Mkuu katika siasa, practically, pale mtu anapokuwa mwanachama basi huyo anahesabika kama ameingia kwenye system ya chama kwa sababu kuwa mwanachama maana yake unaijua na kuikubali falsafa, itikadi, sera na malengo ya chama, na cha muhimu kabisa ni KUKIPIGANIA NA KUKILINDA CHAMA (LOYALTY), Kwa siasa zetu, hii kitu kwa sasa imekuwa ni zero, kwa maana kuwa, uanachama umekuwa ni nguzo mojawapo katika public spinning. Siyo kitu cha kushangaza kila siku watu wanabadilisha uanachama kama njugu.
Kwa jinsi siasa zetu zilivyo, kujuana imekuwa ni mojawapo ya merits ya kuwa kiongozi wa kisiasa kwa misingi ya sababu nilizoziainisha hapo juu. Kwa sababu kama hizo, hata viongozi wa CDM inawawia vigumu kujipambanua nje ya misingi hiyo ukichukulia kuwa, chama kwa sasa kina wanachama wa aina zote ( mamluki, loyal and neither mamluki nor loyal)