Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,189
- 128,277
Amebaki Musiba tu kupewa huu Udokta.
Hao hawajajipamba, waliojipamba ni akina Dr Mwaka, Babu Tale na wenzake kina Jakaya kuna vyuo ndiyo vimewapa tittle hizo iwe tunapenda au hatupendi.Kwa hiyo Dkt ya ubongo ijulikane haina thamani, sivyo?? Maana yeyeote anaruhusiwa kujipamba anavyotaka (pamoja na hao maaskofu, manabii, mitume na kadhalika...)
pesa ni sawa na semesters 😝😝😝😝Kweli tutafute pesa
Ni vyema kuwapongeza Hawa wafanya biashara maana hata uwe na PhD ya biashara hauwezi kuwa na brain ya abood kufanya biashara utaishia kufundisha chuo tu. Hata uwe na PhD yamusic na utamaduni hauwezi kuwa diamond , Leo hii diamond akienda kufundisha darasa la PhD ya music ataeleweka kuliko profesa wa music , Msukuma ok! Babutale sielewi anamchango upi.Mhe Abdulaziz M. Abood, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udakitari kwa kutambua mchango wake katika uongozi na kuisaidia jamii.
Kuanzia sasa atafahamika kwa jina la Dkt. Abdulaziz M. Abood.
Mchango wa Dkt. Abood kwa wananchi wa Morogoro hauna mashaka hata kidogo na amekuwa akijidhihirisha hivyo kupitia kazi zake kama Mbunge na misaada binafsi ambayo amekuwa akiitoa kwa wananchi wake.
Hongera sana Dkt. Abood. Unastahili!
------
TAARIFA ZAIDI
Ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini na mfanyabiashara maarufu wa usafirishaji nchini Abdulaziz Abood ambaye ametunukiwa Udaktari wa Heshima na taasisi ya Academy of University Global Peace ya nchini Marekani.
Kwahiyo rasmi ukitaka kumuita kuanzia leo usimwite Abood, ni sharti uanze na Mheshimiwa Dkt Abdulaziz Abood ukimaanisha kutambua heshima aliyotunukiwa kutokana na uongozi thabiti katika mambo mbalimbali ya kijamii.
Sherehe za kumtunuku Dkt Abood udaktari huo zimefanyika jijini Dar es Salaam ambapo watanzania wengine kadhaa wamepewa heshima hiyo.
Dkt Abood ni mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini kwa takribani vipindi vitatu na amekuwa na mafanikio mengi katika nyanja mbalimbali kwa wananchi wa jimbo lake.
View attachment 2497939
Alishirikiana na aliyekuwa RPC kuiba kuraHuyo Abood kafanya nn kwenye jimbo lake?
Kwa haya uliyoandika utakuwa miongoni mwa mlionunua vyeti. Aliyekwmbaia degree ya heshima inasomewa nani?Kumekucha kumekucha, nakumbuka mstari mmoja kwenye wimbo wa langa "sasa yanini kusoma wakati elimu inauzwa."
Watu wanachangamya sana kuhusu tuzo za falsafa ya udaktari, hizo hutolewa kwa heshima ya kutambua mchango wa mtu fulani katika nyanja fulani ya kijamii ama kiuchumi, na wala hazina uhusiano wowote ule na zile shahada za kitaaluma za uzamivu.Hivi hizi degree za heshima ni PhD? Kuna kitu tunachanganya. Honorary degree sio PhD wandugu..
Sio tutafute madaraka?Kweli tutafute pesa
Ukiwa una ufinyu na uvivu wa fikra na kujitafakari ili nawe upige hatua utabaki kumsema aliyefanikiwa .Alishirikiana na aliyekuwa RPC kuiba kura
Watu wanachangamya sana kuhusu tuzo za falsafa ya udaktari, hizo hutolewa kwa heshima ya kutambua mchango wa mtu fulani katika nyanja fulani ya kijamii ama kiuchumi, na wala hazina uhusiano wowote ule na zile shahada za kitaaluma za uzamivu.
Diamond Kuna kitu alichotunukiwa na UD sikumbuki ni niniZinatoka mara moja tu kwa mwaka baada ya tathmini kufanyika. Na ukifuatilia, wote wanaopewa wanastahili.
Mfano siku moja akipewa msanii Diamond Platnumz utaona hastahili?
Binafsi naona ni jambo jema kuwatambua watu wanaofanya mambo makubwa kwenye jamii na kuwapa heshima.
Nyie ndio msiotaka kuambiwa ukweli, hatukatai kufaniliwa Ila fanikiwa kwa njia halali basi, ubunge wake ni magumashi matupu, kachukua viwanda serikalini anafugia mbuziUkiwa una ufinyu na uvivu wa fikra na kujitafakari ili nawe upige hatua utabaki kumsema aliyefanikiwa .
Ulichokiandika kila mtu anaweza kuandika. Uthibitisho uko wapi?
Na zile zinazotolewa na chuo chetu UDSM bei yake ikoje mkuu?
Je, zile zinazotolewa na Oxford, Harvard, Cambridge nazo una bei zake?
Sent from my SM-E135F using JamiiForums mobile app
www.chubmagazine.com
Utakuwa wa Chennai India , ambapo address ya hicho chuo kilichoa hizo PhD inasomekaMhindi yupi huyo mkuu?
Si halali kwako kwa wanaotambua mchango wake ndio kapewa sasa nyamaza uangalie familia yako .kwani hicho cheti kitamfanya ashibe. Always lazy minds discuss people . Wewe kapata hakupata inakupa shida gani .Nyie ndio msiotaka kuambiwa ukweli, hatukatai kufaniliwa Ila fanikiwa kwa njia halali basi, ubunge wake ni magumashi matupu, kachukua viwanda serikalini anafugia mbuzi
Ndio kama wanaomsifia abood ambaye anatumia fedha za urithi kutokana na biashara haramu ya Meno ya temboMnapenda sana kumsifa huyo Dogo wa NALA utafikiri kapambana kinoma.
Wakati Jamaa aatumia pesa za baba yake anazokamua waumini wake.
Duh..Mh alipata Zero form 4 Forest Hill secondary school morogoro..hongera yake
Kwanini wasifanye mpango wakawatunuku wabunge wote tu kwa ujumla, kwa kutambua mchango wao mkubwa katika kutuletea maendeleo? Ili pia badala tu ya kuitwa waheshimiwa, kila Mbunge sasa awe anaitwa "Mheshimiwa Dokta..."
Au nakosea ndugu zangu?