EasyFit
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 1,269
- 1,082
Mwenyeki wa Chadema Taifa Mh. Freeman Mbowe akijibu tuhuma za Katibu mkuu wa CCM Mukama kuwa chama chake kimeingiza makomandoo 33 kutoka nje, ameshangaa na kueleza kuwa kauli za katibu mkuu huyo wa CCM ni matokeo ya kushiriki siasa za uzeeni.
"Sasa hili Mukama hawezi akajua kwa sababu yeye anafanya siasa za uzeeni. ..Yeye (Mukama) hajawahi kugombea udiwani, uenyekiti wa mtaa, ubunge au nafasi yoyote ndani ya chama chake zaidi ya huu ukatibu mkuu ambao alipewa tu.. atayajuaje hayo?" Alihoji Mbowe
Alisema katika kipindi cha uchaguzi ni jambo la kawaida kwa chama chenye wapenzi wengi kama Chadema na CCM yenyewe kupokea mashabiki, makada na wapenzi kutoka nje ya eneo la uchaguzi. Mbowe alisema Chadema kina wapenzi na mashabiki kadhaa kutoka nje ya wilaya ya Igunga, lakini akaeleza kuwa siyo makomandoo kama anavyodai Mukama vinginevyo atoe ushahidi na kuwataja kwa majina.
::Mwananchi::