MWANAMUZIKI nguli wa Hip hop Tanzania na Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Osmund Mbilinyi amewapa mwongozo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu ziara ya mwanamuziki nyota wa Hip hop Marekani, William Leonard Roberts II anayetambulika kama Rick Ross au The Boss, kwamba anastahili kulipa kodi kutokana na pato atakalaolingiza katika shoo yake ya leo.
Rick Ross atatumbuiza usiku wa leo katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012 kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam, ambalo linaandaliwa na Prime Time Promotions nakudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL).
Mbunge Mbilinyi ambaye anajulikana kwa majina ya kimuziki kama Mr II au Sugu, ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook;
"RICKY ROSS ANAKUJA, SAWA HAINA SHIDA, ILA TUNATAKA KUJUA AMELIPWA KIASI GANI NA ATAKATWA KIASI GANI KIBAKI KWENYE KODI YA TAIFA LETU KAMA AMBAVYO MIMI NIKIENDA KUFANYA SHOW/CONCERT MAREKANI NAKATWA KODI NA SERIKALI YAO"
Source:http://daresalaam-yetu.blogspot.com/2012/10/mbunge-sugu-ataka-tra-wamtoze-kodi-rick.html#.
****Nawasilisha****