Mbowe: Tatizo la Mukama kaanza siasa uzeeni

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,080
Mwenyeki wa Chadema Taifa Mh. Freeman Mbowe akijibu tuhuma za Katibu mkuu wa CCM Mukama kuwa chama chake kimeingiza makomandoo 33 kutoka nje, ameshangaa na kueleza kuwa kauli za katibu mkuu huyo wa CCM ni matokeo ya “kushiriki siasa za uzeeni”.
"Sasa hili Mukama hawezi akajua kwa sababu yeye anafanya siasa za uzeeni. ..Yeye (Mukama) hajawahi kugombea udiwani, uenyekiti wa mtaa, ubunge au nafasi yoyote ndani ya chama chake zaidi ya huu ukatibu mkuu ambao alipewa tu.. atayajuaje hayo?" Alihoji Mbowe

Alisema katika kipindi cha uchaguzi ni jambo la kawaida kwa chama chenye wapenzi wengi kama Chadema na CCM yenyewe kupokea mashabiki, makada na wapenzi kutoka nje ya eneo la uchaguzi. Mbowe alisema Chadema kina wapenzi na mashabiki kadhaa kutoka nje ya wilaya ya Igunga, lakini akaeleza kuwa siyo makomandoo kama anavyodai Mukama vinginevyo atoe ushahidi na kuwataja kwa majina.

::Mwananchi::
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
58,644
116,816
Mwenyeki wa Chadema Taifa Mh. Freeman Mbowe akijibu tuhuma za Katibu mkuu wa CCM Mukama kuwa chama chake kimeingiza makomandoo 33 kutoka nje, ameshangaa na kueleza kuwa kauli za katibu mkuu huyo wa CCM ni matokeo ya "kushiriki siasa za uzeeni".

CCM watatafunwa na siasa zao za maji ya chooni, okey Mukama peleka ushahidi tuone nani atakayeumbuka. Kumbe baadhi ya watu wanavyozeeka wanazidi kuwa watupu kichwani.
 
Kabakabana

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
5,553
1,157
safi mbowe achana nao masaburi tu hawa wanatuchafulia jina halafu nyyiiiiiiiiiiiiieeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
Tena inabidi siyo atoe information polisi inabidi watoe taarifa hizo jeshini maana huo ni uvamizi kutoka nje.
huo ni uongo ikiwemo propaganda za kitoto za kupanga matukio ya uvunjaji wa sheria ili kuwapa mavi wapinzani wake.
 
Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,877
6,831
Ukitaka kuzeeka vibaya basi ingia anga za siasa wakati umestaafu utachanganyikia na kutembea na pills za kutelemsha mapigo ya moyo kila saa.
 
RMA

JF-Expert Member
Oct 10, 2010
409
87
Tena inabidi siyo atoe information polisi inabidi watoe taarifa hizo jeshini maana huo ni uvamizi kutoka nje.
huo ni uongo ikiwemo propaganda za kitoto za kupanga matukio ya uvunjaji wa sheria ili kuwapa mavi wapinzani wake.
Kama Mkama anakiamini hicho alichokisema, sasa aonyeshe mfano! Amshinikize waziri wa Mambo ya ndani ajiuzuru mara moja kwa kuruhusu makomandoo hao kuingia nchini kinyume cha sheria! Kisha na yeye ajiuzuru kwa kuwa chama chake kinaongoza serikali isiyowajibika. Chadema ungeni mkono hoja ya Mkama mara moja! ... kwamba ni kweli kuna makomandoo na kisha ashinikizwe kujiuzuru!
 
gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,226
3,087
safi mbowe achana nao masaburi tu hawa wanatuchafulia jina halafu nyyiiiiiiiiiiiiieeeeeeeeeeeeeeeeeeee

isue hapo ni ushahidi na si ushabiki yasije yakawa ya madawa yakulevya ya viongozi wa dini na jakaya then baada ya ushahidi wakaloa
 
niweze

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
1,008
114
Mbowe kasema ukweli na ukiangalia hii ccm imejaa uzeee, njaa, ugaidi, unyama, killings n.k.

Tutanawashughulikia sasa Igunga!
 
Ochutz

JF-Expert Member
May 21, 2011
465
105
Poor ccm,dalili zote za chama kuanguka zinaonekana wazi,yani ni kama wamezama baharini vile,maji ya shingo wanatapatapa tu,soon watachoka na kuzama!
 
MESTOD

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
4,795
1,987
Nashangaa safari hii taarifa za intelijensia hazijapata hiyo! Au satelite za intelijensia za polisi zimekuwa butu kuliko za CCM? Maana kada wao IGP angeita wanahabari na kuipigia debe CCM kiaina.
 
kilemi

JF-Expert Member
Mar 13, 2009
544
98
Nimesoma hilo gazeti, Mukama kasema CDM wako hovyohovyo kama Ghadafi! Hapo ameitukana CDM au Kikwete na waziri wake Membe?
 
  • Thanks
Reactions: SG8

Felixonfellix

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
1,672
180
MHHHHHHHHHHHHHHHH
Huyu mzee Mukama ana kazi kwelikweli
Mwenyeki wa Chadema Taifa Mh. Freeman Mbowe akijibu tuhuma za Katibu mkuu wa CCM Mukama kuwa chama chake kimeingiza makomandoo 33 kutoka nje, ameshangaa na kueleza kuwa kauli za katibu mkuu huyo wa CCM ni matokeo ya "kushiriki siasa za uzeeni".
"Sasa hili Mukama hawezi akajua kwa sababu yeye anafanya siasa za uzeeni. ..Yeye (Mukama) hajawahi kugombea udiwani, uenyekiti wa mtaa, ubunge au nafasi yoyote ndani ya chama chake zaidi ya huu ukatibu mkuu ambao alipewa tu.. atayajuaje hayo?" Alihoji Mbowe

Alisema katika kipindi cha uchaguzi ni jambo la kawaida kwa chama chenye wapenzi wengi kama Chadema na CCM yenyewe kupokea mashabiki, makada na wapenzi kutoka nje ya eneo la uchaguzi. Mbowe alisema Chadema kina wapenzi na mashabiki kadhaa kutoka nje ya wilaya ya Igunga, lakini akaeleza kuwa siyo makomandoo kama anavyodai Mukama vinginevyo atoe ushahidi na kuwataja kwa majina.

::Mwananchi::
 
matungusha

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
594
125
isue hapo ni ushahidi na si ushabiki yasije yakawa ya madawa yakulevya ya viongozi wa dini na jakaya then baada ya ushahidi wakaloa
Acha kichaa mbona huyo jk hajawataja hoa viongozi wa dini ili tuwafahamu? na kama wapo mbona hawafikishwi mahakaman? does it mean wapo juu ya sheria? tunataka ushahid na sio maneno matupu ya rais asiyejiamin...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

9 Reactions
Reply
Top Bottom