Mbunge Saashisha Mafuwe amlilia Katibu wake, Mwal. Benson Lema

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

Mbunge Saashisha Mafuwe Amlilia Katibu wake, Mwal. Benson Lema

Aliyekuwa Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Hai Mwl. Benson Lema azikwa kijijini kwao Nronga – Machame.

Mamia ya waombolezaji wakiongozwa na mbunge wa jimbo la Hai Saashisha Mafuwe wameshiriki katika ibada ya maziko ya aliyekuwa katibu wake na mwalimu mstaafu Benson Lema aliyeaga dunia Januari 2 2024 katika hospitali ya Machame huku wakimzungumzia kama mpenda maendeleo na mtu aliyejitoa katika jamii.

Akizungumza wakati wa zoezi la kuuaga mwili wa marehemu Mwalimu Benson Lema mbunge wa jimbo la Hai Saashisha Mafuwe amesema kuwa Mwl Benson Lema alikuwa kiungo mkubwa katika jamii na moja ya mtu aliyependa kujishusha na kuwa mfano wa kuigwa katika kila nafasi aliyotumika huku akimwelezea kama nguzo ya mtu aliyesimama katika mstari bora wa maadili na uongozi.

Saashisha amesema kuwa maisha ya Mwalimu Benson Lema yamefanyika baraka kwa jamii yake na kwamba ni wazee wachache wanaopenda jamii yao kwa dhati kwani katibu huyo alikuwa mwadilifu wa kweli na mtu asiyependa mzaa hasa katika utendaji wake wa kazi.

Akizungumza wakati wa ibada ya maziko ya Mwalimu Benson Lema yaliyofanyika hii leo katika usharika wa Nronga Machame Mchungaji Calvin Kessy wa usharika wa Uswaa aliyemwakilisha mkuu wa jimbo la Hai amesema kuwa Mwalimu Benson Lema aliishi maisha yenye maadili ambapo vijana wengi wa sasa wanashindwa kuyaishi hasa pale wanapoishi maisha ya kubweteka na kuwa tegemezi kwa wazazi wao.

Kwa upande wao baadhi ya waombolezaji waliotoa salamu za rambirambi wamemzungumzia mwalimu Benson Lema kama mmoja wa mtu aliyependa kutengeneza viongozi katika jamii huku akijitoa katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Hai katibu tawala wa wilaya ya Hai Sospeter Magonera amesema kuwa wilaya imepoteza mchapa kazi na mpenda maendeleo na kwamba alikuwa na busara na hekima na msaada kwa watu wengi.

Mwalimu Benson Lema alistaafu rasmi kazi ya ualimu mwaka 2014 na kisha mwaka 2020 Mbunge Saashisha Mafuwe alimuomba awe katibu wake, kazi aliyoifanya hadi umauti ulipomfika. BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-01-06 at 22.34.21.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-06 at 22.34.21.jpeg
    98.9 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-01-06 at 22.34.22(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-06 at 22.34.22(1).jpeg
    115.2 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-01-06 at 22.34.22.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-06 at 22.34.22.jpeg
    102.3 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-01-06 at 22.34.20.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-06 at 22.34.20.jpeg
    47.7 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-01-06 at 22.34.19.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-06 at 22.34.19.jpeg
    90.2 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-01-06 at 22.34.17.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-06 at 22.34.17.jpeg
    69.5 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-01-06 at 22.33.55.jpeg
    WhatsApp Image 2024-01-06 at 22.33.55.jpeg
    62.7 KB · Views: 2
Mbunge ulikosa vijana wenye uwezo na nguvu ya kukusaidia ukakimbilia wazee wa kulipwa posho badala ya Mshahara?

Hizo ni dalili za 2025 kuondoka!
 
Mbunge ulikosa vijana wenye uwezo na nguvu ya kukusaidia ukakimbilia wazee wa kulipwa posho badala ya Mshahara?

Hizo ni dalili za 2025 kuondoka!
Vijana wenye akili na busara hupenda kuwa karibu na wazee Ili wawaongoze vyema. Mh. Saasisha Mafuwe analijua na ndio maana haropokiropoki kama Godbless Lema!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom