Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,162
- 17,632
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema Serikali haitoi ruhusa ya utekaji na kwamba vitendo vya utekaji, mauaji na kupotea kwa watu ni makosa ya jinai yanayokiuka sheria na yatachunguzwa kwa kina ili ukweli ubainike.
Amesema endapo mtu anahusishwa na uhalifu, Serikali humkamata kwa mujibu wa sheria na kumfikisha katika vyombo vya sheria, ikiwemo kushikiliwa na polisi na baadaye kufikishwa mahakamani ikiwa ushahidi unathibitisha tuhuma zinazomkabili.
Akizungumzia tuhuma zinazowahusisha baadhi ya maafisa wa polisi, Katambi amesema tuhuma pekee hazitoshi kuchukua hatua za kinidhamu au kisheria bila ushahidi, akiwataka wenye vielelezo kuviwasilisha ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria.