Mbowe na Dr. Slaa ndani ya Liberia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe na Dr. Slaa ndani ya Liberia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CPA, Mar 12, 2011.

 1. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 738
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Mbowe na dr. Slaa wameelekea liberia kuhudhuria mkutano mkuu wa vyama vya siasa africa unaofanyikia Liberia.

  =============
  UPDATE from IPP

  Viongozi wa kitaifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wameondoka nchini kwenda Liberia, kuhudhuria mkutano wa vyama vya kidemokrasia Afrika.

  iongozi hao ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, ambaye pia kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na Katibu Mkuu Dk. Wilibrod Slaa.

  Mkutano huo wa siku mbili unaanza leo na utahudhuriwa na viongozi wa vyama toka nchi mbalimbali za Afrika ambazo ni wanachama wa umoja huo.

  Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chadema, John Mnyika, ilieleza kuwa Mbowe na Dk. Slaa watapata pia fursa ya kukutana na Rais Ellen Johnson Sirleff wa Liberia ambaye ni Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika.

  Mkutano huo utaongozwa na Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Afrika Dk. Kizza Besigye, ambaye pia ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha FDC cha nchini Uganda.

  Pamoja na ajenda nyingine, mkutano huo pia utajadili hali ya kisiasa ya Afrika ya Kaskazini na mabadiliko ya msingi ya kimfumo katika uendeshaji wa uchaguzi barani Afrika.

  Aidha kupitia mkutano huo vyama shiriki vitabadilishana uzoefu kuhusu demokrasia na kuleta maendeleo katika maeneo yanayoongozwa na vyama wanachama wa umoja huo.
   
 2. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 916
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kama ndivyo, wapo ktk kutimiza majikumu yao ya kisiasa.
   
 3. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Wanaenda kudiscus nini?
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Tunawatakia mkutano mwema, tunaamini watakachojadili watatugawia.
   
 5. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,770
  Likes Received: 6,103
  Trophy Points: 280
  I hope wakirudi jamii itapewa taarifa/ripoti kamili ya yaliyojiri huko na safari yao ilikuwa na manufaa gani kwa chama chao na jamii kwa ujumla.

  Ni lazima wajitofautishe na wa upande wa pili. Mambo ya ukale/kizamani ya kufanya kila kitu SIRI yamepitwa na wakati. Siri siri nyingi kwa kawaida huwa hazijengi zaidi ya kuficha uozo kama ambavyo taifa limefikia hivi sasa. Tena ikiwezekana wafanye "Press Conference" pale pale airport na kueleza mambo kwa ufasaha. Hii ni muhimu sana na itasaidia kuongeza imani kwa umma.

  Hiki ni kizazi cha "Open Source"; let things be open.
   
 6. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  basi kuna chombo cha habari kimepotosha na kusema wameenda libya kwenye huo mkutano
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  inahuu?
   
 8. S

  Salimia JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 665
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi, kwanini asingekwenda kiongozi mmoja tu wa juu na mwingine akabaki? Au ndiyo uroho wa safari tu? Maana hapa akisafiri JK tu nongwa,, haya sasa hawa, mwenyekiti na katibu wote hao! Vipi tena hapa??? Ingeleta tija zaidi kama angekwenda Slaa na mtu kama Wenje au Mbowe na mwingine yeyote mpya kama Lissu aua Sugu ili kumjengea uzoefu wa kimataifa. Sasa magwiji yote mawili yanafuatana!

  Safari tamu jameni,, maana hapa tusimseme mwenzetu tu wa mlango wa pili.

  Napita tu lakini wakuu.
   
 9. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Ni mkutano wa vyama vya kidemokrasi barani afrika
   
 10. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  All the best my cdm leaders.
   
 11. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #11
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Kila la heri
   
 12. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Kabla hujatoa mrorongo wa maneno, inakupasa kufanya uchunguzi kwanza ni mkutano unahusu nini na ni nani mlengwa usipende kuongea sana. Usiwafananishe Mbowe, Dr Slaa na JK anayeenda kutoa mada kwenye mkutano.

  Jiulize ni mara ngapi umesikia watu hawa wakisafiri pamoja?

  Mkutano huo uliwahitaji wenyeviti na makatibu. Endelea kuanzia hapo. Be wise before you talk.
   
 13. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Afadhali hao wameenda wawili lakini unafikiri Kikwete huwa anaenda peke yake? Kikwete husafiri na kundi la watu wakiwemo mawaziri. Usihofu ndugu yetu kwani viongozi wa Chadema wanasafiri mara chache sana na nadhani hata wewe huwa huwasikii.

  Hata hivyo wao ndio viongozi wa wananchi maana sera za chama chao ndizo zinazotekelezwa ndio maana wakisema bei ya sukari imepanda serikali inaanza kuwaambia wafanyabiashara washushe bei.

  Tunawatakia safari njema
   
 14. S

  Selemani JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  The Monrovia meeting, according to Bakandonda, started yesterday and will end tomorrow. It is being attended by parties from various African countries, with a delegation from Britain and Norway.

  The Democratic Union of Africa brings together political parties with conservative related ideology. It is sponsored by the Conservative Party of Britain.

  Several top FDC leaders like Aswa MP Reagan Okumu, Odonga Otto, Bugweri MP Abdu Katuntu, FDC former Youth leader Ibrahim Kasozi and FDC vice-chairperson for Buganda Joyce Ssebugwawo have come out openly to oppose Besigye's call for protests and, instead, advised on shifting such efforts to rebuilding the party.
   
 15. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Umeniwahi mkuu,nawaza gharama za kwenda viongozi wote wakuu wa chama ambacho kina hitaji kujengwa vyema!
  Me naona tuna mlaum JK kwa safari bure,tuna laumu kwa sababu hatujapata hizo "chance"

  Huu ni ufujaji wa hela ya ruzuku,otherwise labda tuambiwe ni viongozi woote wa vyama walikuwa wana takiwa,.....mambo kama hayo ilibidi katibu mkuu ndo aya shughulikie kwa sasa maana ndo kazi yake,....

  Mbowe ni mbunge,pamoja na kwamba ni mwenyekiti wa chama huo ni "Uroho" wa safari!

  Mungu awajalie muingie ikulu tuwaone mtakavo safiri,i guess mtanunua ndege ya kifahari balaa kwa mtindo huu
   
 16. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #16
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Maneno ya mkosaji hayo,kwenye ukweli wala tusiupinge!

  Hata chadema kwa mtindo huu,.....wakipata uongozi,....ikatokea Dr.Slaa raisi,mbowe waziri mkuu,....duh kila safari lazima kundi mara3 ya kikwete watasafiri!

  Uaminifu unaonekana kwanza katika kidogo ulicho nacho,huwezi kuwa mfujaji wa kidogo ulicho nacho afu unasema "mimi sio mfujaji kama yule tajiri".............................zinduka,kemea tabia kama hizi,......mkiziendekeza ndami ya chama mtakuja kuona aibu pale chama pinzani enzi zijazo (ccm) watakapo kuwa wana wasema na nyie kwa safari
   
 17. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #17
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mkuu salamu.

  Msiwe wepesi kuanza kulaumu kabla hamjapata taarifa za kutosha. Ulipaswa kwanza kuuliza details za huo mkutano sio kuanza kurusha mawe. Information is Power.

  Mkutano ni wa Viongozi Wakuu wa Vyama Vya Kidemokrasia Vya Afrika - Democratic Union Of Africa (DUA). Unawahusu Viongozi Wakuu tu, Mwenyekiti na Katibu Mkuu na sio Wabunge wala Watendaji wengine. Wanahitajika watu ambao ni well informed kuhusu chama na wanafahamu background ya DUA. Wanapaswa kuwa wote ili wasaidiane sio mkutanoa wa kuwakilishwa. Vile Vile Hon Mbowe ameandaliwa hafla ndogo ya kumpongeza kwa kuwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni (KUB), kwahiyo kwa namna yeyote ile Mbowe supposed to be there.

  Katika Mikutano yao yote huwa hakuna Perdiem isipokuwa Umoja huu hugharamia Usafiri, Chakula na Malazi. Unaenda na kurudi kama ulivyoenda bila fedha yeyote kutoka kwa waandaaji au wafadhili.

  No Data No Right to Speak
   
 18. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #18
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Regia bora umefafanua,maana walishaanza,,
   
 19. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #19
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Are You sure Bwana/Bibi Selemani?Nenda kasome vizuri acha kupotosha umma.
   
 20. S

  Selemani JF-Expert Member

  #20
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wewe ndio unapotosha umma. DUA is sponsored by the conservative party of Britain, and the right wing ideological. Na ndio waliotoa fedha kwa viongozi wako kwenda huko Liberia. Those are the facts. It is embarrassing wewe kama muwakilishi wa kina mama unataka kubend facts humu ndani.

  Its all known kwamba Torries are funding Chadema, they want an ideological partner in Tanzania for their religious and economical ideology. Huo ndio ukweli.

  New Vision Online : FDC's Besigye flies out for consultations
   
Loading...