Sugu aainisha baadhi ya mambo muhimu atakayopigania akiwa bungeni... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sugu aainisha baadhi ya mambo muhimu atakayopigania akiwa bungeni...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Smiles, Nov 12, 2010.

 1. Smiles

  Smiles JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 1,231
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mbunge wa Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mheshimiwa Joseph Mbilinyi ameainisha baadhi ya mambo muhimu ambayo atayapigania akiwa bungeni ikiwemo:
  • Kutumikia wananchi wa jimbo lake
   Sugu, ambaye pia anajulikana kwa majina ya utani ya `Mr II' au `II Proud', anasema asilimia 99 ya ajenda yake itakuwa kutatua matatizo ya wananchi wa Mbeya, ambao wana changamoto nyingi.
  Msanii huyo amewashukuru wananchi wa Mbeya kwa kuwa na imani naye na kuahidi kushughulikia matatizo yao ya barabara, elimu na afya katika kipindi cha miaka mitano ya ubunge.
  • Sheria ya Haki Miliki
   Anasema itakuwa ni sehemu kubwa ya majukumu yake lakini kuna mambo, ambayo angependa ayafanyie kazi ili asaidie kutatua matatizo ya sanaa ya muziki wa Bongo Fleva, ambao anakiri umemtoa kimaisha.
  Sugu anasema sheria ya Haki Miliki ina upungufu mkubwa unaofanya iwe ngumu kudhibiti wizi wa kazi za wasanii. Anatolea mfano wa adhabu zinazotolewa kwa wale wanaokamatwa wakidurufu kazi za wasanii kuwa hazijawekwa bayana.

  "Unajua hii sheria inaeleza adhabu ya juu tu (maximum' penalt) lakini haizungumzii adhabu ya chini (mininum penalt). Hii sheria inaeleaelea tu.

  "Hii inafanya kwa mfano mtu inapotokea mtu amejaza lori aina ya Fuso kazi za wasanii zenye thamani ya Sh. milioni 10 anaweza kutozwa faini ya sh. 200,000. Sheria hii haiko wazi," anaeleza Sugu, ambaye anahesabiwa kati ya waasisi wa Bongo Fleva kiasi cha kufikia kuitwa `Nyerere wa Rap'.
  • Anataka Cosota ipewe meno
   Sugu anasema angependa kuona Taasisi ya Kusimamia Haki Miliki (Cosota) ikiimarishwa ili iweze kuwajibika vizuri. Anadai Cosota kwa sasa ni taasisi ndogo kuweza kusimamia kazi za wasanii nchi nzima.
  "Moja ya mambo nitakayoshughulikia nikifika mjengoni (bungeni) ni kuona Cosota inapewa meno. Unajua tunafanya biashara nchi nzima lakini Cosota inayotakiwa kulinda kazi zetu hawana vitendea kazi vya kutosha na hata rasilimali watu," anaeleza Sugu, ambaye tangu ameanza mwaka 1994 amefyatua albamu 10.

  Anasema muziki unalipa kama wezi wa kazi za wasanii watadhibitiwa na kuongeza yeye alifanikiwa kimuziki baada ya kuamua kusimamia kazi zake mwenyewe na kuuza nakala zaidi ya 40,000 za albamu ya `Ndani ya Bongo' mwaka 1996.
  • TRA waweke alama kwenye kazi za wasanii
   Sugu anapendekeza kuwekwa kwa alama au stika za Mamlaka ya Kukusanya Mapato ya Kodi (TRA)kwenye kazi za wasanii ili kudhibiti wizi. Anatetea utaratibu huo kuwa ni mzuri kwani utasaidia Mamlaka ya Kukusanya Mapato ya Kodi (TRA) kuongeza wigo wa mapato na utadhibiti wenye tabia ya kudurufu kazi za wasanii.
  Anadokeza kuwa aliwahi kushirikiana na wasanii wengine wa Bongo Fleva na kupeleka mapendezo serikali tangu wakati wa uongozi wa awamu ya tatu nchini ya Benjamin Mkapa.

  "Tulipeleka maombi yetu mwaka 1995 kwenye Wizara ya Viwanda na Biashara na tuliambiwa maombi yetu yalikubaliwa lakini kukawa kuna urasimu. Kipindi Rais Jakaya Kikwete alipoingia madarakani mwaka 2005 tulipeleka tena maombi yetu, Waziri wa wakati ule Nazir Karamagi alikubaliana na ombi letu na akasaini.

  "Kilichobaki ilikuwa kuchapishwa kwenye Gazeti la serikali ili iwe sheria," anaeleza Sugu, ambaye anaongeza baada ya kufikia hatua hiyo walikuja kutaarifiwa faili lao liliibiwa kutoka meza ya Karamagi.

  • Mabadiliko ya Basata
   Sugu anasema kuwa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) linafanya kazi zake kizamani.
  Anaona linahitaji kufanyiwa mabadiliko kimuundo ili kufanya vizuri kazi zake za kusimamia na kuendeleza sanaa.

  Anasema kuna haja ya baraza hili kusambazwa nchi nzima kwani haoni mantiki ya msanii anayetoka mkoani kufunga safari Dar es Salaam kwa ajili ya kujisajili na anaeleza kuwa sanaa nchi nzima sasa inakuwaje Basata iwe Dar es Salaam pekee.
  Kuunganisha wasanii

  Sugu anaeleza itakuwa ngumu kwa wasanii kupigania haki zao bila ya kuwa kitu kimoja na ametaka wasanii hao kuwa na chombo cha kuwateta na atapigania kufufuliwa kwa Chama cha Wasanii wa muziki wa Kizazi Kipya (Tuma).

  Anaeleza kuwa chama hicho kilisajiliwa mwaka 2004 lakini kilishindwa kuibuka kutokana na wasanii wenyewe wa Bongo Fleva kukosa ushirikiano. Anasema atashirikiana na wabunge wengine kutetea wasanii lakini nao wanatakuwa kuwa kitu kimoja.

  Sugu anasema kitendo cha wasanii kukosa umoja ndio maana hata Rais Jakaya Kikwete alipotoshwa wakati alipotaka kusaidia wasanii wa Bongo Fleva. "Rais Kikwete kwa nia njema alitaka kutusaidia lakini kuna watu wakampotosha kuwa eti wasanii tunataka studio
  .
  "Kaka studio ziko kibao mtaani hadi zinakosa wasanii wa kurekodi," anasema Sugu, ambaye anamshauri Rais Kikwete kutengeneza mazingira mazuri ya wasanii kufanya kazi. Nitaandaa mikutano na matamasha ya kuwaunganisha wasanii. Siwezi kuacha harakati za muziki wa Bongo Fleva," anaeleza Sugu, ambaye amesema hatarudi jukwaani bali ataendeleza harakati za kupigania kuinua maisha ya wasanii ya kutumia njia nyingine.
   
 2. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Huyu ndiye Mr Sugu. Mmmh mwaka huu kuna mambo
   
 3. A

  Ashangedere Senior Member

  #3
  Nov 12, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Kilichobaki ilikuwa kuchapishwa kwenye Gazeti la serikali ili iwe sheria," anaeleza Sugu, ambaye anaongeza baada ya kufikia hatua hiyo walikuja kutaarifiwa faili lao liliibiwa kutoka meza ya Karamagi.

  Hii kweli kiinimacho, Sugu hakikisha faili linapatikana, Mambo gani haya!! EBoo
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kumbe huyu jamaa anaongea vitu vyenye akili eeeh..CCM bana si walimbeza sna alipokuwa anataka kugombea ...hahaaaa ..
   
 5. Gelange Vidunda

  Gelange Vidunda JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 312
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  "Wananiita Sugu! Wananiita Sugu, Sugu, Sugu!!!!"

  Go get them, soldier!!
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hapo natumaini atakuwa anawazungumzia wakina Ruge
   
 7. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  fanya kweli sugu 5yrs si mbali umetumwa na wana mbeya
   
Loading...