Singida ipo tayari kumpokea Rais Samia

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Peter Serukamba ameeleza namna ambavyo wananchi wa mkoa huo walivyojipanga kwa mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi mkoani Singida itakayoanza Oktoba 15, 2023.

Serukamba amesema wanatarajia kumpokea Mhe.Rais eneo la Sagala mpakani mwa mkoa wa Manyara na Singida na kuelekea moja kwa moja kuzindua shule ya msingi Imbele ambapo itazinduliwa ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa shule zilizojengwa kupitia mradi wa Boost, ambapo kwa upande wa elimu mwaka huu wa 2023 mkoani Singida Rais Samia ametoa kiasi cha shilingi Bilioni 9 ambazo zimetumika kujenga shule mpya 12, ukarabati wa madarasa, nyumba pamoja na Ofisi za walimu

Pia amesema, Rais ametoa shilingi Bilioni 3 kwa ajili ya upanuzi wa shule za sekondari zinazochukua wanafunzi wa kidato cha tano na sita

Mbali na Miradi hiyo ya elimu pia kuna miradi mingi ya kimkakati inayotekelezwa mkoani humo ambayo Mhe. Rais ataizindua ikiwemo mradi wa ujenzi wa Barabara ya Singida - Mbeya kipande cha km 56 kwa kiwango cha Lami, Ujenzi wa vituo viwili vya Polisi wilayani Ikungi na Mkalama, Ujenzi wa daraja wilayani Mkalama lililogharimu kiasi cha Bilioni 11, pamoja na kuzungumza na wananchi wa mkoa wa Singida katika mikutano ya hadhara

Katika ziara hiyo ya Mhe. Rais inayoanza kesho, pia Mhe. Rais atafungua mradi wa maji kutoka ziwa Victoria katika eneo la Shelui wilayani Iramba huku akitarajiwa kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi wa umeme vijijini mkoa wa Singida ambapo mkoa huo umepewa fedha takribani Bilioni 71 kwa ajili ya kupeleka umeme vijijini ambapo kwa taarifa iliyotolewa na mkuu huyo wa mkoa imeeleza kuwa kufikia mwaka 2024 kila kijiji kitakuwa kimepata umeme mkoani Singida.

Katika hatua nyingine Serukamba amesema kuwa ili kudhihirisha furaha waliyonayo wakazi wa mkoa huo kwa Raisa Samia Suluhu Hassan leo wanatarajia kukesha eneo la Sagala wakimsubiri, mkesha ambao umetanguliwa na maandamano yaliyofanywa na vijana wakiwemo Bodaboda wa mkoa huo

Aidha, Serukamba amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameacha deni kubwa kwa wakazi wa mkoa wa Singida, deni ambalo linatarajia kulipwa mwakani 2024 na mwaka 2025.

255739828236_status_62dc7c4bab474841b15ce906e50996f5.jpg
FB_IMG_1697201061703.jpg
IMG-20231012-WA0001.jpg
 
Back
Top Bottom