Mbowe: Polisi tukutane Mahakamani ila siwapi Ushahidi

Mbowe: Polisi tukutane Mahakamani ila siwapi Ushahidi

Red brigade iboreshwe upesi inakazi kubwa ya kufanya yaani mtu anakulia wanachama wako kisha anakupa siku upeleke ushahidi na vitisho juu..ujinga huu haukubaliki...
 
Policcm na ccm wameshindwa kazi.mimi nashauri huyu janga la taifa avunje jeshi lake chafu la policcm aliunde upya.maana linatumika kwa maslahi ya ccm.hakuna mtu mwenye imani na jeshi la policcm.muwacheni mh.mbowe ana mambo mengi uakufanya.nyambafff.
 
Iko siku tutawanasa tu, dawa iko jikoni

Pale tutakapopata tume huru.... Vinginevyo maigizo yanaendelea..... Aliyemuua Mwangosi yuko wapi? Kesi imeishia wapi? Waliokamatwa baada ya kumuua kikatili Mbwambo walitorokaje mikononi mwa polisi??? Chilisosi wewe ulisema ni x-polisi hebu saidia hapa!!! Unaona ni sawa??? Utaifa hatunao tena tumebakizi ushabiki wa vyama tu.....
 
Last edited by a moderator:
Kwanini hao askari hawajapelekwa dafur.au Congo wakafuliwe uko kama nguo.Ushahidi anayo mwingulu nchemba.narudia tena ushahidi anayo mwingulu nchemba tena atautoa mpaka mbunguni
 
Kwanini hao askari hawajapelekwa dafur.au Congo wakafuliwe uko kama nguo.Ushahidi anayo mwingulu nchemba.narudia tena ushahidi anayo mwingulu nchemba tena atautoa mpaka mbinguni
 
Kwani safari hii kaandaa shilingi ngapi ya kuwahonga majaji make ya lwakatare aliandaa kiasi kikubwa.

Aisee unadhani kazoea kuhonga kama nyie maana nyie mnahonga mpaka vilivyomo kwenye chupi
 
Kauri hii siyo bure polisi wawe makini anaweza kufa mtu hawa watu kuuwa kwaokama kawa tu,polisi jiandaeni mwenzenu hamaanishi mahakama kweli ni lugha ya picha tu.
Mirembe style buku 7 ''''' weye
 
Mbona mwigulu hakulazimishwa kupeleka ushahidi wake?muendelezo wa wa double standard tu
 
Aisee unadhani kazoea kuhonga kama nyie maana nyie mnahonga mpaka vilivyomo kwenye chupi

Hahaha hahaha hahaha hahaha hahaha dah hapo umeliambiya ukweli gamba .magamba hayataki kuambiwa ukweli.
 
Kwani Mbowe ni polisi?

Ndiyo,Kafaulu maisha ndio maana biashara zake zinaendelea vizuri sana na pia ni Mwenyekiti wa Chama kikubwa cha Upinzani Nchini cha CHADEMA.Je wewe mwenzetu umefaulu/umefanikiwa nini katika maisha yako?
 
IKIWA leo ni siku ya mwisho aliyopewa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Jeshi la Polisi nchini kuwasilisha ushahidi wa kuhusika kwa jeshi hilo na mlipuko wa bomu uliotokea mwezi uliopita mkoani Arusha, kiongozi huyo amegoma kuutoa.

Jeshi la Polisi kupitia Mkurugenzi wake wa Makosa ya Jinai Julai 17 lilimwandikia Mbowe barua yenye kumbukumbu namba AR/IR/6223/2013 ikimtaka kupeleka ushahidi wake leo kabla ya saa nane mchana, kiongozi huyo amewataka polisi kumpeleka mahakamani kwani hatawapa ushahidi huo.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Mbowe alisema kamwe hawezi kwenda kinyume cha msimamo wa chama chake walioamua kutoukabidhi ushahidi huo kwa polisi hata kama watawapa vitisho kama walivyozoea.

Alibainisha kuwa alipokea barua iliyomtaka aende polisi leo na ataitikia wito huo, lakini hatapeleka ushahidi wanaoutaka, kwakuwa wao ni watuhumiwa.

Alisema CHADEMA ilimwandikia Rais Jakaya Kikwete barua ikimwomba kuunda tume huru ya majaji kwa ajili ya tukio hilo, ambayo wataikabidhi ushahidi wao.

Aliongeza kuwa masuala muhimu yagusayo chama na masilahi ya taifa yanafanyika kulingana na maamuzi ya vikao, hivyo yeye hawezi kwenda kinyume cha kilichoamuliwa.

Kwa mujibu wa Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, suala la Arusha linahusisha viongozi, wanachama na wapenzi wa CHADEMA, hivyo lilifikishwa kwenye vikao na kufanyiwa uamuzi wa kutopeleka ushahidi polisi.

“Nina mambo mengi ya kukutana na polisi, nitaitikia wito wao lakini kuhusu kupeleka huo ushahidi ni msimamo wa chama kwamba hatupeleki… waende mahakamani, wachukue hatua za kisheria au waamue lolote.

“Tunasubiri kauli ya rais ya ama ataunda tume ama hataunda tume huru ya kimahakama yenye majaji. Lakini pia ninamsubiri mwanasheria wa chama ambaye anakuja kutoka Tabora, polisi nitaenda tu,” alisema Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Barua ya polisi

Jeshi la Polisi kupitia Mkurugenzi wake wa Makosa ya Jinai Julai 17 lilimwandikia Mbowe barua yenye kumbukumbu namba AR/IR/6223/2013 ikimtaka kupeleka ushahidi wake Julai 23 (leo) kabla ya saa nane mchana.

“Kutokana na mahojiano uliyofanya na Polisi Mkoa wa Arusha mnamo Juni 20, 2013 kuhusu mauaji yaliyotokana na ulipuaji wa bomu huko Soweto, Arusha ulidai kuwa unao ushahidi unaobainisha wahusika wa tukio hilo.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 10 (2) na (2A) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai nchini, sura 20 kama ilivyorekebishwa mwaka 202, unaamriwa kufika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai tarehe 23 Julai, 2013 saa nane mchana bila kukosa na ulete ushahidi huo.

“…Unatahadharishwa kuwa kushindwa au kukataa kufika na kuleta ushahidi huo ni kosa la jinai chini ya sheria iliyotajwa,” inasomeka sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Hussein Laisseri, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai.

Juni 15, mwaka huu wakiwa kwenye mkutano wa wazi uliokuwa ukihutubiwa na Mbowe katika viwanja vya Soweto mjini Arusha wakati wa kuhitimisha kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani wanne, bomu la kutupwa kwa mkono lililipuka na kusababisha vifo vya watu wanne na kuwajeruhi wengine 70.

Awali jeshi hilo lilituma viongozi wake wa juu mkoani Arusha kwa ajili ya uchunguzi, ambapo waliwahoji watu kadhaa akiwamo Mbowe, kwamba alisema alimwona aliyelipua bomu hilo kuwa ni askari polisi na kuweka bayana kwamba hawezi kuutoa ushahidi huo kwa polisi kwa madai kuwa watauharibu.
 
Kwani safari hii kaandaa shilingi ngapi ya kuwahonga majaji make ya lwakatare aliandaa kiasi kikubwa.

Hivi rushwa tanzania imekuwa kubwa kiasi hata cha majaji kuhongwa? Basi takukuru if
utwe tu...ikiwezekana waondoke na bosi zao.
 
Back
Top Bottom