Ana frastulation za maisha
We kilaza umeandika nini hapa ndo hawa wa shule za kata!dah unawezakuta nili DC linaongoza watu wenye akili wakati yeye ni kiazi!:deadhorse:Ana frastulation za maisha
Star TV walimwalika mbunge wa zamani wa CCM Mh. Leonard Derefa ili atoe maoni yake juu ya jinsi anavyoliona bunge la sasa leo asubuhi. Matumaini wa wanahabari hawa ni kupata negative feed back hali ikawa the other way round.
Derefa amesema kuwa anafurahia hili bunge kwa kuwa ni bunge la vyama vingi linalozungumzia issues na siyo siasa.
Akamponda Mchemba kwa jinsi anavyoleta U -CCM bungeni na kusahau majukumu yaliyomleta la kupigania maslahi ya wananchi waliomchagua.
Akamponda Anna Makinda (binti wa mkuu wa mkoa wa Tabora wa miaka ya 60) kuwa huenda amekuwa adicted na mfumo wa chama kimoja kwani amekuwa mbunge kwa takriban miaka 37 (tangia 1975). Amesema huenda mama bado anamtizamo wa kizamani.
Alimsifu Sita kuwa alikuwa akiliendesha bunge katika hali inayotakiwa ingawa CCM walimtoa kwa kuwa alikuwa hawabani wapinzani ipasavyo.
Mwandishi alipotaka kumpeleka mahali kwa kuponda wapinzani, mzee alichomoa na kuwasifia. Kuhusu matusi amesema hafurahii, ila kila mwanadamu ni mwendawazimu, ila inategemea ni jinsi gani ya ku m handle. Matusi yanakuja kama mtu anaona hapewi nafasi sahihi ya kusikika au kile anavyoona kinafaa hakitekelezeki. Na kwamba mbunge ana sheria zinazomlinda pale anaposema maneno makali.
Kuhusu vurugu, alisema haoni vurugu inayotokea ktk bunge letu. Amesema bunge la sasa linamsisimua, ni zuri lenye kila aina ya upinzani. Alisema mabunge mengine ya vyama vingi mtu anaingia bungeni na meno yake lakini akitoka bungeni ana mapengo kutokana na ngumi alizopigwa. Amesema watanzania wategemee vuguvugu hilo ndani ya bunge kwani ndiyo ukomavu wa kisiasa.
mlengo wa kati unaona matatizo ya elimu za kata hayo? hata neno frustration linakushina? au wewe ndo umepata frustration baada ya kuona amewageuka?Ana frastulation za maisha
Mbunge mstaafu Derefa anajua anachokisema,hata enzi za ubunge wake alikuwa mwakilishi mzuri kwa wanashinyanga na aliwatetea vyema wakulima wa pamba,huyu na marehemu kabuye waliutumia vyema ubunge wao na walijipambanua kama watetezi wa wakulima na masikini,na si kama wanavyofanya akina mwigulu,serukamba,wassira,lukuvi n.k kwa kuweka mbele maslahi ya matumbo yao na watoto wao badala ya wanaowawakilisha.
Derefa si wa kudanganyika anafahamu nini anakisimamia si kama wanasiasa vijana na wazee wa leo wanaopotoka na kununuliwa kwa bei rahisi kwa sababu ya kuendekeza shida zao.Mzee kama Derefa anapoongea ukweli yatupasa tumpongeze na si kumkatisha tamaa kama wengine wanavyofanya.
Ana frastulation za maisha
hii ndio nini tena?
Star TV walimwalika mbunge wa zamani wa CCM Mh. Leonard Derefa ili atoe maoni yake juu ya jinsi anavyoliona bunge la sasa leo asubuhi. Matumaini wa wanahabari hawa ni kupata negative feed back hali ikawa the other way round.
Derefa amesema kuwa anafurahia hili bunge kwa kuwa ni bunge la vyama vingi linalozungumzia issues na siyo siasa.
Akamponda Mchemba kwa jinsi anavyoleta U -CCM bungeni na kusahau majukumu yaliyomleta la kupigania maslahi ya wananchi waliomchagua.
Akamponda Anna Makinda (binti wa mkuu wa mkoa wa Tabora wa miaka ya 60) kuwa huenda amekuwa adicted na mfumo wa chama kimoja kwani amekuwa mbunge kwa takriban miaka 37 (tangia 1975). Amesema huenda mama bado anamtizamo wa kizamani.
Alimsifu Sita kuwa alikuwa akiliendesha bunge katika hali inayotakiwa ingawa CCM walimtoa kwa kuwa alikuwa hawabani wapinzani ipasavyo.
Mwandishi alipotaka kumpeleka mahali kwa kuponda wapinzani, mzee alichomoa na kuwasifia. Kuhusu matusi amesema hafurahii, ila kila mwanadamu ni mwendawazimu, ila inategemea ni jinsi gani ya ku m handle. Matusi yanakuja kama mtu anaona hapewi nafasi sahihi ya kusikika au kile anavyoona kinafaa hakitekelezeki. Na kwamba mbunge ana sheria zinazomlinda pale anaposema maneno makali.
Kuhusu vurugu, alisema haoni vurugu inayotokea ktk bunge letu. Amesema bunge la sasa linamsisimua, ni zuri lenye kila aina ya upinzani. Alisema mabunge mengine ya vyama vingi mtu anaingia bungeni na meno yake lakini akitoka bungeni ana mapengo kutokana na ngumi alizopigwa. Amesema watanzania wategemee vuguvugu hilo ndani ya bunge kwani ndiyo ukomavu wa kisiasa.
Ana frastulation za maisha
Ana frastulation za maisha
Ana frastulation za maisha
Mwanaderefa hana njaa kama unavyodhani na ndio maana hayuko tayari kuandikishwa kwenye payment list ya kina Nape na Nchemba,nenda Shinyanga watakwambia kama ananjaa kama yako.Njaa inamsumbua huyo anapo ongea hapo hajielewi
Ana frastulation za maisha
Mwanaderefa hana njaa kama unavyodhani na ndio maana hayuko tayari kuandikishwa kwenye payment list ya kina Nape na Nchemba,nenda Shinyanga watakwambia kama ananjaa kama yako.
Tatizo Maccm hamtaki kuambiwa ukweli,hivi kwa mtu mwenye akili yake timamu kuna haja ya kubishana juu ya yaliyotokea bungeni?kama spika katangaza atakaetukana matusi atamwita polisi kesho yake Serukamba katukana mchana kweupe na kwa uwazi na alisikika kila kona,na alitukana bila kujali kuna wazee wa umri mkubwa sana pale wanastahili kuwa babu,bibi,mama na baba zake lakini pasipo aibu akatoa toa kali kama vile alikuwa amekaa kitaa,lakini Spika Makinda na mwenzie Ndugai kimyaaa kama vile Serukamba alikuwa anatoa pongezi.
Leo utaniambia nini niiamini CCM kuwa inatenda haki bungeni?utanishawishi vipi nikubali kuwa kiti cha spika kinatenda haki?
Ni wendawazimu kuamini hivyo hata kama umesoma mpaka vitabu vijikunja nasema ni ujinga na utaahira kuamini spkia makinda na ndugai wanatenda haki bungeni.