Mbowe na Dr Slaa, natoa saa 24!

Mbowe na Dr Slaa, natoa saa 24!

Status
Not open for further replies.
sifongo

Ni kweli kabisa, hawa watu wa chadema inaonesha wameshiba ruzuku zinazotokana na kodi tunazokatwa kwenye mishahara yetu na biashara zetu wanaanza kutunishiana misuli. Tusiruhusu

Njia ya muongo ni fupi sana hapo kwenye RED umejidhihirisha kuwa wewe si CHADEMA kama ni CHADEMA basi ni PANDIKIZI.
 
Sisi tunaokukosoa tuna upeo kuliko wanaokusifia kinafiki. UNamkosoa LEMA kutumia mitandao kosa ambalo hata MWIGAMBA alilitenda na wewe unaanzisha mada ileile!

Mwigamba yule ni Mjinga. Usinifananishe nae. Mimi ninachopinga ni swala la Lema kutotumia njia sahihi.

Mimi nlimpongeza Lema alivyolishughulikia swala la Mwigamba kwenye kikao. Sasa yeye badala ya kutumia vikao anakuija mtandaoni kumchafua Zitto. Zitto angepuuzwa pia ni strategy. Usifikiri namtetea zitto. Kwa anayoyafanya lema na yericko wanakupaint chama na rangi mbaya, inayonuka vibaya
 
Najiuliza tu, hivi hiki chama chetu si kina mwenyekiti, na katibu? Haiingii akilini Zitto naibu katibu anashambuliwa na Lema na baadhi ya wanaoitwa makada wa chadema then mwenyekiti na katibu hawasemi lolote. Hivi angekuwa amesemwa John Mnyika, Josephine Mushumbusi ama Slaa si matamko yangetolewa? Mungekaa Kimya?

Binafsi nina matatizo na mwenendo wa Zitto, lakini katika hali ya kawaida uongozi wa chadema mmechemsha, badala ya kujibu hoja mnaleta risiti zinazomhusu Zitto sasa hizo risiti tuzifanyeje?

Ninachotaka kuona ni maamuzi yasiyo na double standard. Yaani hiki chama kimekuwa cha ajabu sana yani kwa mfano wapo vijana kama Yericko Nyerere anatoa matamko utafikiri chadema ni chama cha shangazi yake (naongea kama wanachama wanavyosema huku mitaani) na haoni madhara ya anayoyaandika humu.

Natoa saa 24 Mbowe na Dr Slaa najua mtasoma hii post, mchukue hatua na kuhakikisha Zitto hashambuliwi katika taratibu zisizo sahihi, laa sivyo nitaungana na wanachama wa kanda yangu tutatoa tamko latakalofuatiwa na kujitoa katika shughuli zote za kichama. Tunaweza!

sixgates,
Unatoa saa 24 kama nani?

Kama wewe ni mwanachama na ukaona tatizo ni kwanini usifuate taratibu tofauti na taratibu hizo hizo unazozilalamikia?

Unallamika kuwa kuna kiongozi ameshambuliwa lakini wewe unashambulia viongozi wa juu kwa kutumia njia hiyo hiyo

Ni lini uliona viongozi wa juu wa Chadema wameingilia mijadala humu kwenye mitandao?

Nakushauri ujifunze juu ya Itifaki.Kujaribu ku-imagine kwamba Mwenyekiti na katibu mkuu wanaweza kuja huku kumtetea kiongozi wa chini mwenye uwezo wa kujisemea na kujitetea ni gross insubordination

Tangu ianzishwe JF yamesemwa mengi lakini inapotokea hitilafu mara nyingi aliyeko rank ya chini na au msemaji wa chama mwenye mamlaka ya kusemea yote hufanya hivyo
 
Last edited by a moderator:
Binafsi nashangazwa sana na chama ambacho nilihisi kipo kwa maslahi yetu (Tz). Lakini sasa kimekua kwa maslahi ya Lema na Mbowe...........kweli baada ya masaa 24 makamanda wa kanda yangu pia tutatoa tamko. Nonsense.....stupid

Mnasubiri nini? Toeni hata dakika hii tena mkimaliza ondokeni wanafki wakubwa nyinyi mnatishia nyau
 
Yericko hajawahi kuwa objective, ndio maana anakuja na id ya john borne kuchafua viongozi wa chadema (zito) kisa hampendi
Mbona wanapotukanwa wengine kupitia wafuasi wa ZITTO waliovaa U-CCM husemi?
 
Nadhani sasa wamesha lewa madaraka kwani hawaambiliki wala hawasikilizi .Niweka Uzi hapa masaa machache yaliyopita wenye kichwa cha habari barua kwa Mheshimiwa Lema toka Uk baada ya kupata sapoti nyingi wameshaunyofoa.Nadhani Uzi wako pia utaondolewa

Nimeusoma mkuu nikauelewa sana. Unajua ukiwa na mawazo huru huogopi
 
Chadema kwa kutokomaa na kupeana madaraka..wanasambaratishwa kijingajinga sana.
 
usimusumbue kamanda kwa hoja zako za kimagamba gamba hapa, kwanza kuanzia leo zitto simtambui kama kimgozi wa chama changu, bali kama muuza sura,mtafuta ujiko, mropokaji na asiyejielewa. Huu upuuzi pelekeni mwandiga. Kama na wewe uko upande wa zitto na masalia kuanzia kesho wambieni jamb zenu wa lumumba tumewashitukia.
ujinga wa lema hauvumiliki.

Lema ni wakifundwa.
 
In short nimempigia simu Mnyika na kasema atahakikisha anacontrol situation, Zitto hapokei simu. Dr Slaa na Mbowe sijazoeana nao.


Duh inasikitisha sana, kama Mnyika atacontrol mambo baada ya kupokea simu yako na kumueleza kuwa mambo haya yanaichafua chama. Jee alikuwa anangoja nini waki wote huo????

wote hao kitu kimoja, hii ni roject fukuza zitto chadema , alafu tufanye uchaguzi ndani ya chama , kwani zitto is game spoiler for Mbowe na slaa team. Na sidhani kama atafanya kitu chochote.
 
Risiti hazijaletwa na viongozi wa chadema.... Zitto ni kiongozi asingezipitisha!

Mkuu mbona unajifanya blind can't yu see kuwa accusation zilizoletwa huku mtandaon ni nzito sana? Hayo ndio nayoyalalamikia kuwa viongozi wa chadema wangereact mapema kuepusha hii kadhia.
 
Yeriko na wenzake wanatumiwa na viongozi wengine wa chadema kumwangamiza zitto sijui kwa manufaa ya nani.

maskini mke wangu simiyu, kihelehele cha nini? Kesho ntakuja na basi la mbasa raha kukuletea matumizi usihangaike, tulia mama.
 
Cahadema walianza na shetani watamaliza na shetani dhambi ya kunyanyasa watu wengine wanayo tu na elementi za damu ya watu wanazo tu.

mwigamba alionewa na kuteswa kisa kaandika kwenye mitandao halafu leo wao wamepanga kumchafua zitto kwa makusudi halafu wanajifanya wema.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom