BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wafanyabiashara wa Ukonga, aliwaambia wananchi hao kuwa wanasalimiwa na Mbunge wao, ambaye pia ni waziri wa Ardhi, Jerry Slaa, lakini wananchi hao walionesha kutokubaliana na salamu hizo.
Baadhi ya wananchi walionesha kuwa wanataka kumuona, ambapo Ulega aliwaambia mbunge huyo atafika kuwasilimia. Japo hakueleza kwa nini kwa safari hiyo hakuja naye ambapo yeye ndio mbunge wa jimbo husika.
Katika Video hiyo hapo juu ni zaidi ya dakika nne Ulega amekuwa akitaka kuzitua salamu za Slaa kwa wananchi ambao wamegoma kupokea salamu hizo.