Rais Dkt. Mwinyi akutana na Mwenyekiti wa Chama cha Wajane Afrika

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mwenyekiti wa Chama cha Wajane Afrika (TAWS), Hope Nwakwesi na ujumbe wake Ikulu Zanzibar tarehe: 19 Desemba, 2023.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali inathamini haki za wajane.

Naye, Mwenyekiti wa Wajane Afrika Hope Nwakwesi amemweleza Mh. Rais Dk. Mwinyi kuhusu kufanyika Zanzibar mkutano mkubwa wa Wajane Afrika utakaoshirikisha nchi zaidi ya 54 kuanzia tarehe 20,21 na 22 Juni mwaka 2024.

Mkutano huo utajadili changamoto, masuala yanayohusu wajane na kutafuta ufumbuzi.

Halikadhalika Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali itajitahidi kusimamia kuhakikisha mkutano huo unakwenda vizuri.
IMG-20231219-WA0026.jpg
IMG-20231219-WA0027.jpg
IMG-20231219-WA0028.jpg
IMG-20231219-WA0025.jpg
IMG-20231219-WA0024.jpg
IMG-20231219-WA0021.jpg
IMG-20231219-WA0023.jpg
IMG-20231219-WA0022.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom