Siku chache zilizopita, asha dii alikuja na mjadala mzuri juu ya kwanini yeye binafsi anadhania CCM itashinda uchaguzi mkuu wa 2015; Mwendelezo wa kauli kama hizi kutoka kwa Mbowe (ukiachilia ile ya mwaka jana kwamba CCM ikishinda 2015 atajiuzulu siasa), inaonyesha kwamba aidha kwa kujua au kutojua, kuelekea 2015, kutakuwa na more rhetoric (from chadema leaders) kuaminisha wananchi kwamba CCM itaanguka, kuliko effective practice/action ya kushirikiana na wananchi mapema kufanikisha hilo, hasa kwa Chadema kuachana na strategy ya kuvua wanachama milioni tano wa CCM and recruit them kuongezea idadi yao (chadema) ya wanachama takribani milioni mbili - tatu, na badala yake kujikita na swing voters bila ya kuhangaika kuwageuza kwanza kuwa wapiga kura wenye political affilitions na chadema; Kwa mujibu wa takwimu za wapiga kura 2010 ambao ilikuwa ni watanzania millioni kumi na nane, ukitoa wanachama wa CCM milioni tano, na wa chadema na vyama vingine vya siasa ambao sidhani kama wanazidi milioni tatu in total, it means column ya swing voters ni zaidi ya idadi ya wanachama wa vyama vyote vya siasa Tanzania, na hawa ndio watakuwa key to victory ya chama chochote baina ya hivi viwili iwapo turn out itakuwa ni kubwa 2015;
Unless chadema imefanya utafiti na kubaini kwamba ili kupigiwa kura na watanzania, ni lazima kwanza watanzania hao wawe wanachama wa Chadema; vinginevyo mimi kama mwanachama wa CCM pamoja na wengine wengi, tulipigia kura mgombea wa Chadema jimbo la Kawe - Halima Mdee kwani tuliona anatosha zaidi ya wagombea wa CCM na NCCR, huku kura yetu ya urais ikienda CCM kwa Kikwete kwani tulikuwa na imani nae kwamba atatekeleza mambo mengi kwa kasi zaidi baada ya serikali kuanguka 2008; mwenendo wetu wa kupiga kura kwa chadema 2010 (ubunge) means Chadema ina kura nyingi zaidi katika column ya swing voters (let alone ccm members) hata kama hawatakuwa wanachama wa Chadema by 2015; all Chadema needs is to engage them kisaikologia na kuwahamisha wajitokeze 2015, hasa kwa kuwa na rekodi zao ili wawe in constant communication kuliko kuhangaika kukusanya kadi za CCM; isitoshe, enzi za mass - based political parties zimeshapitwa na wakati, it no longer works for CCM, so Chadema should stop copying something which is already obsolete;
Vinginevyo, kama ya 2010 yatajirudia ambapo zaidi ya nusu ya wapiga kura hawakujitokeza kupiga kura, Chadema wasisahau kwamba a low voter turn out 2015 itakuwa ni ushindi wa CCM kwenda ikulu;