Mbunge Lema akamatwa na Polisi!

wakuu hii ni balaa There are currently 3537 users browsing this thread. (170 members and 3367 guests
 
Tunaomba updates na pia kama unajua sababu zozote za Llema kukamatwa
Soma alama za nyakati. Kama ujui lema kakamatwa kwa sababu gani. Basi wewe ni kilaza wa kutupwa. Wahehe atupo kama wewe, unatudhalilisha sana ndugu. Kila mtanzania anasubiri mageuzi 2015 sasa wewe endelea kujipendekeza itakukosti.
Serukambaa wewe
 
Pole Kamanda Lema.
Hakuna yasiyo kuwa na mwisho hata Mandela alipitia mazingira kama hayo na mwisho akawa Raisi muhimu mkono wa Mungu
.
 
kwa kweli walio karibu na lema wanatakiwa wamuweke kitako na kumshauri kuhusu mwendo anaenda nao. siasa sio ugomvi na kutengeneza matatizo kila siku

kuna njia nyingi za kupita kufanya siasa. hii njia aliochagua inashangaza sana tena sana. mbona kuna wabunge wengi wa chadema na vyama vyengine hawabehave kama yy? hata wenziwe mwisho watamchoka

Mktu umeweza kufuatilia mwanzo wa hili sakata then ndo uamue kuandika haya uliyoandika?
 
Pole sana makamanda. I wish i could be in TZ to get all what is trending now.

But good thing to believe, God is GOOOOOOOD!!!!!!!!!!!!!!!!

All the best GUYZ, we are going to be the champions soon.

 
huuuuuuu upuuzi sana kazi yote atakayo ifanya kama aliraise profile ya ccm kwa asilimia 20 huyu mkuu wa mkoa ameipeleka negative kabisa kwa mkoa wa arusha ......hivi ndio vitu vinavyowapa sifa chadema bila sababu ......mkuu wa mkoa alishindwa nini kujishusha na kuwapa pole sema tunashughulikia .......haya mambo yalitokea na mtwara pia upuuzi kweli aiseee
 
Kwenye nchi hii kukamatwa hakutegemei mtu kuwa na kosa la jinai. Kama ni hivyo Kamanda Kamuhanda angekuwa amekamatwa kwa kuwa tume ya haki za binadamu ilimuona amehusika katika mauaji ya Mwangosi. Akili ya kawaida inaweza kukutuma kuamini kuwa kushinda kwake ubunge na kauuli zake za hivi karibuni dhidi ya mkuu wa nchi zinatosha kuwafanya wasaidizi wake kumkamata. Kama tatizo ni yaliyotokea chuoni kulikuwa na sababu gani kwa mfano ya kulichukua gari lake kituoni? Na kama anahusishwa na vurugu za wanachuo ni mtu gani mwenye weledi wa kawaida tu asiyeona ukosefu wa kusoma saikolojia ya watu ulivyosababisha kauli za mkuu wa mkoa kuzua tafrani iliyotokea. Lema anachukiwa, Lema anawindwa, na wanaofanya hivyo wamekosa busara ya kufanya matendo hayo bila kujulikana. Nguvu inayotumika kwa Lema haifanani na kosa linalotajwa. Polisi wetu lini wataacha kushughulika mambo madogo ya kudhaniwa tu na kuanza kushughulikia mamabo halisi yenye ushahidi. Wameshindwa "kuwatambua" na kuwashughulikia wang'oa kucha na meno wa Ulimboka na Kibanda na kuanza kushughulikia video za kwenye Youtube, Wameacha kushughulikia vifo vyenye utata vya wanachuo wawili - (ambalo ndilo dai la wanachuo lililozua yote haya), wanamshughulikia Lema, kana kwamba hiyo ndiyo inayojibu hitaji la wanachuo. Kama wanachuo wasingezuiwa na Lema wakaandamana hadi kwa Mkuu wa mkoa wangekuwa na kosa lipi la kumkamatia Lema? Wangemkamata kwa sababu hakuwazuia waandamanaji? Au kwa kuwa mauaji yametokea kwenye eneo lake? Hawa viongozi wetu kwa nini wanatumia nguvu kubwa zaidi kwa mambo yenye sababu dhaifu na kuacha yenye sababu nzito zilizo wazi? Mungu ibariki Tanzania

na ailaani ccm na wanaoisapoti ktk nia zao mbaya
 
mengi , Naamini CCM na watendaji wake serikalini, Wakuu wa mikoa ambao muda si mrefu hatutawataka wawepo maana umuhimu wao haupo. Hiki cheo hakina Job descriptions tofauti na ile ya kuwinda wapinzani na kuua democrasia ktk nchi yetu. Ni lazima Cheo hiki kifutwe maana ni cheo kilicho na malengo ya kisiasa cha kupeleka taarifa zenye kufitinisha ikulu. The new constitution should stipulate clearly the kinds of appointee by the presida. Kamwe hatutaijenga nchi kwa kutumia vyombo vya usalama, watawala wetu wasipobadirika kuna siku nchi hii moto utawaka na vyombo hivyo vya dola hakika havitaweza kuuzima. Ngoja tuone mwisho wa uongozi huu wa kutumia mabavu. "Kwani huyu mama wa CCM ilikuwa ni lazima ashinde ubunge ndo arusha itulie???, je huyu mama mbona anawatesa watu wa Arusha na watanzania kwa ujumla" Tatizo naona ni yule mama kipenzi cha watawala wa leo kukosekana bungeni wakti kiti chake kilikuwa kimeandaliwa tayari. CCM na Serikali yako waache watu wapumue, msiwatese hiyo, na wakichoka mtajuta....


 
Nakubaliana na mchangiaji mmoja hapo juu kuwa yanatafutwa mazingira ya kuutoa uhai wa Lema,lakini hilo litakuwa ni suala la muda tu kwani maisha yao na ya watoto wao yatafuata mstari huo huo.Hamtaki kusemwa vibaya basi ishini inavyopaswa,kuweni waadilifu,kwisha hata akija mtu akaongea vibaya kukuhusu haitathibitika,jamani hizi ni zama zingine.
 
Kwenye Laptop Yake Zimekutwa Vidio Za Mipango Ya Kigaid,pamoja Na Siraha Yakivita Na Kofia Za Kininja Mia 2 Alikua Amepanga Kufanya 2kio Na Vijana Baaz Yao Alipanga Nao Mipango Hiyo Alipokua Jela Kisongo Na Ndo Mana Alikua Anapenda Kwenda Jela Kumbe Alikua Anaagenda Yake Ya Kigaid,naomba Polc Mcmwachie Gaid Huyo
Bado unahasira za kuuwawa kwa Osama Bin Laden.aliyemuua ni rais OBANA sio LEMA.Nakukumbusha tu.
 
Hakuna kitu kama hicho lema hajashika amani ya nchi

Pile sana. Mupumbavu Siku zote huwa hajui kama ni mupumbavu. Weledi wa mtu hupimwa na fikira zake.
Comment zako ni za kipuuzi sana. Na wenye akiri zao watakuona wewe Ni kama mtu aliyeamua kubadili jinsia yake. Tetea haki ya watanzania wa kesho na walio wadogo kwa sasa. Au ndo kupevuka?? Inasikitisha sana to see someone destroying the truth. Sifikiri kama Lema nimkorofi but CCM ndo mnaharibu inch
 
Back
Top Bottom