Mbowe na Dr. Slaa ndani ya Liberia

Mzee Analysis yako iko juu nimekubali. Nako CCM ni kama hivi:

1. CCM- Uadilifu (Wazee wenzake na Mwalimu Nyerere ambao ni watulivu, wakomavu na masikini wa kutupwa kwa kuipenda sana nchi na wenye moyo kuitetea Tanzania).

2. CCM- Ufisadi ( Ni kundi dogo linalojiita Wanamtandao au kumbakumba wa kila dili / mchecheto wa kila senti irukayo hewani wenye utayari wa kuuza hata mtoto wake alimradi fedha ipatikane zaidi kufanyia kila aina ya uchafu unaoweza kufikiria; ni wale ambao mpaka hivi sasa wamepepetwana pembeni wasio na kitu na kubakia RA + EL).

3. CCM-Unguja (Chama cha Wazanzibara kama Vuai wa Kondoa na Hussein Mwinyi wa Kisarawe Umatumbini).

4. CCM-Yatima (Ni wale akina Sumaye, Kigoda, Mungai, banduka, Komanya, Ngulume, na wengine waliokua chini ya BWM).

5. CCM-Bongo Flava (Rizi1, Februari Ma-Ropes, Ndungai, Malisa, Nchimbi, ... hawa hawana hela ila kamsimamo wa uongo na kweli)

6. CCM-Mwandosya / Mangula (Kanda ya Juu Kusini)

7. CCM- Six/John Liquor Ma-Padlocks (Kanda ya Ziwa)

8. CCM- Two Coins Mramba / Mrema / Mbatia (moshi Vijijini)

9. CCM-Uislamu (Pwani/ Tanga / Mashariki na Pemba)

Sasa hapa mtu unapoongelea CCM ni sharti uwe makini sana sana na ijulikane kwamba unazungumzia CCM ipi hasa.
Kweli kuna CCM za aina nyingi
Kuna kundi jingine umelisahau CCM- Malapulapu wanaoshinda humu kushangia wenzao walio kwenye mechi kwa kuambulia nauli za daladala.

Hivi Magufuli yuko CCM ipi?

8. CCM- Two Coins Mramba / Mrema / Mbatia (moshi Vijijini) + Lipumba + Seifu+ Kafulila
 
Back
Top Bottom