Mbowe: Tatizo la Mukama kaanza siasa uzeeni

Sina ajira ila ukinipa ukatibu mkuu wa ccm nadhan umeniongezea matatizo na presha
 
Assuming Chadema imeleta makomandoo, kazi yao itakuwa ni nini? Labda kama kuna tafsiri tofauti ya komandoo. CCM walikuwa wanachimba kaburi bila kujua watamzika nani.

Hivi zile harakati za Nape na wenzake za kuwataka Chenge na Lowassa waachie ngazi zimeishia wapi? Uchaguzi wa Igunga utawafanya wafikiri upya, maana hicho ni chama maslahi
 
Wapinzani wanalalamika, chama tawala nao wanalalamika. Ccm wanafanya siasa za maji taka.
 
Si kila mzee akizeeka anakuwa na busara ,watu wengine wakizeeka wanakua vichaa ndo Kama Mukama
Slaa ndiye anazeeka vibaya.
Naona tayari amneshaanza kupotea kwenye ulimwengu wa siasa
 
Slaa ndiye anazeeka vibaya.
Naona tayari amneshaanza kupotea kwenye ulimwengu wa siasa

Naona leo mapema umeshaanza kufikiri kwa kutumia masaburi yako!!! huo mshahara nepi anaokupa kwa sababu ya unafiki hautakusaidia ng'o .
kilio cha watz kii juu yako we kihiyo.
 
neno linasema "...utufundishe kuzihesabu siku zetu........." hawa akina mukama kwani hawajui umri wao.
 
mukama hana hoja, kwa nini anasema ametumwa na rais kumwombea kura mgombea wao, kwani hawezi kumnadi yeye mwenyewe???. Kwa nini asisimame yeye mwenyewe kwa miguu yake badala yake anasema eti ametumwa na rais. kwani jk yeye ndo anakubalika sasa?. Naona magamba kama wamechanganyikiwa vile
 
Nashangaa safari hii taarifa za intelijensia hazijapata hiyo! Au satelite za intelijensia za polisi zimekuwa butu kuliko za CCM? Maana kada wao IGP angeita wanahabari na kuipigia debe CCM kiaina.

Polisi wako busy mipakani wanalinda sukari isitoke nje ya nchi,kabla PM hajawawajibisha.....Tete te teh...
 
isue hapo ni ushahidi na si ushabiki yasije yakawa ya madawa yakulevya ya viongozi wa dini na jakaya then baada ya ushahidi wakaloa
baada ya ushahidi upi mkuu...hivi kuna ushahid wa madawa ya kulevya kwa viongoz wa dini umetolewa?au ule wa kuandika kny kijarida chenu cha uhuru bila kutaja majina....i can see hata wenyewe hamuamini mnachokitetea..
 
mukama hana hoja, kwa nini anasema ametumwa na rais kumwombea kura mgombea wao, kwani hawezi kumnadi yeye mwenyewe???. Kwa nini asisimame yeye mwenyewe kwa miguu yake badala yake anasema eti ametumwa na rais. kwani jk yeye ndo anakubalika sasa?. Naona magamba kama wamechanganyikiwa vile
Ulitaka asitoe ujumbe wa raisi?
Try to think big broda
 
Si kila mzee akizeeka anakuwa na busara ,watu wengine wakizeeka wanakua vichaa ndo Kama Mukama

hivi mzee anaechukua wake wa ndoa wa watu na kauli zilizotolewa ni yupi anaonekana kichaa na hana hekima na busara!
 
Mkama alijipendekeza kwa kikwete na kumfanyia utafiti feki kisha wakibuka na kujivua gamba, tangu ameteuliwa hakuna hata pendekezo moja ambalo alipendekeza kwenye utafiti wake ambao umefanikiwa, zaidi sana matatizo ndo yameongezeka, Sasa anaona bora atumie mbinu za mtangulizi wake makamba. na hapo ndo anaharibu zaidi. Yetu macho. Nawaomba wapambanaji waliopo Igunga watumie matokeo ya Zambia kuwaeleza wananchi wazidi kuichukia zaidi ccm.
 
Big up sana Mbowe. Achana na Mukama. Mwambie aangalie breaking news: Zambia chama tawala chali Nasi tutawaonyesha kuwa hata TZ yawezekana tukianzia na Igunga.
 
Tuhuma zilizotolewa na Mukama si za kubeza kwani ndanimwe zimehusisha si tu Chadema bali pia hata Nchi walizochukua mafunzo hao makomandoo na kuonyesha vyombo vyenu vya ulinzi na usalama havifanyi kazi kwa umakini.

Ni vizuri akahojiwa na vyombo husika kuthibitisha kauli yake ili kuondoa khofu kwa wakaazi wa Igunga na wapiga kura wote.
 
Mukama sasa ameonyesha kuchoka kama ccm iliyokumbatia siasa za kizamani za kudanganya watu. Wananchi sasa wameshajua chama hakina jipya zaidi ya kuimba amani ambayo ilitoweka na nyerere.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom