Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 674
Mbunge aswekwa ndani
Waandishi Wetu
Daily News; Tuesday,February 26, 2008 @20:01
MBUNGE wa Magu Mjini ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Festus Limbu, jana alishikiliwa kwa saa kadhaa katika kituo cha Polisi cha Oysterbay Dar es Salaam baada ya kusababisha ajali barabarani.
Chanzo chetu cha habari kilidai kuwa sambamba na Mbunge huyo kugonga gari lililokuwa mbele yake pia alimkunja askari wa Usalama Barabarani aliyefika eneo la ajali hadi ikabidi mgambo wa Jiji waingilie kati na kumpeleka kituo cha Polisi.
Tukio hilo lilitokea saa mbili asubuhi katika barabara ya Bagamoyo eneo la kituo cha mabasi cha Mbuyuni ambako Mbunge huyo inasemekana alishindwa kulizuia gari lake karibu na taa za kuongozea magari na kuligonga gari lililokuwa mbele yake ambalo nalo lililigonga gari jingine.
Baada ya kutokea ajali hiyo askari wa Usalama Barabarani (jina tunalo) aliyekuwa eneo hilo alikwenda kuangalia tukio hilo kujua chanzo na kuchukua taarifa muhimu za tukio zima. Askari huyo alipofika hapo, Mbunge huyo alimkunja akitaka kumpiga hali iliyowashtusha askari wa Jiji waliokuwa kwenye gari lao katika eneo hilo ambao walishuka kwenda kutoa msaada.
Walipofika pale kuona raia kamkwida na kumkunja trafiki, walimkamata Limbu, wakamwingiza kwenye gari lao na kumfikisha katika kituo cha Polisi, kilisema chanzo cha habari. Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha alikwenda kituoni hapo kufuatilia tukio hilo na baadaye Limbu aliachiwa kwa dhamana yake mwenyewe.
Limbu alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alikiri kutokea ajali hiyo na kudai kuwa gari lililokuwa mbele yake lilifunga breki ghafla hali iliyomfanya yeye ashindwe kufunga breki na kusababisha ajali.
Alikanusha kumkaba askari wa Usalama Barabarani wala kufungwa pingu na kuongeza; Baada ya ajali ilikuja break down na kuyachukua magari yaliyopata ajali ambako la mwenzangu liliumia sikufungwa pingu wala Masha hakuja kituoni, lile ni suala la trafiki.
Kwa upande wake Waziri Masha licha ya kukiri kutokea kwa ajali hiyo alisema akiwa karibu na eneo hilo akielekea ofisini kwake, alipigiwa simu na Mbunge wa Geita, Ernest Mabina kuhusu ajali hiyo na ndipo alipokwenda kituoni hapo.
Nilikwenda kituoni kumwangalia Mbunge mwenzangu lakini sikwenda kumuwekea dhamana. Nilipofika pale nilikuta RTO (Mkuu wa Usalama barabarani wa Mkoa) akizungumza na Limbu na kweli niliona kuna hali ya ajali ingawa sijaliona gari lenyewe. RTO aliniambia analishughulikia vizuri suala hilo. Basi nami nikamwambia alishughulikie vizuri kwa mujibu wa taratibu na nikaondoka, alisema Waziri Masha.