Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo amempongeza Rais Samia kwa kuboresha mambo mengi nchini yenye maslahi makubwa kwa Taifa.

KABUDI_0.jpg

Kitila Mkumbo, Mbunge wa Ubungo
Amesisitiza kuwa Rais amefanya sehemu yake katika kupokea na kumekemea changamoto zilizotajwa kwenye ripoti ya CAG, sasa kazi iliyobaki ni ya Bunge kuhakikisha kuwa waliotajwa wanachukuliwa hatua.

Prof. Mkumbo amesema "Yamebaki majukumu mawili, jukumu la kwanza kwa Bunge hili, jukumu la pili kwa Serikali kupitia mawaziri wetu. Na mimi niwaombe, katika muda tulionao hapa, tunatarajia kuona majibu kutoka Serikalini, majibu yatakayojibu zile changamoto za kimfumo, kisheria na kikanuni tuzione kutoka kwa mawaziri"

Ameongeza, "Mhe. Rais kaongea kwa uchungu sana, kazi yetu, sisi Tanzania hatuna utamaduni wa kupisha. Kazi yetu wabunge tuoneshe wenzetu ambao Rais amewasema, tuwaoneshe mlango wa kutokea. Hiyo kazi duniani, huwa haifanywi na Serikali, inafanywa na Bunge"

HAKUNA MTU KWENYE NCHI HII ANAWEZA KUACHIA MADARAKA KIZEMBE
Nae Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku (Musukuma) amesema haiwezi kutokea kwenye nchi hii mtu akaachia sehemu yenye mafuta kizembe, amemtaka Spika Tulia kuacha alama kwa kuhakikisha kuwa Bunge la Mwaka huu linawachukulia hatua kali wahusika wote waliotajwa kwenye ripoti ya CAG.

E2-lD6FXIAAd3tl.jpg

Joseph Kasheku, Mbunge wa Geita Vijijini
Amedai kuwa kauli aliyotoa Rais Samia kuhusu watendaji wa Serikali kula kwa urefu wa kamba yao ilitafsiriwa vibaya kwani watumishi hawa wameamua kutumia manati inayotanuka badala ya kamba ya katani.

Ametaka hatua stahiki zichukuliwe ili kuleta heshima kwenye matumizi ya pesa za Umma.
 
Ukitaka kuwa na maisha marefu huko bungeni kuwa mnafiki tu, funga mdomo wako, utakalia hivyo viti mpaka uvichakaze wakubadilishie na kukuwekea vipya.

Namshangaa Kitila anataka vipi wabunge wahusike kuwashughulikia wezi wa mali za umma, hilo bunge la Tulia ni kibogoyo, Spika mwenyewe chawa wa Rais..

Kitila anaposema Rais ameshamaliza sehemu yake naye hajitambui, Rais hawezi kuimaliza sehemu yake simply kwa kuwaita wezi wa pesa za walipa kodi "stupid" ... we need action.
 
Huu uzi ukiusoma kwa umakini mkubwa wachawi utawaona tu
Roho zinawauma wenzao wanapotekeleza majukumu yao
Wanapolipwa stahiki zao kwa majibu wa sheria taratibu na kanuni za nchi hii hii
 
Tatizo SIO Kutembea usiku tu lakini pia usalama wa abiria wanapokua wanaendeshwa na Madereva wenye usingizi.

Nafikiri pangekua na utaratibu wa kuwa na mapumzuko baada ya kuendesha masaa mtano matatu mpaka manne mfululizo wakati Wa usuki , Waafrika hua hawapumziki wanapotafuta pesa. MTU asiyepumzika ni hatari sana. Hata wasimamizi Wa SHERIA mara nyingi ni wakorofi sana kutokana na kufanya KAZI usiku na mchana bila kupumzika. Wakimkamata mtuhumiwa wanapiga mpaka kumaliza hasira zao na stress zao kwenye nafsi zao.

Kwa madereva wengi hua hawana muda Wa kupumzika kabisa iwe mchana au usiku. Wengine hawapumziki kutokana na kazi nyingi na wengine kutokana na kutumia muda Wa kupumzika kwenye starehe za pombe na wanawake. Sasa wanapokua wanaendesha muda Mwingi wanakua na Hali ya uchovu na usingizi au kukosa utulivu Wa kuchukua maamuzi Sahihi wanapokua Barabarani.

Watu kama hawa kuwaambia waendeshe magari usiku kucha ni hatari mno. Barabara Bado ni finyu Kwa magari Kutembea usiku kwani magari mengi hayana vizibiti mwendo.

VTS za LATRA ni upigaji mwingine kisheria . Hakuna udhibiti kwenye Alam bila kuwa na uwezo Wa kuzima hilo gari Kwa njia ya mtandao na kumwadhibu Dereva huko huko mtandaoni kupitia miamala yake Binafsi.

Vinginevyo magari yanayotembea mchana yawe ni mchana tu na yanayotembea usiku yawe usiku tu. Na ya usiku Yote iwe ni lazima kufungwa vidhibiti mwendo.
 
Tatizo SIO Kutembea usiku tu lakini pia usalama Wa abiria wanapokua wanaendeshwa na Madereva wenye usingizi.
Nafikiri pangekua na utaratibu Wa kuwa na mapumzuko baada ya kuendesha masaa mtano matatu mpaka manne mfululizo wakati Wa usuki , Waafrika hua hawapumziki wanapotafuta pesa. MTU asiyepumzika ni hatari sana . Hata wasimamizi Wa SHERIA mara nyingi ni wakorofi sana kutokana na kufanya KAZI usiku na mchana bila kupumzika. Wakimkamata mtuhumiwa wanapiga mpaka kumaliza hasira zao na stress zao kwenye nafsi zao.
Kwa madereva wengi hua hawana muda Wa kupumzika kabisa iwe mchana au usiku. Wengine hawapumziki kutokana na KAZI nyingi na wengine kutokana na kutumia muda Wa kupumzika kwenye starehe za pombe na wanawake. Sasa wanapokua wanaendesha muda Mwingi wanakua na Hali ya uchovu na usingizi au kukosa utulivu Wa kuchukua maamuzi Sahihi wanapokua Barabarani.
Watu kama Hawa kuwaambia waendeshe magari usiku kucha ni hatari mno. Barabara Bado ni finyu Kwa magari Kutembea usiku kwani magari mengi hayana vizibiti mwendo.

VTS za LATRA ni upigaji mwingine kisheria . Hakuna udhibiti kwenye Alam bila kuwa na uwezo Wa kuzima hilo gari Kwa njia ya mtandao na kumwadhibu Dereva huko huko mtandaoni kupitia miamala yake Binafsi.

Vinginevyo magari yanayotembea mchana yawe ni mchana tu na yanayotembea usiku yawe usiku tu. Na ya usiku Yote iwe ni lazima kufungwa vidhibiti mwendo.
Mabasi ya route ndefu huwa yana madereva zaidi ya mmoja ambao huwa wanapokezana. Japo still ni risk lakini inawezekana.
 
Back
Top Bottom