Mbowe na Dr. Slaa ndani ya Liberia

Selemani said:
Nenda kaangalie website ya DUA and what they believe in, halafu njoo tena ujibu hoja. DUA, through global conservative coalition sponsors parties who believe in "free market economy and the policy of reducing the size and scope of government provide the best means of creating the wealth and material prosperity to meet the legitimate aspirations of individuals".

Selemani,

..sasa mbona CCM nao kwenye makaratasi wameandika ni Wajamaa?

..je, in practice unaweza kusema kwa uhakika kwamba hicho ndicho wanachofuata?

..huu UFISADI wa CCM si bora hata hao ma-Conservative.
 
Hivi unajua mheshimiwa Rais akisafiri hata nchi jirani huwa anaondoka na watu wangapi kweli?
Hapo sawa mkuu. Umesema "Mheshimiwa Rais" akisafiri hata nchi jirani. Hujasema JK. Swali ni kwamba leo hii Mheshimiwa Rais akawa SLAA,, akaenda nchi jirani atakwenda na watu wangapi?

Napita wakuu
 
hivi does a mistake justify th mistake?
sijakuelewa mkuu ,so unalipiza kisasi cha jk kusemwa au unatoa facts?
Hakuna anayelipiza kisasi hapa,, tunatumia "logic" kutokana na comments za watu humu ili kuonyesha wkamba ni comments za kutumwa au za chuki binafsi. Logic ni kujiuliza kwamba kwa conditions zile zile, kibao kikabadilika,, watasema nini hawa? maana yake ni kwamba unapotoa comments humu usilete ushabiki, hoja zako ziwe valid kwa whoever is in the power. Iweje leo hoja hizo zimhukumu tu JK, na hoja hizo hizo zionekane sawa tu kwa mwingine. Common sense is not common.
 
Salimia,

Salamu toka Monrovia. Kama sikosei nilikwisha kufanya posting kwenye Jamvi hili kutoka hapa Monrovia tulipokuwa tu tumewasili hapa tarehe 9 Machi, 2011. Nilieleza kuwa tuko hapa na Mheshimiwa Mwenyekiti wa Taifa kuhudhuria Mkutano wa Mwaka wa Democratic Union of Africa, (DUA) ambayo wengi wenu watakumbuka hadi 2009 Chadema ilikuwa Secretariat, na NPP ya Ghana ilikuwa mwenyekiti.

DUA ni Chapter ya Africa ya vyama vya mrengo wa "Centre Centre Parties" katika mfumo wa vyama vya siasa Duniani na wote tunaunganika katika International Democratic Union kwa Dunia nzuri. Wanachama ni pamoja na vyama tawala katika nchi zao na au vyama vya upinzani ikikumbukwa kuwa kutawala au kutokutawala kwa wanaoelewa demokrasia ni swala la kupokezana vijiti. Hivyo kinachotuunganisha ni "values" au mambo tunayosimamia katika jamii.

Kama nilivyosema huu ni mkutano wa Mwaka yaani Annual General meeting, na wajumbe ni wenyeviti na Makatibu wakuu. Si kosa lako inawezekana umechangia bila kufahamu Katiba ya umoja huo. Mkutano una sehemu kubwa mbili, Deliberative Session, ambayo theme yake ni "Re-bilding the blocks of Democracy in Africa". Mhe. Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinani Bungeni alitoa Mada kuhusu "Consolidating Democracy -Tanzania Election and Aftermath".

Mkutano pia umejadili Trends zinaziojitokeza katika Demokrasia Afrika mifano ya Afrika Kaskazini, Ivory Cost,Kenya na Zimbabwe. Hakuna siri katika Democrasia na kesho Mkutanpo utatoa Tamko rasmi kutokana na mambo yaliyojitokeza katika deliberative Session. Sehemu ya pili na maswala zaidi ya uongozi wa umoja wenyewe Dua. Nadhani ulinganisho na upande mwingine ungelikuwa na maana iwapo "wakubwa" hao wangelikuwa wanahudhuria tu semina ambayo hata mtu mwingine angeliweza kuhudhuria.

Hivi, kwanini asingekwenda kiongozi mmoja tu wa juu na mwingine akabaki? Au ndiyo uroho wa safari tu? Maana hapa akisafiri JK tu nongwa,, haya sasa hawa, mwenyekiti na katibu wote hao! Vipi tena hapa??? Ingeleta tija zaidi kama angekwenda Slaa na mtu kama Wenje au Mbowe na mwingine yeyote mpya kama Lissu aua Sugu ili kumjengea uzoefu wa kimataifa. Sasa magwiji yote mawili yanafuatana!

Safari tamu jameni,, maana hapa tusimseme mwenzetu tu wa mlango wa pili.

Napita tu lakini wakuu.
 
Salimia,

Salamu toka Monrovia. Kama sikosei nilikwisha kufanya posting kwenye Jamvi hili kutoka hapa Monrovia tulipokuwa tu tumewasili hapa tarehe 9 Machi, 2011. Nilieleza kuwa tuko hapa na Mheshimiwa Mwenyekiti wa Taifa kuhudhuria Mkutano wa Mwaka wa Democratic Union of Africa, (DUA) ambayo wengi wenu watakumbuka hadi 2009 Chadema ilikuwa Secretariat, na NPP ya Ghana ilikuwa mwenyekiti.

DUA ni Chapter ya Africa ya vyama vya mrengo wa "Centre Centre Parties" katika mfumo wa vyama vya siasa Duniani na wote tunaunganika katika International Democratic Union kwa Dunia nzuri. Wanachama ni pamoja na vyama tawala katika nchi zao na au vyama vya upinzani ikikumbukwa kuwa kutawala au kutokutawala kwa wanaoelewa demokrasia ni swala la kupokezana vijiti. Hivyo kinachotuunganisha ni "values" au mambo tunayosimamia katika jamii.

Kama nilivyosema huu ni mkutano wa Mwaka yaani Annual General meeting, na wajumbe ni wenyeviti na Makatibu wakuu. Si kosa lako inawezekana umechangia bila kufahamu Katiba ya umoja huo. Mkutano una sehemu kubwa mbili, Deliberative Session, ambayo theme yake ni "Re-bilding the blocks of Democracy in Africa". Mhe. Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinani Bungeni alitoa Mada kuhusu "Consolidating Democracy -Tanzania Election and Aftermath".

Mkutano pia umejadili Trends zinaziojitokeza katika Demokrasia Afrika mifano ya Afrika Kaskazini, Ivory Cost,Kenya na Zimbabwe. Hakuna siri katika Democrasia na kesho Mkutanpo utatoa Tamko rasmi kutokana na mambo yaliyojitokeza katika deliberative Session. Sehemu ya pili na maswala zaidi ya uongozi wa umoja wenyewe Dua. Nadhani ulinganisho na upande mwingine ungelikuwa na maana iwapo "wakubwa" hao wangelikuwa wanahudhuria tu semina ambayo hata mtu mwingine angeliweza kuhudhuria.

U meant to say Center-Right Muheshimiwa. Not Center-Center. In light of transparency, tuambie hao wadau kutoka Norway na UK wana uhusiano gani na DUA--na Chadema.

And stop saying kwenye majukwaa kwamba unataka Tanzania iwe Tunisia. That is gross irresponsibility on your part. Words matters, and as u aspire to be a statesman, we would like if you pay attention to what u say Majukwaani. Mifano--Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga amekufa, au Kontena la shahada la kura limevuka Tunduma, au Kikwete owns Dowans. Those were FALSE statements, coming from your mouth Muheshimiwa. Throngs of people believe you and u need to take that serious, and not feed your followers with statements za uongo.

Ni hayo tu. Tunashukuru kwa Changamoto unayotoa kuchochea maendeleo.
 
Hivi Regia Mtema do you understand what a conservative ideology is? Kiitikadi Chadema haijulikani kwa sababu mnaficha makucha yenu. Au you are a nobody in the party kwa hiyo nobody tell u anything significant. The way Mtei and Mbowe run the party kama biashara ya kifamalia, the rest of u are as clueless as Jambo Forum members. .

you are one of them.
 
U meant to say Center-Right Muheshimiwa. Not Center-Center. In light of transparency, tuambie hao wadau kutoka Norway na UK wana uhusiano gani na DUA--na Chadema.

And stop saying kwenye majukwaa kwamba unataka Tanzania iwe Tunisia. That is gross irresponsibility on your part. Words matters, and as u aspire to be a statesman, we would like if you pay attention to what u say Majukwaani. .

the same standard should be used on Kikwete.. ana ushahidi mkubwa wa kauli nyingi za uongo ambazo hazijawahi kuhojiwa na watu wengine. Kuanzia alipolidanganya taifa kuwa "Watanzania hawali mapanki" hadi madai ya kuwa "siwajui Dowans".
 
Selemani,

Nakushukuru sana kwa ushauri. Ushauri wowote unaotolewa una thamani na unastahili klufanyiwa kazi.Kwa msingi huo huo naomba nawe ukubali ushauri:

1) Kwenye mikutano ya hadhara statements zinazosemwa mara nyingi sizo zinazorepotiwa "Verbatim" Ni vema kabla hajahukumu ukafanya uchunguzi wa kina kama ulichosoma ndicho kilichosemwa na mhusika au Gazetu unalosoma au chombo unachotazama kwa sababu wanazojua wamechakachua au kutoa sehemu na hivyo kuripoti out of context. Nikukuuliza ni nani kati ya wanachadema amesema "Nataka Tanzania iwe Tunisia" sijui kama unaweza kumtaja. Labda nikusaidie tu, Tunisia, Egypt, Yemen, etc ni current affairs na kutoa mfano si dhambi. Kwenye siasa ni muhimu kujua "exact language iliyotumika" vinginevyo wewe ndiyo utaponekana wa ajabu. Mikutano yote hakuna hata moja ambako Usalama wa Taifa hawajahudhuria na kama unayosema ni kweli leo tungelikuwa magerezani tayari. Jiulize ni kwanini Serikali inapata kigugumizi kutufungulia mashitaka. Vinginevyo labda wajaribu kuchakachua kama walivyofanya wakati wa mauaji ya Arusha. Sasa usubiri jinsi watakavyishushuliwa mahakamani.

2) Mwenye uwezo wa kuhukumu na au kushauri authiritatiuvely ni yule aliyesikia "kauli" kwa masikio yake.Vinginevyo ni hatari zaidi kufanya kazi na "hearsay", kwa kuwa utawajengea watu hofu ambayo haipo.

3) Its being blind not to realise hali tete ya Tanzania. Watanzania huhitaji kuwafundisha kuwa "kama Tunisia,Misri etc" Wanaona kwa macho yao wenyewe. Watanzania saa hizi wako mbele kuliko sisi, na kama siyo kuwapoza sisi hali ingelikuwa tayari. Asiyetaka kuona hilo ni "kipofu" bila sababu (siyo wasioona kuna tofauti ya msingi sana). Unahitaji tu kwenye mikutano mabango yanayoandikwa, nani kawafundisha. Wakati wa kufanya mchezo wa Bundi umeisha. Let us be realistic and come out of our cages tutaokoa Taifa letu. Taifa haliokolewi kwa kujenga hofu bali kwa "kuondoa kero", kufanyia kazi kero za watu, kujibu hoja zilizoko kwa hoja". Mbinu za mwaka 47 hazina nafasi tena.

4) Ni vizuri ungeliuliza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza alisemwa kuwa kafa katika mazingira gani, na lugha ipi ilitumika. Ukweli ni kuwa nikiwa Shinyanga nilimsema sana Dr Ballele kwa kuwafanyia Watanzania majaribio ya Dawa inayoitwa Virodine iliyotengenezwa Afrika Kusini kama dawa ya Ukimwi, lakini ikapigwa marufuku Afrika Kusini. Bila kibali cha NIMRI, au mamlaka nyingine yeyote, Dr alifanyia majaribio kwa Watanzania bila vibali husika na wengine walitumika kupitia zahanati ya bwana Mahita (wakati huo IGP jambo ambalo ni kinyume na maadili. Taarifa hizi ziko pia kwenye Hansard ya Bunge kama unahitaji. Maswa wakati nataka kumsema Dr Ballele ndipo nikaletewa "Taarifa kuwa kafariki" na source ilikuwa Jamvi hili (kama chombo cha habari) na mimi nikasema " kama Taarifa hizi ni kweli...." Unahitaji kuwa makini sana unaponukuu kauli za watu ambao wewe mwenyewe hujazisikia. Ndio maana walioshikia bango hawakuweza kuendelea.

Usisahau kwa sheria za Tanzania "Evidence Act"(RE) ushahidi wa mtandao unakubalika. Hivyo tatizo Slaa au aliyeandioka kwenye mtandao kuwa yuko "kwenye eneo la tukio"...Wengine tumefundishwa kuwa makini sana kwa kadiri inavyowezekana kibinadamu. Hivyo ndugu yangu pamoja na kupokea ushauri wako, katika mambo uliyoshauri ushauri wako una madosari kibao.

Hata hivyo nauheshimu kwa kuwa ni ushauri, lakini ushauri ni lazima upokelewe au kufuatwa.....!
 
Mkuu salamu.Msiwe wepesi kuanza kulaumu kabla hamjapata taarifa za kutosha.Ulipaswa kwanza kuuliza details za huo mkutano sio kuunza kurusha mawe.Information is Power.

Mkutano ni wa Viongozi Wakuu wa Vyama Vya Kidemokrasia Vya Afrika(DUA)Democratic Union Of Africa.Unawahusu Viongozi Wakuu tu,Mwenyekiti na Katibu Mkuu na sio Wabunge wala Watendaji wengine.Wanahitajika watu ambao ni well informed kuhusu chama na wanafahamu background ya DUA.Wanapaswa kuwa wote ili wasaidiane sio mkutanoa wa kuwakilishwa. Vile Vile Hon Mbowe ameandaliwa hafla ndogo ya kumpongeza kwa kuwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni(KUB),kwahiyo kwa namna yeyote ile Mbowe supposed to be there.

Katika Mikutano yao yote huwa hakuna Perdiem isipokuwa Umoja huu hugharamia Usafiri,Chakula na Malazi.Unaenda na kurudi kama ulivyoenda bila fedha yeyote kutoka kwa waandaaji au wafadhili.

No Data No Right to Speech.

Shukrani Regia,
Kwa kuongezea kwa faida ya wanaJF kujua Democratic Union of Africa pata picha kibao za 'slide show' na habari kemkem za kilichojiri kwa kugonga hapa http://www.du-africa.org/
 
Kabla hujatoa mrorongo wa maneno ,inakupasa kufanya uchunguzi kwanza ni mkutano unahusu nini na ni nani mlengwa usipende kuongea sana.Usiwafananishe Mboye,Dr Slaa na JK anayeenda kutoa mada kwenye mkutano.Jiulize ni mara ngapi umesikia watu hawa wakisafiri pamoja?

Mkutano huo uliwahitaji wenyeviti na makatibu.Endelea kuanzia hapo.Be wise before you talk.

Good,manake majitu mengine yanapeenda kuongea sana!!!Asante kwa kunisaidia kumjibu maana ningemjibu mm nahisi nisingepata maneno malaini kama uliotumia.
 
Salimia,

Salamu toka Monrovia. Kama sikosei nilikwisha kufanya posting kwenye Jamvi hili kutoka hapa Monrovia tulipokuwa tu tumewasili hapa tarehe 9 Machi, 2011. Nilieleza kuwa tuko hapa na Mheshimiwa Mwenyekiti wa Taifa kuhudhuria Mkutano wa Mwaka wa Democratic Union of Africa, (DUA) ambayo wengi wenu watakumbuka hadi 2009 Chadema ilikuwa Secretariat, na NPP ya Ghana ilikuwa mwenyekiti.

DUA ni Chapter ya Africa ya vyama vya mrengo wa "Centre Centre Parties" katika mfumo wa vyama vya siasa Duniani na wote tunaunganika katika International Democratic Union kwa Dunia nzuri. Wanachama ni pamoja na vyama tawala katika nchi zao na au vyama vya upinzani ikikumbukwa kuwa kutawala au kutokutawala kwa wanaoelewa demokrasia ni swala la kupokezana vijiti. Hivyo kinachotuunganisha ni "values" au mambo tunayosimamia katika jamii.

Kama nilivyosema huu ni mkutano wa Mwaka yaani Annual General meeting, na wajumbe ni wenyeviti na Makatibu wakuu. Si kosa lako inawezekana umechangia bila kufahamu Katiba ya umoja huo. Mkutano una sehemu kubwa mbili, Deliberative Session, ambayo theme yake ni "Re-bilding the blocks of Democracy in Africa". Mhe. Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinani Bungeni alitoa Mada kuhusu "Consolidating Democracy -Tanzania Election and Aftermath".

Mkutano pia umejadili Trends zinaziojitokeza katika Demokrasia Afrika mifano ya Afrika Kaskazini, Ivory Cost,Kenya na Zimbabwe. Hakuna siri katika Democrasia na kesho Mkutanpo utatoa Tamko rasmi kutokana na mambo yaliyojitokeza katika deliberative Session. Sehemu ya pili na maswala zaidi ya uongozi wa umoja wenyewe DUA. Nadhani ulinganisho na upande mwingine ungelikuwa na maana iwapo "wakubwa" hao wangelikuwa wanahudhuria tu semina ambayo hata mtu mwingine angeliweza kuhudhuria.

Mh.Slaa, salaam:
Nakushukuru sana kwa majibu yako ya kistaarabu yaliyojaa hekima iliyotukuka. Natamani na wafuasi wako humu watakuwa wamejifunza toka kwako namna ya kutoa au kuchangia mada kwa lugha za kistaarabu zisizo na matusi na kashfa.
 
Naloli,, while agree with you in red but also when JK went to Ethiopia it was well known that: "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Machi 9, 2011, anaungana na marais wenzake wa Afrika waliopewa jukumu la kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa katika nchi ya Afrika Magharibi ya Ivory Coast, katika hatua za mwisho za jitihada za kujaribu kumaliza mgogoro huo.

Rais Kikwete na marais wenzake wanakutana mjini Addis Ababa, Ethiopia, katika jitihada mpya za kutafuta jawabu la mzozo huo uliolipuka mwishoni mwa mwaka jana kufuatia matokeo ya raundi ya pili ya uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo uliofanyika Novemba 28, 2011."

But, ukiangalia comments za watu (walwale watakatifu na wateule) utashangaa sana.
Mtu kama Zegreaty aliandika "vp kaenda kutalii?"
nngu007 akaandika "Anaogopa kukaa nyumbani kusikiliza matatizo ya wananchi; Ni bora kwenda nje na kula vizuri"
CAMARADERIE akasema "Baba wa kufikia kwa kuwa mimba (kura) si yake"

Na mengine mengi tu na matusi juu just to quote a few here.
Point yangu ni ile ile kwamba,, huku kusema au kutuambia tufanye utafiti kabla ya kulalamika,, kuwiane na mlango wa pili pia. Watelule au malaika wa upande wa pili wao wamakurupuka tu na matusi juu, mbona huwa hamuwaambii wafanye utafiti pia? Tusilalamike tu kwa ujumbe au posts za kujifurahisha au kuchangamsha baraza kama hizo chache nilizozi quote hapo juu. Msumeno unakata kotekote mazee na huo unaowahusu SLAA na MBOWE ndiyo huo huo pia unamhusu JK na timu yake.
Napita wakuu
Salimia kuna watu humu JF wao ni wakereketwa/wafurukutwa wa CDM yaani wao ni kuwa hakuna zuri la CCM na hakuna baya la CDM wao siku zote ni kupinga na kukashifu ccm na vyama vingine na kutukuza CDM. Ni vyema na wewe usijiunganishe nao kwa kupinga kila jambo la CDM na kutetea kila jambo la CCM. Hapo tukiviweka vyama vyote na wanasiasa wote ktk mizania iliyo sawa tutaipeleka nchi yetu sehemu sahihi.

Mwanasiasa akiboronga bila kujali chama atokacho apewe ukweli wake na kushutumiwa kwa uasi kwa Taifa lake lakini akifanya vizuri asifiwe bila kujali chama chake.
 
Hivi, kwanini asingekwenda kiongozi mmoja tu wa juu na mwingine akabaki? Au ndiyo uroho wa safari tu? Maana hapa akisafiri JK tu nongwa,, haya sasa hawa, mwenyekiti na katibu wote hao! Vipi tena hapa??? Ingeleta tija zaidi kama angekwenda Slaa na mtu kama Wenje au Mbowe na mwingine yeyote mpya kama Lissu aua Sugu ili kumjengea uzoefu wa kimataifa. Sasa magwiji yote mawili yanafuatana! Safari tamu jameni,, maana hapa tusimseme mwenzetu tu wa mlango wa pili. Ama labda kama kwa "Babu" dozi haikufua dafu wanafuata nyingine huko.
Napita tu lakini wakuu.

Inategemea na mwaliko ulivyo...kama wanatakiwa viongozi wawili je? Halafu usilinganishe safari za JK na hizi...JK anatumia kodi zetu nyingi kwa safari moja...hawa wamepewa mwaliko...kukosoa safari zisizo tija za JK hakuzuii wengine kusafiri...ni sawa kujadili ajambaye chooni na yule ajambaye jikoni...si sawa
 
Salimia kuna watu humu JF wao ni wakereketwa/wafurukutwa wa CDM yaani wao ni kuwa hakuna zuri la CCM na hakuna baya la CDM wao siku zote ni kupinga na kukashifu ccm na vyama vingine na kutukuza CDM. Ni vyema na wewe usijiunganishe nao kwa kupinga kila jambo la CDM na kutetea kila jambo la CCM. Hapo tukiviweka vyama vyote na wanasiasa wote ktk mizania iliyo sawa tutaipeleka nchi yetu sehemu sahihi.

Mwanasiasa akiboronga bila kujali chama atokacho apewe ukweli wake na kushutumiwa kwa uasi kwa Taifa lake lakini akifanya vizuri asifiwe bila kujali chama chake.
Naloli,
Umesema sahihi kabisa, mimi sina ushabiki wa chama chochote nakaa kwenye haki tu, na ndiyo maana kama umesemo vyema hapo juu baada ya W.Slaa kunijibu,, nilimshukuru na sikuendeleza ligi. Maana yake ni kwamba,, lile swali nililouliza kwamba kwanini asingenda mmoja tu, W.Slaa amenijibu vyema na nimeelewa.

Je uliona nimepinga baada ya uelewesho wa W.SLAA?
 
SAaaaaaaaafi. Nendeni mjinoe tuje tuibandue ccm madarakani imeanza kuvunda
 
Inategemea na mwaliko ulivyo...kama wanatakiwa viongozi wawili je? Halafu usilinganishe safari za JK na hizi...JK anatumia kodi zetu nyingi kwa safari moja...hawa wamepewa mwaliko...kukosoa safari zisizo tija za JK hakuzuii wengine kusafiri...ni sawa kujadili ajambaye chooni na yule ajambaye jikoni...si sawa
Ningekuwa wewe,, nisinge comment tena baada ya W.Slaa kutoa ufafanuzi wa kina na kwa lugha yenye staha. Ni kama unachafua kile ambacho kiongozi wako amekiongea kwa usafi. Hata lugha yako tu, ukilinganisha na aliyotoa W.Slaa, ni kama usiku na mchana kwa kifupi unamdhalilisha W.Slaa.

Ushauri: Kiongozi wenu mkubwa ameshatoa ufafanuzi,, sasa ninyi kaeni kimya msiharibu kile alichosema.

Inueni mioyo.
 
Mikutano hii inamanufaa kwa wananchi wetu na chama chetu cha cdm...

Waende salama na mkutano mwema... Na warudi salama wapiganaji wetu..
 
Mh. Dr. Slaa salaam;

Tunashukuru sana kwa kujibu baadhi ya hoja humu JF. Hakika ni viongozi wachache Afrika wenye uthubutu huo. Kama sijakosea, jana kwenye thread nyingine inayofanana na hii, nilishauri ingekuwa vizuri pindi mnaporejea kutoka kwenye safari muhimu hama hii ya Liberia angalau kabla mambo hayajapoa mkaitisha "Press Conference" pale pale airport (JNIA) ili kuufahamisha umma juu ya safari yenu na yote yaliyojiri huko. Hii itasaidia sana kuongeza imani ya umma kwenu na chama chenu pamoja na kuondoa tetesi ambazo hazina msingi; kama ujuavyo taifa hili kwa uvumi pengine linaongoza.

Hivyo, kama bado hamjarudi, Ofisi husika ifanye maandalizi muhimu ili muweze kukutana na umma kupitia waandishi wa habari. Haina haja kufanya kama wengine kwamba lazima wachakachue ndipo ofisi ya mahusiano itoe taarifa baada ya uchakachuaji. Jiepusheni na kufanya kila kitu SIRI.
 
Ningekuwa wewe,, nisinge comment tena baada ya W.Slaa kutoa ufafanuzi wa kina na kwa lugha yenye staha. Ni kama unachafua kile ambacho kiongozi wako amekiongea kwa usafi. Hata lugha yako tu, ukilinganisha na aliyotoa W.Slaa, ni kama usiku na mchana kwa kifupi unamdhalilisha W.Slaa.
Ushauri: Kiongozi wenu mkubwa ameshatoa ufafanuzi,, sasa ninyi kaeni kimya msiharibu kile alichosema.
Inueni mioyo.

Wewe nani unipangie namna ya kukuelewesha? Mimi si sawa na Dr...YEYE ANAUWEZO MARADUFU YANGU...na bado humuelewi. Mimi nimekuelewesha kulingana na ubongo wako finyu...usinichonganishe na kiongozi wangu...niko huru kutoa mawazo yangu nitakavyo na ukipenda unihukumu mimi bila kumhusisha Dr..sawasawa?
 
Naloli,
Hapo palipo wekundu,, ni kujua huko huko kwamba urais ni taasisi na si mtu mmoja, itakupa maana kwamba si lazima Rai abaki nchini kutekeleza jukumu fulani, basi "taasisi" itatekeleza on his absence. Sasa hii taasisi tunaitambua tu kwa yeye kusafiri nje?? Vipi kubaki ndani?
Pia unasema kwamba waziri wa mambo ya nje anaweza kumuwakilisha,, hilo ni kweli,, sasa nani kakwambia kwamba waziri wa mambo ya nje anakwenda peke yake bila watu? Acha kukurupuka.
Nitarudi
Kumbuka kuwa dhamana ya URAIS kapewa RAIS ingawa URAIS ni Taasisi, hatasiku moja nchi ikiendeshwa ndivyo sivyo hawatolaumiwa wasaidizi bali atalaumiwa aliyepewa jukumu hilo, ndio maana viongozi maRais makini hawaendi safari za nje kama watalii, wanajua wazi uzito wa majukumu ya Rais hata siku moja Rais hawezi kutegemea wasaidizi wake ktk mambo mazito ya nchi anapaswa kujua wazi kuwa hilo ni jukumu lake yeye, kumbuka hakuna jambo zito ktk uongozi kama kufanya uamuzi (decision) ndio maana katiba imetoa msamahaa wa Rais kushtakiwa kwa makosa atakayoyafanya wakati wa kutekeleza majukumu yake ya Urais (kwa maslahi ya Taifa) uhuo msamaha hauwagusi wasaidi wake ingawa URAIS NI TAASISI(Salimia fukunguka macho). Hata Mwl. Nyerere alipaswa kusema kuwa "Urais ni mzigo maana ukiona ombaomba barabarani, Nyumba za nyasi na zisizo bora, Baa la njaa ktk nchi wote huo ni mzigo wa Rais maana yeye ndiye aliye ahidi kuwaondolea matatizo yote hayo na kupewa dhamana hiyo na watu wake"
Hapo nakushangaa Salimia unapotoka mapovu kutaka kufanya ulinganisho wa safari ya Rais na Safari ya SLAA au MBOWE, kumbuka DKT. JK ni Rais wa Watanzania wote bila kujali vyama vyao, dini zao au makabila yao. Lakini DKT SLAA na MBOWE ni viongozi wa CHADEMA. Elewa kuwa kwa maisha yake yote kwa kipindi cha miaka kumi DKT KIKWETE atakuwa anaishi kwa fedha za walipa kodi wa Tanzania tofauti na DKT SLAA na MBOWE hivyo usishangae watu wakimbana sana JK kuhusiana hata na maisha yake na familia yake, hivyo suala la safari za nje ni sehemu moja tu ktk mambo mengi ya kumbana.

Sijakwambia waziri wa mambo ya nje anakwenda safari za nje peke yake sijapata kusema hivyo hata siku moja. Tatizo lako uelewi kabisa hata protocal zinazohusu safari ya RAIS kuwa ni tofauti na zinazohusu safari ya waziri wa mambo ya nje. Elewa kuwa Rais kabla hajasafiri lazima timu ya Usalama wa Taifa iwahi kwenda nchi ambayo Rais atatembelea si chini ya siku tatu kabla Rais ajasafiri, hizo zote ni gharama za safari ya Rais, ambapo kwa waziri hiko kitu hakuna, pili Rais anawasaidizi wake kama waandishi, Daktari, wabeba makarabrasha, mkewe (pale anapoamua kwenda nae) na wataalam(watendaji ambao ziara hiyo inahusu sekta yao) wote hao ni sehemu ya msafara wake, wakati mwingine hutumika ndege ya Raisi kumbuka watumishi wote ktk ndege hiyo na gharama za uendeshaji wa ndege hiyo ulipwa na kodi zetu. Wakati waziri yeye ataambatana na wataalam(watendaji wa sekta husika tu) sasa bado huoni unafuu wa safari zisizo muhimu kuwakilishwa na Waziri wa Sekta husika au Waziri wa Mambo ya Nje? Nimekupa mfano wa uamuzi wa Rais wa Malawi Bingu Wamuthatika kuamua kuwa kuwakilishwa na Mabalozi wake waliopo nje ya nchi na ikibidi waziri wa mambo ya ndani au mawaziri wa kisekta ili yeye abaki kushughulikia mambo ya kimsingi nchini kwake. J e Bingu si niRais wa nchi kama JK mbona unakuwa na mahaba ya kumbenda vibaya wewe?

Kumbuka Taifa kwanza vyama, dini na makabila baadae, usiwe unatetea tu ilimradi uonekane ni muaminifu kwa chama chako na Rais wenu, mwambieni ukweli Rais wenu ndipo mtamsaidia kujifanya watetezi hata kwa mambo ambayo hata mtoto mdogo anaona Rais au Serikali inachemsha hakumsaidii Rais, Angalia Waziri Sitta anavyomsaidia Rais kwa kumuambia ukweli hata kama nyinyi na Rais amuupendi lakini ndio ukweli, Na ndivyo wasaidizi wa Rais wanavyopaswa kuwa na si kukimbilia PERDIEM za nje ya nchi tu. SALIMIA funguka macho huu sio wakati wa ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI, UZALENDO kwa nchi yetu kwanza.
 
Back
Top Bottom