Mbunge ailipua Mohamed Enterprises Bungeni

Mbunge ailipua Mohamed Enterprises Bungeni

Hizi kampuni zimewakamata sawasawa viongozi wakubwa wa nchi hii kiasi kwamba hawaoni sababu yoyote ya kuhoji kinachoendelea ndani ya kampuni hizo. Kampuni hizi zikae zikijua watanzania wanaona jinsi rasilimali zao zikihujumiwa na kutoa viji-misaada visivyo na kichwa wala miguu. Iko siku kitaeleweka.
Duh
 
Yeye kama mfanya biashara hawezi kuingia kwenye biashara ya hasara. Moja ya vitu vinavyoturudisha nyuma nchi hii ni kuwalaumu waliofanikiwa kwa matatizo yetu. Mheshimiwa mbunge alitakiwa achangamkie fursa ya soko la agoa kuliko kumtupia lawama Metel. Mfano sasa hivi tuna viwanda vingi vya juice na bei wanazonunua matunda ni ndogo mno, hatuwezi kuwalaumu kwa kununua matunda yetu kwa bei ndogo wakati wamejenga viwanda vyao ili wapate faida.

Nimeona mh mbunge ametoa mfano mfu wa kujilinganisha na kenya wakati kila zao tunalozalisha na kenya wakazalisha wanaonekana kuongoza kwa mauzo kuliko sisi, angalia takwimu za mauzo ya nje ya maparachichi, maembe, machungwa, mananasi na hata tanzanite(inayopatikana kwetu tu) wanatuzidi kwa mauzo.
fact mkuu...ulikuwa uzembe wa serikali kutokubuni sera zitakazonufaisha mkulima. mfanyabiashara anaangalia fursa mda wote...he use your fool 2 gain profit... profit oriented... that's all....tuwe wakwel hata sisi tungechungulia huu mchongo tungepiga.
 
Tanzania ina listi ya mafisadi hatari sana wenye asili ya kigeni ambao wamewaweka waandishi karibu wote kwenye mfuko. Pia vyombo vya dola na viongozi wengi (mpaka wa upinzani) wanahongwa na hawa jamaa. Wakiona mtu yeyote anawabughudhi wako tayari kuhonga fedha nyingi ili wamnunue au wamuangamize. Hawa mafisadi wanajua namna na kunyemelea na kukwapua raslimali za nchi.... ole wao ole wao ole wao. Yana mwisho....
1. Roztam aziz
2. Yususf Manji
3. Mohamed enterprises
4. Tania Somaia.
Hili ni listi ya hatari sana. Ole wao ole wao.....ole wao..... siku isiyo na jina yaja...
Mhm
 
dewiji ni hatari sana kwa maendeleo ya uchumi na demokrasia mkoani singida, naamini ndiye amewafanya wanyaturu pale singida wameanza kuwa kama omba omba vile, wanasubiri akija dewiji anagawa hela za bure, anamtumia mazala kugawa hizo hela, kwa kuwa tunakubaliana mfanyabiashara hutafuta faida mara zote, fedha anazozigawa dewiji anatumia kanuni ipi ya biashara. akishidwa kufanya kama rostam, basi awajibishwe!!!!!!
Ok
 
Ina maana ndio mmeifanyia kazi post hii? Mimi sikushauri mumteke!!

Kwa kuwa mmeamua kuteka
Mtekeni basi na yule aliyeuza nyumba za serikali maana nilitoa hadhari pia.
 
Salaam kutoka Dodoma,

Nimeamua kuileta habari hii humu JF kwani vyombo vyote vya habari Tanzania viko mfukoni mwa Gullam Dewji, mwenyekiti wa Mohamed Enterprises, pamoja na mtoto wake, Mbunge Mohamed Dewji. Kwa masikitiko makubwa sana, najua nikiipeleka habari hii newsroom kwetu Mhariri Mtendaji wetu haiwezi kuitoa habari hii. Sijui na humu JF hii post haitaondolewa?
Mbona hukusema tangu awali kabla ya kutekwa kwake
 
Ina maana ndio mmeifanyia kazi post hii? Mimi sikushauri mumteke!!

Kwa kuwa mmeamua kuteka
Mtekeni basi na yule aliyeuza nyumba za serikali maana nilitoa hadhari pia.
Watu wengine bwana.
 
Huyu bwana anayeitwa Masoud Nasser ambaye imedaiwa kuwa amepewa mamlaka na Serikali ya Libya kusimamia deni la chi hiyo hapa Tanzania, wiki iliyipita alikana kwa kiapo alichokitoa mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu kwa usimamizi wa Wakili Majura. Katika kiapo hicho hich Bwana Masoud anakana kabisa kupewa mamlaka hayo toka Serikali ya Libya. Aliendelea kuapa kwa kusema kuwa documents alizo saini ni batili na alifanya hivyo kwa KULAZIMISHWA na akina Dewji ambao walimtishia kuwa asipofanya hivyo maisha yake yatakuwa hatarini.
Aliyasema yote haya mahakamani?
 
Back
Top Bottom