Mbowe: Polisi tukutane Mahakamani ila siwapi Ushahidi

Mbowe: Polisi tukutane Mahakamani ila siwapi Ushahidi

Hivi katika hili nani anatakiwa kwenda Mahakamani, POLISI au MBOWE? Polisi ni taasisi inayofanyia uchunguzi sasa kama mwenye ushahidi asipokuwa na imani na Polisi yeye ndiye anapaswa kwenda mahakamani na siyo vinginevyo. Hakuna serikali yoyote diniani ambayo rais wake hushinikizwa na wanasiasa kuunda tume.

Usijali ,kuna makosa mengi ambayo ni ukatili dhidi ya binadamu yanayotakiwa kupelekwa mahakaman na wahusika ni viongozi waliopo madarakani akiwemo JK, ni suala la muda tu.
 
Muulize Chagonja alietumwa Arusha kuchunguza kwa kutumia kodi zetu yeye alichogundua mlipuaji ni nani?Kwani Mbowe aliondoka na ule uwanja palipolipuliwa pamoja na vielelezo vyote?vile vile palikuwa na polisi,waandishi wa habari na mashuhuda wengine.Je Chagonja na timu yake wamefanya homework waliyopewa??Be professional kidogo.

Huyo mingoi hana uwezo wa kuwa professional, anazidiwa akili na mbuzi
 
polisi waende mahakamani kufanya nini? Hivi mtuhumiwa na mtuhumu nani anakwenda mahakamani? Mbowe mwenyewe anasema polisi ni watuhumiwa yeye aende mahakani, polisi wanachokitaka ni ushahidi waufanyie kazi kama wao ndo watuhumiwa basi watasubiri wapelekwe mahakani.

polisi waende mahakamani kumshitaki mbowe kwa kukataa kutoa ushahidi!
 
IKIWA leo ni siku ya mwisho aliyopewa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Jeshi la Polisi nchini kuwasilisha ushahidi wa kuhusika kwa jeshi hilo na mlipuko wa bomu uliotokea mwezi uliopita mkoani Arusha, kiongozi huyo amegoma kuutoa.

Jeshi la Polisi kupitia Mkurugenzi wake wa Makosa ya Jinai Julai 17 lilimwandikia Mbowe barua yenye kumbukumbu namba AR/IR/6223/2013 ikimtaka kupeleka ushahidi wake leo kabla ya saa nane mchana, kiongozi huyo amewataka polisi kumpeleka mahakamani kwani hatawapa ushahidi huo.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Mbowe alisema kamwe hawezi kwenda kinyume cha msimamo wa chama chake walioamua kutoukabidhi ushahidi huo kwa polisi hata kama watawapa vitisho kama walivyozoea.

Alibainisha kuwa alipokea barua iliyomtaka aende polisi leo na ataitikia wito huo, lakini hatapeleka ushahidi wanaoutaka, kwakuwa wao ni watuhumiwa.

Alisema CHADEMA ilimwandikia Rais Jakaya Kikwete barua ikimwomba kuunda tume huru ya majaji kwa ajili ya tukio hilo, ambayo wataikabidhi ushahidi wao.

Aliongeza kuwa masuala muhimu yagusayo chama na masilahi ya taifa yanafanyika kulingana na maamuzi ya vikao, hivyo yeye hawezi kwenda kinyume cha kilichoamuliwa.

Kwa mujibu wa Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, suala la Arusha linahusisha viongozi, wanachama na wapenzi wa CHADEMA, hivyo lilifikishwa kwenye vikao na kufanyiwa uamuzi wa kutopeleka ushahidi polisi.

“Nina mambo mengi ya kukutana na polisi, nitaitikia wito wao lakini kuhusu kupeleka huo ushahidi ni msimamo wa chama kwamba hatupeleki… waende mahakamani, wachukue hatua za kisheria au waamue lolote.

“Tunasubiri kauli ya rais ya ama ataunda tume ama hataunda tume huru ya kimahakama yenye majaji. Lakini pia ninamsubiri mwanasheria wa chama ambaye anakuja kutoka Tabora, polisi nitaenda tu,” alisema Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Barua ya polisi

Jeshi la Polisi kupitia Mkurugenzi wake wa Makosa ya Jinai Julai 17 lilimwandikia Mbowe barua yenye kumbukumbu namba AR/IR/6223/2013 ikimtaka kupeleka ushahidi wake Julai 23 (leo) kabla ya saa nane mchana.

“Kutokana na mahojiano uliyofanya na Polisi Mkoa wa Arusha mnamo Juni 20, 2013 kuhusu mauaji yaliyotokana na ulipuaji wa bomu huko Soweto, Arusha ulidai kuwa unao ushahidi unaobainisha wahusika wa tukio hilo.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 10 (2) na (2A) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai nchini, sura 20 kama ilivyorekebishwa mwaka 202, unaamriwa kufika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai tarehe 23 Julai, 2013 saa nane mchana bila kukosa na ulete ushahidi huo.

“…Unatahadharishwa kuwa kushindwa au kukataa kufika na kuleta ushahidi huo ni kosa la jinai chini ya sheria iliyotajwa,” inasomeka sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Hussein Laisseri, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai.

Juni 15, mwaka huu wakiwa kwenye mkutano wa wazi uliokuwa ukihutubiwa na Mbowe katika viwanja vya Soweto mjini Arusha wakati wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani wanne, bomu la kutupwa kwa mkono lililipuka na kusababisha vifo vya watu wanne na kuwajeruhi wengine 70.

Awali jeshi hilo lilituma viongozi wake wa juu mkoani Arusha kwa ajili ya uchunguzi, ambapo waliwahoji watu kadhaa akiwamo Mbowe, kwamba alisema alimwona aliyelipua bomu hilo kuwa ni askari polisi na kuweka bayana kwamba hawezi kuutoa ushahidi huo kwa polisi kwa madai kuwa watauharibu.
hivi ule ushahidi wa Mwangozi ulifanyiwa kazi?
 
Heshima kwako mkuu wangu kwa maoni muruwa kabisa.. Sisi tulifundishwa sunday school kwamba unapotaja jina kubwa kama la MUNGU LAZIMA LIANZE KWA HERUFI KUBWA..HATA KAMA NI KATIKATI YA MSTARI!
Unaweza kuwa mjinga usijhitambue na unaweza kuwa -------- usijitambue lakini uwezo wako wa kufikiri unaweza kunaksi ujinga na upumbavu wako, kwa kutoitumia hekima na akili uliyopewa na mungu wako. Tanzania ni nchi ya propaganda, watu wanaua au kuuliwa lakini sheria haichukui mkondo wake, Hivi km wewe ungekoswa koswa na bomu ungefanya nini? mwenye kazi ya kukamata na kushtaki ni polisi au mbowe? kama mbowe hataki kupeleka ushahidi polisi si wamshtaki mahakamani lili mahakama imlazimishe kuupeleka ushahidi mahakamani? Tatizo mehemko ya magamba inaongoza fikra zako.
 
Tunakuunga mkono mwenyekiti... Hakuna kupeleka ushahidi kwa wastakiwa! HAIWEZEKANI HATA KIDOGO..
 
Habari za awali zinasema chadema walinilipu wenyewe. Lukuvi. Bomu la arusha lililipuliwa na wana chadema. Mwigulu. Pois aashikeni hao kisha mmalizie na ushahidi wa mbowe mtamjua nani aliipua
 
Hivi katika hili nani anatakiwa kwenda Mahakamani, POLISI au MBOWE? Polisi ni taasisi inayofanyia uchunguzi sasa kama mwenye ushahidi asipokuwa na imani na Polisi yeye ndiye anapaswa kwenda mahakamani na siyo vinginevyo. Hakuna serikali yoyote diniani ambayo rais wake hushinikizwa na wanasiasa kuunda tume.

Kaka sula sio kushinikizwa bali utaratibu huo wa tume kuundwa tayari umetamkwa bayana ndani ya katiba yetu

Tafakari kidogo..ulishamwona fisi anavyotahayari akinaswa mazima mazima kwenye mtego???
 
katika taasisi ambazo mpaka sasa zimeumbuka hadi kwa watoto wadogo ni Msajili wa Vyama vya Siasa chini ya Tendwa, Polisi nao wasipokuwa makini katika hili huenda wakajikuta wanaangukia katika shimu hilohilo hivyo kuzidi kupoteza imani kwa wananchi wa kawaida ambayo mpaka hapo ina utata. Kuna haja ya kutumia 'logic' wakati wa kutekeleza 'maagizo kutoka juu'.
 
Ndiyo,Kafaulu maisha ndio maana biashara zake zinaendelea vizuri sana na pia ni Mwenyekiti wa Chama kikubwa cha Upinzani Nchini cha CHADEMA.Je wewe mwenzetu umefaulu/umefanikiwa nini katika maisha yako?

Biashara zake ni biashara za kuiharibu jamii, biashara za kishetani. Toka lini ukasikia biashara ya kishetani ni mafanikio? unanchekesha.
 
Ndiyo alifaulu..wewe je ulifaulu?

Nilifaulu vizuri sana, nikakatwa jina langu nafasi yangu akapewa Mkatoliki wakati wa Nyerere. Nikapelekwa shule za "private" nje ya Tanzania, sijawahi kufeli hata mara moja maishani mwangu.
 
kuna kitu sielewi, hivi kwa mfano mbowe angeamua kuwapa huo ushahidi ambao actually watuhumiwa ni wao, wanataka wakiishauona wafanyeje? wauharibu au wakanushe kuwa umetengenezwa au haswa wana lengo lipi kutaka kuuona ushahidi? maana kama ni kuuharibu au kuubishia si hautakuwa copy moja? wanaweza kuchakachua kumbe bbc, wanao au aljaazera wanao au voa wanao. binafsi sijajua kwa kuuona itawasaidia nini polisi, siamini kama wanaweza kubadilisha maana zaidi ya kubisha na kupindisha kauli
 
Tukutane mahakamani tu,

Polisi wapuuzi sana,

Bomu walipue wao, donge nono watangaze wao, tume waunde wao, ushahidi wapelekewe wao, mtuhumiwa namba moja ni wao, nk!

Sasa umefika wakati wa sheria ya Musa, jino kwa jino!
 
Hivi sheria inasemaje polisi au msamaria mwema ni yupi awe mpelelezi wa makosa kama mimi nimeona tukio basi haina haja yakusepa polisi maana tena nitaamrishwa kupeleka ushahidi hiki nalo ni majanga hivi polisi pesa wanayolipwa huwa wanafanya kazi gani Mbowe anacho kitaka ni kesi waipeleke mahakamani na siyo polisi polisi ni sehemu tu yakutoa maelezo tayari ameshatoa maelezo mara 3 hivi au polisi imekuja kuwa ndiyo mahakama? Ndiyo tatizo polisi kuingilia mambo ya siasa ingekuwa hao polisi ni mtu mnyonge ungekuta kashaburuzwa mahakamani zamani.
 
Mbona hawautaki ushahidi wa mwigulu hapa Tanzania hakuna haki kabisa vyombo vya dola vmenunuliwa
 
Nilifaulu vizuri sana, nikakatwa jina langu nafasi yangu akapewa Mkatoliki wakati wa Nyerere. Nikapelekwa shule za "private" nje ya Tanzania, sijawahi kufeli hata mara moja maishani mwangu.
unanisononesha sana...
 
Mbowe heshimu mamlaka,Mbowe heshimu roho za watu wa Arusha waliopoteza maisha kutokana na mlipuko wa bomu ili waliyofanya wahukumiwe hapa duniani na akhera.Msuguano na polisi hautokupa umaarufu zaidi ya kuonekana mpuuzi mbele ya wenye kujitambua.

Ataonekana Mpuuzi Mbele yenu Misukule ya Lumumba inayofikri kwa Kutumia Tumbo
 
Back
Top Bottom