Mzee Mwanasiasa,
Majibu yako ni murua sana, isipokuwa binafsi nina maswali ya nyongeza,
(1). umekubali kuwa wafadhili wa Chadema ni pamoja na FREEMAN MBOWE, NDESAMBURO, na Mzee EDWIN MTEI, kipesa hawa tunafahamu kuwa ni wananchi wenye uwezo, sasa the fact kwamba wote ni kutoka kabila moja la eneo la Kaskazini, yaani Wachagga, huoni kwamba inaweza kuleta hisia mbele ya jamii kwamba huenda kuna cheche za ukabila ndani ya chama hicho cha taifa cha siasa, ambacho kikatiba ya taifa letu kinapaswa kuwa ni kioo chenye sura zote za taifa letu kuanzia kwenye level ya udhamini, mpaka viongozi na wanachama wake?
(2). Pia uamuzi wa kutumia helikopta wakati wa uchaguzi, nitashukuru kama utanifafanulia kama ni kweli ulikuwa ni wa kamati kuu ya chama hicho kama katiba ya chama hicho inavyosema, ninauliza hivyo kwa sababu kuna wagombea ubunge wa chama hicho ambao ilibidi wajitoe kwenye uchaguzi wa ubunge uliopita kutokana na kutokuwa na pesa za kuendesha kampeni kutoka kwenye mfuko wa chama hicho, huku mapesa mengi yakitumika katika kutumia chombo hicho ambacho ni cha kisasa, na ambacho sisi wananchi tunafahamu kuwa kinahitaji mapesa mengi kukitumia kwa ajili ya kampeni za uchaguzi kama kilivyotumika na chama hicho?
(3). Katika uchaguzi uliopita ni mafundisho gani Chadema imejifunza, kuanzia na positives na pia negatives as far as siasa na wananchi wa Tanzania yaani wapiga kura kwa ujumla is concerned?
Ahsante ndugu yangu na pia nitashukuru kama kuna na wengine wanaweza kuongezea majibu ya hayo maduku duku yangu!
Halafu nina mengine zaidi ya nyongeza tutaulizana as we go, Ahsante!