Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,096
Mhe Abdulaziz M. Abood, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udakitari kwa kutambua mchango wake katika uongozi na kuisaidia jamii.
Kuanzia sasa atafahamika kwa jina la Dkt. Abdulaziz M. Abood.
Mchango wa Dkt. Abood kwa wananchi wa Morogoro hauna mashaka hata kidogo na amekuwa akijidhihirisha hivyo kupitia kazi zake kama Mbunge na misaada binafsi ambayo amekuwa akiitoa kwa wananchi wake.
Hongera sana Dkt. Abood. Unastahili!
------
TAARIFA ZAIDI
Ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini na mfanyabiashara maarufu wa usafirishaji nchini Abdulaziz Abood ambaye ametunukiwa Udaktari wa Heshima na taasisi ya Academy of University Global Peace ya nchini Marekani.
Kwahiyo rasmi ukitaka kumuita kuanzia leo usimwite Abood, ni sharti uanze na Mheshimiwa Dkt Abdulaziz Abood ukimaanisha kutambua heshima aliyotunukiwa kutokana na uongozi thabiti katika mambo mbalimbali ya kijamii.
Sherehe za kumtunuku Dkt Abood udaktari huo zimefanyika jijini Dar es Salaam ambapo watanzania wengine kadhaa wamepewa heshima hiyo.
Dkt Abood ni mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini kwa takribani vipindi vitatu na amekuwa na mafanikio mengi katika nyanja mbalimbali kwa wananchi wa jimbo lake.