Star TV walimwalika mbunge wa zamani wa CCM Mh. Leonard Derefa ili atoe maoni yake juu ya jinsi anavyoliona bunge la sasa leo asubuhi. Matumaini wa wanahabari hawa ni kupata negative feed back hali ikawa the other way round.
Derefa amesema kuwa anafurahia hili bunge kwa kuwa ni bunge la vyama vingi linalozungumzia issues na siyo siasa.
Akamponda Mchemba kwa jinsi anavyoleta U -CCM bungeni na kusahau majukumu yaliyomleta la kupigania maslahi ya wananchi waliomchagua.
Akamponda Anna Makinda (binti wa mkuu wa mkoa wa Tabora wa miaka ya 60) kuwa huenda amekuwa adicted na mfumo wa chama kimoja kwani amekuwa mbunge kwa takriban miaka 37 (tangia 1975). Amesema huenda mama bado anamtizamo wa kizamani.
Alimsifu Sita kuwa alikuwa akiliendesha bunge katika hali inayotakiwa ingawa CCM walimtoa kwa kuwa alikuwa hawabani wapinzani ipasavyo.
Mwandishi alipotaka kumpeleka mahali kwa kuponda wapinzani, mzee alichomoa na kuwasifia. Kuhusu matusi amesema hafurahii, ila kila mwanadamu ni mwendawazimu, ila inategemea ni jinsi gani ya ku m handle. Matusi yanakuja kama mtu anaona hapewi nafasi sahihi ya kusikika au kile anavyoona kinafaa hakitekelezeki. Na kwamba mbunge ana sheria zinazomlinda pale anaposema maneno makali.
Kuhusu vurugu, alisema haoni vurugu inayotokea ktk bunge letu. Amesema bunge la sasa linamsisimua, ni zuri lenye kila aina ya upinzani. Alisema mabunge mengine ya vyama vingi mtu anaingia bungeni na meno yake lakini akitoka bungeni ana mapengo kutokana na ngumi alizopigwa. Amesema watanzania wategemee vuguvugu hilo ndani ya bunge kwani ndiyo ukomavu wa kisiasa.