Nashauri safari za mabasi kutembea saa 24 zisitishwe, vifo vitamaliza watu

chamaclotus

JF-Expert Member
Apr 19, 2019
971
1,969
Kwema wakuu?

Kwa Hali ilivyo usalama barabarani nyakati za usiku ni mdogo madereva hawazingatii Sheria barabarani wakati wa usiku maana hamna Oolisi. Malori nayo ndio mida yao ya kukimbia so ajali ni nyingi mno. Madereva pia usiku wanasinzia barabarani sababu ya uchovu.

Kuna siku nimesafiri na basi la Frester kwenda Dar es Salaam, kufika Morogoro usiku kama saa nane, dereva anataka kugonga semi za mafuta sababu ana overtake pia hamna Polisi barabarani.

Hivyo hivyo gari la Abood juzi tumetoka Dar dereva anaendesha kwa kasi pia tulilipanda pale Mbezi saa kumi na moja alfajiri gari halikufanyiwa service maana ilikuwa inatoka mkoani na watu wanashuka pale Mbezi na sisi tunapanda sababu hawana muda wa service.

Chonde chonde Serikali sitisheni hizi safari.

NB: Hata ajali mchana zinatokea lakini chanzo hasa ni madereva kuendesha magari usiku so wanachoka wanakosa focus ya kuendesha mchana na kupelekea kupata ajali
 
Gari lingekua lako ungefanya service ukifika dar na ukifika moro unafanya ungeweza. Mbona unaongea vitu vya ajabu sana.

Gari hizo zina ratba yake ya service sio kila siku. Unadhani service ni kuweka mafuta. Unajua ifike mahali wana jf kama hujui uliza.. Gari hujawahi miliki unaanza leta stry za service every return day. Daah
 
Inaonekana huna uelewa au hujui unachokiandika mpaka serikali imeruhusu safari za usiku walishafanya tathmini maaskari wa usalama wapo barabarani kama kawa madereva wanafuata sheria hizo lori unazosema zinakimbia mbona hatupewi taarifa kila siku kwamba zimepata ajali? Mwezi huu kna ajali ngapi umzisikia za usiku?

Ww kama huna harakati zinazohitaji kusafiri usiku tulia tu mkuu watu wamepata nafuu sana Kwa safari z usiku ndio maana unaona bado mabasi yanafanya kazi mbali na hapo ajali haina kinga inatokea muda wowote
 
Gari lingekua lako ungefanya service ukifika dar na ukifika moro unafanya ungeweza. Mbona unaongea vitu vya ajabu sana.
Gari hizo zina ratba yake ya service sio kila siku. Unadhani service ni kuweka mafuta.
Unajua ifike mahali wana jf kama hujui uliza.. Gari hujawahi miliki unaanza leta stry za service every return day. Daah
Usijifanye mjuaji mkuu service hazifanyiki za kueleweka yaani service ifanyike morogoro, wakijitahidi ni dakika kumi maana wanawashusha abiria ili wakachimbe dawa.
 
Inaonekana huna uelewa au hujui unachokiandika mpaka serikali imeruhusu safari za usiku walishafanya tathmini maaskari wa usalama wapo barabarani kama kawa madereva wanafuata sheria hizo lori unazosema zinakimbia mbona hatupewi taarifa kila siku kwamba zimepata ajali? Mwezi huu kna ajali ngapi umzisikia za usiku?

Ww kama huna harakati zinazohitaji kusafiri usiku tulia tu mkuu watu wamepata nafuu sana Kwa safari z usiku ndio maana unaona bado mabasi yanafanya kazi mbali na hapo ajali haina kinga inatokea muda wowote
Haya kwa bongo bado muda utaongea
 
Usijifanye mjuaji mkuu service hazifanyiki za kueleweka yaani service ifanyike morogoro, wakijitahidi ni dakika kumi maana wanawashusha abiria ili wakachimbe dawa
Hizi fani na ni kazi za watu na huwezi kuwa unajua kila kitu. Hata dakika 2 zinatosha kufanya unachoita service. Inategemea ni kitu gani kinafanyika. Pia gari alifanywi service kila siku
 
Back
Top Bottom