Mbowe: Tutashika dola kirahisi 2015

Mbowe: Tutashika dola kirahisi 2015

ndiyomkuusana

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
668
Reaction score
426
Na George Ramadhan|21st February 2013


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema sera mpya ya majimbo itakiwezesha chama hicho kushika dola na kuongoza nchi kwa urahisi zaidi.

Akifungua kikao cha kazi za Chadema kilichofanyika jijini hapa jana, Mbowe alisema sera ya majimbo ni mkakati uliobuniwa na chama hicho kwa lengo la kusogeza madaraka kwa wananchi ili kushiriki kufanya maamuzi ya jinsi ya kuongoza nchi.

Alisema utamaduni, ambao umezoeleka hapa nchini na ambao unatumiwa na serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kuongoza nchi kutokea Dar es Salaam. Mbowe alisema hatua hiyo imeonyesha kushindwa kuboresha hali ya maisha ya Watanzania wengi.
"Kwa zaidi ya miaka 20 sasa Tanzania tumekuwa na utamaduni wa kutawala nchi kutokea Dar es Salaam. Chadema tumeliona hili na tumegundua kasoro zake. Ndiyo maana tumeamua kuja na sera ya majimbo ili kusogeza madaraka kwa wananchi," alisema.

Alisema kwa kutumia mfumo huo, CCM imeonyesha kushindwa kushughulikia matatizo ya msingi ya wananchi, ikiwamo mgawanyo sahihi wa rasilimali za taifa. "Pamoja na kusogeza madaraka kwa wananchi, sera ya majimbo inalenga kutaka kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali zao tofauti na sasa. Maeneo yenye raslimali nyingi kama madini, ndiyo yenye kiwango kikubwa cha umaskini," alisema.

Alisema pia kwa kufuata mfumo huo, ndiyo sababu serikali ya CCM imekuwa ikijipanga kuwadhibiti viongozi wa Chadema kila wanapojipanga kwenda kufanya shughuli za kisiasa maeneo mbalimbali nchini.

Alisema kwa kufuata sera ya majimbo, serikali ya CCM haiwezi tena kuwadhibiti viongozi wa Chadema isipokuwa watashtukia chama hicho kimeshika dola na kuongoza nchi.



CHANZO: NIPASHE
 
Mzee Mwanakijiji ,
Vetting is not that easy. Bora ukitumie hicho hicho ulichonacho na unakiamini badala ya kukaribisha mamluki wengine ndani ya chama, wakati huo huo safu ya uongozi ambao tayari wanaaminiwa ni ndogo. Hebu fikiria, Hata CCM pamoja na kusaidiwa na usalama wa Taifa katika vetting, bado huwa mara nyingine wanapata makapi ya viongozi.
 
Last edited by a moderator:
Kweli wanasiasa wanaongoza kuota ndoto za mchana..Tena wanasiasa wa Tz kama wamelogwa hawataki kuongea ukweli kabisa.Mmelaniwa wote mnaoota Chadema kushika nchi 2015
 
Siku chache zilizopita, asha dii alikuja na mjadala mzuri juu ya kwanini yeye binafsi anadhania CCM itashinda uchaguzi mkuu wa 2015; Mwendelezo wa kauli kama hizi kutoka kwa Mbowe (ukiachilia ile ya mwaka jana kwamba CCM ikishinda 2015 atajiuzulu siasa), inaonyesha kwamba aidha kwa kujua au kutojua, kuelekea 2015, kutakuwa na more rhetoric (from chadema leaders) kuaminisha wananchi kwamba CCM itaanguka, kuliko effective practice/action ya kushirikiana na wananchi mapema kufanikisha hilo, hasa kwa Chadema kuachana na strategy ya kuvua wanachama milioni tano wa CCM and recruit them kuongezea idadi yao (chadema) ya wanachama takribani milioni mbili - tatu, na badala yake kujikita na swing voters bila ya kuhangaika kuwageuza kwanza kuwa wapiga kura wenye political affilitions na chadema; Kwa mujibu wa takwimu za wapiga kura 2010 ambao ilikuwa ni watanzania millioni kumi na nane, ukitoa wanachama wa CCM milioni tano, na wa chadema na vyama vingine vya siasa ambao sidhani kama wanazidi milioni tatu in total, it means column ya swing voters ni zaidi ya idadi ya wanachama wa vyama vyote vya siasa Tanzania, na hawa ndio watakuwa key to victory ya chama chochote baina ya hivi viwili iwapo turn out itakuwa ni kubwa 2015;

Unless chadema imefanya utafiti na kubaini kwamba ili kupigiwa kura na watanzania, ni lazima kwanza watanzania hao wawe wanachama wa Chadema; vinginevyo mimi kama mwanachama wa CCM pamoja na wengine wengi, tulipigia kura mgombea wa Chadema jimbo la Kawe - Halima Mdee kwani tuliona anatosha zaidi ya wagombea wa CCM na NCCR, huku kura yetu ya urais ikienda CCM kwa Kikwete kwani tulikuwa na imani nae kwamba atatekeleza mambo mengi kwa kasi zaidi baada ya serikali kuanguka 2008; mwenendo wetu wa kupiga kura kwa chadema 2010 (ubunge) means Chadema ina kura nyingi zaidi katika column ya swing voters (let alone ccm members) hata kama hawatakuwa wanachama wa Chadema by 2015; all Chadema needs is to engage them kisaikologia na kuwahamisha wajitokeze 2015, hasa kwa kuwa na rekodi zao ili wawe in constant communication kuliko kuhangaika kukusanya kadi za CCM; isitoshe, enzi za mass - based political parties zimeshapitwa na wakati, it no longer works for CCM, so Chadema should stop copying something which is already obsolete;

Vinginevyo, kama ya 2010 yatajirudia ambapo zaidi ya nusu ya wapiga kura hawakujitokeza kupiga kura, Chadema wasisahau kwamba a low voter turn out 2015 itakuwa ni ushindi wa CCM kwenda ikulu;
 
DAHHH MBOWE Anachekesha kweli kha ninechekabsaaaaaaanaaaa kama mtoto ea chekechea akuambie kesho najiunga na chuo kikuu nimefaulu
 
Sera ya majimbo inaiumiza sana kichwa ccm wamekimbilia propaganda za ukanda lakini hazikufua dafu sasa wamebakia na Yale makapi (shoza na Mwampamba) wakiulizia baba yake slaa wakati wao wenyewe Hawajui baba zao
 
Mzee Mwanakijiji ,
Vetting is not that easy. Bora ukitumie hicho hicho ulichonacho na unakiamini badala ya kukaribisha mamluki wengine ndani ya chama, wakati huo huo safu ya uongozi ambao tayari wanaaminiwa ni ndogo. Hebu fikiria, Hata CCM pamoja na kusaidiwa na usalama wa Taifa katika vetting, bado huwa mara nyingine wanapata makapi ya viongozi.

It is unnecessary consolidation of power in the hands of few... ni yale yale ya CCM.
 
Mzee Mwanakijiji ,
Vetting is not that easy. Bora ukitumie hicho hicho ulichonacho na unakiamini badala ya kukaribisha mamluki wengine ndani ya chama, wakati huo huo safu ya uongozi ambao tayari wanaaminiwa ni ndogo. Hebu fikiria, Hata CCM pamoja na kusaidiwa na usalama wa Taifa katika vetting, bado huwa mara nyingine wanapata makapi ya viongozi.
Vyeo vinavyotolewa kwa kujuana kuna vetting gani?Yale yale ya rubbe stamp tu.
 
It is unnecessary consolidation of power in the hands of few... ni yale yale ya CCM.
Absolutely. Kama binadamu tulivyo, "It is the unknown we fear when we look upon betrayal and party conflict.

Kwenye thread ya Mh. Mnyika aligusia hii kitu pale aliposema aliuomba mpaka uongozi kumpunguzia majukumu ya chama ili ajishughulishe na mambo mengine lakini uongozi ulikataa na kumuomba aendelee.

By consolidating the power kwa wachache, inaondoa hata maana/dhana nzima ya party decentralisation kwa sababu viongozi wa majimbo wanakuwa ni walewale wenye majukumu mengine ya chama kitaifa.
 
Vyeo vinavyotolewa kwa kujuana kuna vetting gani?Yale yale ya rubbe stamp tu.

Mkuu,
Kwenye siasa swala kujuana haliwezi kuepukika. Kitu cha maana kwanza ni uwezo wa kiutendaji utakaochagizwa na mahusiano yaliyopo. Tatizo litakuja tu kama kujuana kunatangulizwa kabla ya uwezo wa kiutendaji kama baadhi ya viongozi wa CCM walivyofanya katika chaguzi za kuteuwa wagombea udiwani na ubunge mwaka 2010 na kupelekea kushindwa katika chaguzi.
 
Kwanini watu ambao tayari wana nyadhifa ndani ya chama wanapewa nafasi nyingine za kuongoza kwenye kanda?

Unauliza?

Habari zenu wanajf:
Walikwepa sana kujitokeza kuzungumzia sakata la Kukiuzia chama magari chakavu(Fuso).Leo naomba Mbowe na Dr.slaa wajibu kwanini wameidhinisha kununua magari ya chama kwa bei kubwa kupitia kampuni ya MTEI LIMITED?
Mbowe na Slaa wamepitisha si kwalazima bali jeuri yao ya ubabe kuidhinisha tenda kampuni ya Mtei kwenda china kutengeneza pikipiki zenye lebo ya CHADEMA kupitia kampuni ya MTEI LIMITED yenye ofisi zake Mkwepu road(city centre)?.
Watanzania Dr.slaa na Mwenyekiti wa chama cha chadema wamefanya lebo ya pikipiki kwa gharama za TSh:Million 1 kila lebo nje ya kununua pikipiki husika,Je huu si ufisadi?.Kampuni iliyopewa tenda ni co-neccted na mwasisi wa chama.


Kampuni hiyohiyo imepewa tenda za kununua magari ya chama(Toyota-Pickup) kwa gharama za juu,
Kampuni imeimport magari na kusimamia usajili wake.Je kunanini kimefichika nyuma ya pazia?.
Mbowe na Dr.slaa kuna mikoa na wilaya ngapi chama hakipo?Kuna wilaya ngapi ruzuku haifiki?
Leo mnagharamia Lebo ya pikipiki kwa tsh:Million moja kila piikipiki moja?.Ni lini tutakuwa na dhamira ya kweli ya kuimarisha chama taifa zima?.


Wana jf hii ni ruzuku ya chama inaliwa kwa mtindo wa kuweka lebo pikipiki na kupeana tenda feki.
Chama chenye nia ya kuishi miaka mingi zaidi mbele na kuchukua dola kingeendelea kuishi kwenye nyumba ya kupanga tena makao makuu ya chama.?Ruzuku ya chadema(wabunge+madiwani) ni zaidi ya Million 350 kwa mwezi.Je kwanini chama hakina kiwanja wala wazo la kujenga makao makuu yake?.


Tunaomba tusiwe wakurupukaji,Tuhoji mwenendo wa vyama vyetu.Tusipo wahoji wataishia kutuandamanisha bila wayfoward.


Mwisho:Form 4 mliofeli ni matunda ya uvivu wa wazazi,kupuuzia madai ya walimu na matumizi ya viambata-utandawazi.
Nikirejea nchini mwezi ujao,Nitafikisha hili mbele ya wajumbe wa chadema(kamati kuu)
Contact:hazinam8@hotmail.com
phone:+23(654 88 94)
facebook:Hamza Maulid
twitter Hamzamau
 
Mkuu,
Kwenye siasa swala kujuana haliwezi kuepukika. Kitu cha maana kwanza ni uwezo wa kiutendaji utakaochagizwa na mahusiano yaliyopo. Tatizo litakuja tu kama kujuana kunatangulizwa kabla ya uwezo wa kiutendaji kama baadhi ya viongozi wa CCM walivyofanya katika chaguzi za kuteuwa wagombea udiwani na ubunge mwaka 2010 na kupelekea kushindwa katika chaguzi.
Kwahiyo wakati wa vetting kujuana inakuwa ni kigezo cha ngapi?Kipi kinaanza kati ya qualifications vs kujuana?
 
It is unnecessary consolidation of power in the hands of few... ni yale yale ya CCM.

Katika mazingira magumu ya kisiasa kama haya Chadema inayopitia ni bora na ni ulinzi mzuri ukitumia aina hii ya uongozi. Nafikiri watakuwa wakijibadilisha kila mwaka kwa kuongeza network zao. Sababu ndio wanaanza ni vyema wakawekana wenyewe na hao waliowekwa wakijikita vizuri kwenye majimbo yao watawapata waaminifu zaidi na kuongeza network.

Sidhani kama wataendelea na kagroup haka kadogo mpaka 2015, maana lazima watanuke ila si kwakuruhusu mamluki kwa kasi na mwanzoni tu. Sikatai mamluki hawatakosekana lakini kwa namna hii ni rahisi kuwashughulikia na kusimama upya.
 
Very interesting topic. Let me add my two cents into the discussion.

Kama mkuu Mchambuzi alivyo sema hapo juu kuna a lot of rhetoric coming out of Chadema na hata ukiangalia washabiki wengi wa Chadema humu ndani (kama kweli ni washabiki wa Chadema maishani au mitandaoni tu) utakuta kauli nyingi ziko based on emotions (hisia). Mwaka 2010 kuna wanaJF wengi walio kuwa wakii support Chadema (at least humu ndani, sijui mchango wao kiuhalisia) ambao walikua wana apa humu kwamba lazima Chadema itashinda 2010. Sisi ambao hatukua emotional about it tukasema its a premature declaration tuka tukanwa na kuitwa "mamluki", "mafisadi", nk. Matokeo yake Chadema ikashindwa 2010 na kwa sababu walisha jiaminisha kwamba ushindi ulikua must badala ya kujichunguza baada ya uchaguzi what went wrong kimbilio ikawa kwamba kulikua na uchakachuaje nk. Niwakumbushe tu watu kuhusu uchaguzi wa uraisi wa mwaka wa jana Marekani. Kambi ya mpinzani wa Obama, Mitt Romney na chama chake walisha jiaminisha ushindi na kujilisha data zisizo za ukweli kiasi kwamba matokeo ya uchaguzi yalipo anza kutiririka walishikwa na butwa.

Kitu kimoja nilicho gundua kuhusu siasa za Tanzania, na hii ni kwa vyama vyote, ni kwamba siasa zetu ni za kienyeji. Kwa wenzetu kama Marekani kuna kuwa na wanasiasa ambao kazi yao ni kutoa rhetoric na topic points lakini nyuma yao kuna wataalamu haswa wawe wa kukusanya data (research), wa communications (speech) nk. Kwa hiyo unakuta mgombea ndiyo mwanasiasa lakini behind him kuna team of professionals. Sisi kwenye chaguzi zetu kila mtu ni mwanasiasa kwa hiyo unakuta they has been no research done what so ever. Sijui kwa upande wa Chadema ila mimi ningekua na cheo Chadema baada ya 2010 ningetaka status report ya what went wrong. Ningetaka uchunguzi ufanyike na wataalamu siyo wanasiasa waangalie je ujumbe wetu ulipokelewaje na different groups of people (wa mjini/vijijini, wanaume/wanawake, wazee/vijana nk.). Pia ningeagiza kwamba kila baada ya muda fulani ifanyike polls kuangalia uhalisia wa kukubalika kwetu. Kumbuka kujaza watu kwenye mikutano haimaanishi kukubalika kwenye sanduku la kupigia kura. Sidhani kama kume wahi tokea mashabiki wa chama passionate kama wa CUF lakini leo chama kikoapi.

Kwa hiyo ushauri wangu kwa vyama vyote, especially CCM na Chadema kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 ningeomba wafanye professional research na kujipima uhalisia wa kukubalika kwao. Watu wanasahau Tanzania ni nchi ya watu milioni 45 na wengi wanaishi mjini lakini watu wakiona kwenye tv mikutano ya kivyama ya mjini imejaa watu wao wana chukulia kama ishara ya chama kukubalika kiasi hicho nchini kote na hii ina tokana na too much emotions and lack of professionalism. Mfano ni huu wa Mbowe kusema ujumbe wao wa kimajimbo unakubalika na ndiyo utawafikisha ikulu 2015. Hajaonyesha any study or research kuprove so which means kauli ni either rhetoric as usual au its based on emotions.
 
Katika mazingira magumu ya kisiasa kama haya Chadema inayopitia ni bora na ni ulinzi mzuri ukitumia aina hii ya uongozi. Nafikiri watakuwa wakijibadilisha kila mwaka kwa kuongeza network zao. Sababu ndio wanaanza ni vyema wakawekana wenyewe na hao waliowekwa wakijikita vizuri kwenye majimbo yao watawapata waaminifu zaidi na kuongeza network.

Sidhani kama wataendelea na kagroup haka kadogo mpaka 2015, maana lazima watanuke ila si kwakuruhusu mamluki kwa kasi na mwanzoni tu. Sikatai mamluki hawatakosekana lakini kwa namna hii ni rahisi kuwashughulikia na kusimama upya.

Waswahili husema "mazoea hujenga tabia". Kuna kitu kinaitwa "setting precedence". Kwamba ukianza hivyo kuna uwezekano mkubwa huku mbeleni ukaendelea hivyo hivyo maana una put in place the status quo na kama tunavyo jua kubadilisha status quo ni ngumu sana (after all movement nzima ya Chadema ni changing the status quo kwa hio wana lijua hilo. Ukasha weka utaratibu fulani ukazoeleka ina maana hao watakao fuata watafanya hicho hicho kwa kuwa cite nyie. Kwa hiyo tusiangalie short term tu bali long term after all hii tabia ya viongozi wetu kuto kuona mbali ndiyo ina sababisha hali ya udini sasa nchini.
 
Mkuu,
Kwenye siasa swala kujuana haliwezi kuepukika. Kitu cha maana kwanza ni uwezo wa kiutendaji utakaochagizwa na mahusiano yaliyopo. Tatizo litakuja tu kama kujuana kunatangulizwa kabla ya uwezo wa kiutendaji kama baadhi ya viongozi wa CCM walivyofanya katika chaguzi za kuteuwa wagombea udiwani na ubunge mwaka 2010 na kupelekea kushindwa katika chaguzi.

Kama ni hivyo basi Chadema ikubali it cannot change the status quo. Maana movement yao nzima ni ya "anti establishment". Sasa kama on one hand utafanya yale yale unayo dai mwenzio kafanya na yanaiponza nchi on the other hand na wewe unayafanya meaning wewe ukija kuwa na nafasi ya mwenzio tutegemee yale yale.
 
Kwanini watu ambao tayari wana nyadhifa ndani ya chama wanapewa nafasi nyingine za kuongoza kwenye kanda?
je ni wangapi kati ya hao unaowataja wana nyazifa ndani ya chama? Embu chambua uongozi wa kanda moja unayoiona wewe.

Loyality na uwezo wa kiutendaji katika siasa za tz ni kitu muhimu sana. Ni kitu kigumu kupata watu ambao wako able na loyal kwenye vyama vya upinzani.
 
mwanakijiji ameshakuwa mmarekani,anarusha smart bombs tokea cleveland,ohio,anaogopa vita ya ardhini!!
 
Back
Top Bottom