Mbunge ailipua Mohamed Enterprises Bungeni

Mohamed Enterprises ni kampuni hatari sana Tanzania. Ni hatari kama kina Rostam Aziz, Yusuf Manji na Tanil Somaiya. ..............

maeneo ya Las Vegas.............tunawaita............ "High Rollers"
 
Tanzania ina listi ya mafisadi hatari sana wenye asili ya kigeni ambao wamewaweka waandishi karibu wote kwenye mfuko. Pia vyombo vya dola na viongozi wengi (mpaka wa upinzani) wanahongwa na hawa jamaa. Wakiona mtu yeyote anawabughudhi wako tayari kuhonga fedha nyingi ili wamnunue au wamuangamize. Hawa mafisadi wanajua namna na kunyemelea na kukwapua raslimali za nchi.... ole wao ole wao ole wao. Yana mwisho....
1. Roztam aziz
2. Yususf Manji
3. Mohamed enterprises
4. Tania Somaia.
Hili ni listi ya hatari sana. Ole wao ole wao.....ole wao..... siku isiyo na jina yaja...

Umemsahau Subhash Patel huyu ndie alikuwa kinara wa kukusanya mabilioni toka kwa Wahindi wenzie ili yatumike na mtandao katika kuhakikisha Kikwete anaingia Ikulu 2005 yupo pia mwingine kwa jina maarufu la Jitu (Jeetu)
 
Kwani kalazimisha kuuziwa, serikali ndiyo inayoleta umaskini kwa kuua vyama vya ushirika halafu lawama mnamtupia mwingine. Dewji ni mfanyabiashara na ili ufanikiwe unahitaji faida regardless inatoka wapi, kwanza nadhani wakulima wanashukuru Dewji ananunua otherwise ingewaozea, au bunge lina uwezo wa kununua?

Unachosema ni kweli mtumpu hasa kama TZ pangekua uwanja wa haki. Mohamed Enterprise amemonopolize biashara na anatumia uwezo wake wa kipesa kulinda hiyo monopoly kwa njia yeyote. Ninachosema ni kua kama utataka kufanya biashara ya ku export ufuta ama Korosho toka TZ si rahisi kwa kuwa kuna wenye monopoly. Kuna vijiji unaweza hata pigwa ukienda kufuata ufuta.
 
Mwisho wa siku anawapa maticha fifty fifty anaonekana wa maana kumbe hiyo hela kawaibia hao hao.
 
Huyu jamaa ni fisadi kweli huwa anapakiaga nafaka hasa mahindi kwenda rwanda na burundi na huwa halipii kodi yeyote anadai ni ya msaada.
 
Salaam kutoka Dodoma,

Nimeamua kuileta habari hii humu JF kwani vyombo vyote vya habari Tanzania viko mfukoni mwa Gullam Dewji, mwenyekiti wa Mohamed Enterprises, pamoja na mtoto wake, Mbunge Mohamed Dewji. Kwa masikitiko makubwa sana, najua nikiipeleka habari hii newsroom kwetu Mhariri Mtendaji wetu haiwezi kuitoa habari hii. Sijui na humu JF hii post haitaondolewa?

Mimi naona huyo mbunge ana hoja ya msingi ila ameshindwa kuainisha kiini cha matatizo. Malengo ya mfanyabiashara yoyote ni kupata faida kubwa kadri inavyowezekana (maximize profit). Mfanyabiashara hawezi kubadili malengo hayo kwa sababu tu amefanikiwa kununua uwakilishi wa wananchi na kuitwa "Mheshimiwa Mbunge". Kimsingi wananunua uwakilishi ili kufanikisha malengo yao ya kibiashara ya kupata faida kubwa kadri inavyowezekana huku wakilindwa na nguzo mojawapo ya dola.

Kwa hiyo wanachofanya Mohamed Enterprises ni sahihi kabisa kwa mujibu wa sheria na malengo yao ya kibiahsara hasa ukizingatia kuwa hawajawahi kuwashurutisha hao wakulima ili wauze mazao yao kwa bei chee. Sijawahi kusikia wakulima wameuza mazao huku wakiwa wamewekewa bastola vichwani. Na hata kama wangeuza AGOA badala ya India bado faida ingekwenda kwa Kampuni na siyo kwa Mkulima.

Suala la msingi hapa la kujiuliza ni je serikali imeandaa utaratibu gani kuwalinda wakulima wadogo hawa ili wasihujumiwe na wafanyabiashara (sio Mohamed Enterprise peke yake) wenye malengo ya kupata faida kubwa? Wote tunajua kuwa vyama vya ushirika ni vichaka vya wezi na uwepo wa wafanyabiashara umewasaidia kwa kiasi kikubwa wakulima walau kupata sehemu ya kuuza mazao yao. Hivyo badala ya kumlaumu mfanyabiashara huyu mwakilishi angemshukuru kwa kutoa soko la korosho za wakulima. Kwani vinginevyo hayo mazao yao yangeishia kuharibikia shambani tu.
 
What about wanavyochakachua mizani ili kilo moja na nusu ya ufuta isomeke kama kilo moja nalo linahalalishwaje?...
 
MO ni mbunge wa Singida. Sijawahi kumsikia akiwasemea jambo lolote wananchi wa singida bungeni.
Sijui ni mwakilishi wa wananchi au mfadhili wananchi.

Wanachi wa Singida amkeni jamani.
 
Mimi naona huyo mbunge ana hoja ya msingi ila ameshindwa kuainisha kiini cha matatizo. Malengo ya mfanyabiashara yoyote ni kupata faida kubwa kadri inavyowezekana (maximize profit). Mfanyabiashara hawezi kubadili malengo hayo kwa sababu tu amefanikiwa kununua uwakilishi wa wananchi na kuitwa "Mheshimiwa Mbunge". Kimsingi wananunua uwakilishi ili kufanikisha malengo yao ya kibiashara ya kupata faida kubwa kadri inavyowezekana huku wakilindwa na nguzo mojawapo ya dola.

Kwa hiyo wanachofanya Mohamed Enterprises ni sahihi kabisa kwa mujibu wa sheria na malengo yao ya kibiahsara hasa ukizingatia kuwa hawajawahi kuwashurutisha hao wakulima ili wauze mazao yao kwa bei chee. Sijawahi kusikia wakulima wameuza mazao huku wakiwa wamewekewa bastola vichwani. Na hata kama wangeuza AGOA badala ya India bado faida ingekwenda kwa Kampuni na siyo kwa Mkulima.

Suala la msingi hapa la kujiuliza ni je serikali imeandaa utaratibu gani kuwalinda wakulima wadogo hawa ili wasihujumiwe na wafanyabiashara (sio Mohamed Enterprise peke yake) wenye malengo ya kupata faida kubwa? Wote tunajua kuwa vyama vya ushirika ni vichaka vya wezi na uwepo wa wafanyabiashara umewasaidia kwa kiasi kikubwa wakulima walau kupata sehemu ya kuuza mazao yao. Hivyo badala ya kumlaumu mfanyabiashara huyu mwakilishi angemshukuru kwa kutoa soko la korosho za wakulima. Kwani vinginevyo hayo mazao yao yangeishia kuharibikia shambani tu.

Mchango wa serikali ni mdogo au upo tu kwenye makabrashi tu.Ukiuza korosho iliobanguliwa utapata bei nzuri zaidi,lakini viwanda vya kubangulia korosho alivyojenga Mwl Nyerere havitumiwi vimekufa.Maganda ya korosho yangeweza kutoa byproduts nyingine kama kuzalisha umeme au kukamuliwa na kutoa aina za mafuta yatumikayo kwenye mitambo kama hydraulic oils nk.Lakini inauzwa korosho ikiwa malighafi ni sawa na bure.
Kwani kama kawaida ya serikali yetu kujifanya wanajua kila jambo lakini matendo ni kinyume.Ni aibu kuuza 13 ml $ kwenye AGOA wakati jirani yako anauza 200 ml $.
 
Na huyu sasa inabidi afuate nyayo kama tulivyo kwisha muombea...!!
 
MO anawadanganya sana watu wa singida...hana uchungu nao hata kidogo kwani kachukua ubunge ili kurahisisha mambo yake.

Haswaaaa Mkuu! Hapo umenena. Anapokuwa bungeni anawakilisha Kampuni yake na si wapiga kura wake... Umewahi kumsikia akichangia hoja bungeni?
 
Who is to blame? The farmers/sellers or buyers?

Inategemea na akili ya anayetaka kulaum na thamani yake, kama ni mtu wa njaa na akili za tumboni wakulaumiwa ni Mkulima, kama ni mtu mwenye weledi, utu na hasiye na bei katika soko la Ufisadi lazima MO alaumiwe ndiye wakulaumiwa na ndio maana wanaingia Bungeni ilikupatanafasi ya kununu viongozi wetu wabovu kwa maslahi ya kutengeneza faida kubwa.

Wanapo twambia anafanya biashara tulitakiwa tujuwe analipa kodi kiasi gani kwa mwaka, au ndio mlolongo wa misamaha ya kodi? na kwanini wakulima hawapati faida? pia kuna maswali marahisi kama kwa mwaka anasaidia kiasi gani wakulima?

Hiyo kenya wanayojilinganisha nayo wamevuka mipaka mingi sasa wakitaka kuiga kutoka kenya wasiige kuuza bidhaa tu nje, aige na katiba mpya maana kama siasa ni chafu hakuna biashara itafanyika safi ndani nchni!
 
Mkuu Arafat nadhani hapo ulipogusa ndio penyewe haswaaa. Hivi vingine binafsi naviona kama ni vichekesho kwa kweli. Hivi sisi tunapata wapi jeuri ya kujilinganisha na Kenya wakati mambo yetu ni mizaha tu kila kona? Ni nani amesema mafanikio yanadondoka toka mbinguni kama mana? Hivi vitu ni matokeo ya ufanisi kwenye nyanja zingine (cause & effect) hayaji tu kwa kuwa umetaka yaje. Wenzetu Kenya wana serikali na rais makini of course ufisadi upo pia lakini kazi pia wanapiga hasa. Kama unafuatilia jinsi wanavyoendesha mambo yao wala hutashangaa wanapofanikiwa. Arafat umetaja katiba, na huyo naibu waziri mwenye vyeti fake ametaja AGOA lakini ni ukweli unaouma (sad fact) kwamba Kenya wametuzidi karibu maeneo yote (utalii, mazao, viwanda etc) kimapato wakati sisi tumewazidi kila eneo resources wise. Kwa hiyo mambo yako kinyume, yule mwenye rasilimali kachoka (TZ) na asiye na rasilimali (Kenya) mambo mazuri kabisa. Kwanini mimi sijui huenda kikwete na serikali yake wanajua sababu.
 
Na huyu sasa inabidi afuate nyayo kama tulivyo kwisha muombea...!!
dewiji ni hatari sana kwa maendeleo ya uchumi na demokrasia mkoani singida, naamini ndiye amewafanya wanyaturu pale singida wameanza kuwa kama omba omba vile, wanasubiri akija dewiji anagawa hela za bure, anamtumia mazala kugawa hizo hela, kwa kuwa tunakubaliana mfanyabiashara hutafuta faida mara zote, fedha anazozigawa dewiji anatumia kanuni ipi ya biashara. akishidwa kufanya kama rostam, basi awajibishwe!!!!!!
 
Back
Top Bottom