Mbowe katika Clouds FM, afafanua juu ya suala la Shibuda

Mkuu wangu hata kama wewe ni Chadema damu usipotoshe wote tumemsikia Mbowe alichosema.

Mbowe kasema anaomba radhi na kukiri kuwa Clouds ni Radio ya vyama vyote tofauti na alivyokuwa anavyofikilia hapo mwanzo.

Akaendelea kusema Clouds vyama vyote ni wateja wake CCM, Chadema, Cuf. Ebu tuambie wapi kaionya Clouds?
Ritz,nani hakufahamu?wewe huwa unasikia yale yakufurahishayo,yasiyokufurahisha huyasikii wala kuyaelewa
 
Wanabodi.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, leo kalitolea ufafanuzi wa kina suala la Mbunge wa Chadema John Shibuda, kutangaza nia yake ya kugombea urais kupitia Chadema.

Mbowe kasema John Shibuda, alichofanya ni sahihi na wala hakuna kosa wala tatizo lolote ndani ya Chadema wakati kasema hayo wakati akifanya mahojiano na kituo cha redio cha Clouds FM Jijini Dar es Salaam.

Mbowe aliendelea kusema alichofanya Shibuda ni haki yake ya kikatiba.

SOURCE: CLOUDS FM.

Tayari kuna thread ya hii habari na Mbowe akihojiana na clouds.Kwanini ulete mpya tena?
 
Nimeipenda sana hii kauli ya kamanda Mbowe
"Inshu ya Shibuda ni ndogo na haiwezi kuleta madhara kwenye chama maana haijagusa misingi ya uwepo wa chama" Mbowe.


yaani majibu ya mbowe yananifurahisha sana ..maana yanam diminish shibuda vibaya sana...yaani issue yake ni very scant....
 
Tayari kuna thread ya hii habari na Mbowe akihojiana na clouds.Kwanini ulete mpya tena?

Muache tu, na usifikiri alichokiandika hapo ndio ujumbe anaotaka kutuma, na kwa sababu namjua, namsubiri aanze vibweka vyake.
 
Ishu ya shibuda ni ndogo na ni kawada kwenye vyama vya siasa,kwani chama kina watu wenye malengo/mtazamo mmoja ila nji tofauti ya kufikia malengo =kamanda MBOWE

Hii nini? Yaani unaweza kuweka mguu mmoja kwenye gari, mwingine kwenye ndege, safarini kwenda Nairobi kutoka Dar, tutafika kweli? Njia tofauti tofauti zinatoka wapi? Kwani chadema ni ya mtu mmoja mmoja au ni taasisi? Kwanini kusiwe na njia moja inayojengwa na falsafa ya chama?
Ccm walipanda farasi wawili, tena waliokuwa na uelekeo tofauti, mwingine kaskazini na mwingne kusini, matokeo yake ndio haya, msamba hadi kifuani, imebaki shingo tu, nayo hiyoooo!
Aah! Siasa bwana, ukiwa muongo uwe na kumbukumbu, lakini za mwizi arubani pia!
MUNGU WETU ANAITA SASA!
 
Mbowe hasemi ukweli anaposema kuwa CHADEMA ndio "custodians" na initiators wa hoja ya Katiba, amesahau CUF ndio waliobuni hoja hiyo na ndio walioandika mpaka rasimu ya katiba yao miaka mingi sana kabla ya chadema hata kufikiria.

Mambo mengine jamani mwambieni huyu Mwenyekiti wa magwanda awe anauliza kabla hajakurupuka.

Ribosome usiwasahau NCCR mkuu!
 
WENJE anasemaje kuhusu SHIBUDA????? "Its not a minor issue hata Mbowe hajui afanyeje" tehe tehe tehe kimewang'ang'ania hakibanduki hicho....!
 
Mbowe anaomba CUF washariki mkutano wa Chadema Jangwani...sasa hapo nashindwa kumuelewa Mbowe CUF si CCM B sasa unawaomba wa nini?
M4C ni kwa ajili ya ukombozi wa Taifa la Tanzania, kila mtu anapaswa kushiriki, hata ccm wanashiriki ingawa ni chini ya kapeti.
Nukuu maneno ya Mbowe aliyosema ''Watu wanakosea wanapodhani tunapo address mabadiliko chanya tunataka kila mtu abelong to CHADEMA, lakini tunataka kila mtu awajibike pale alipo''.
 
Mkiti wa Chadema kakaribishwa Clouds leo na kupewa airtime zaidi ya nusu saa. Ameongelea mambo kadhaa ikiwemo kwamba kwa muda mrefu CloudsFM imekuwa ikipendelea CCM na kuandama Chadema.

Kwa ujumla pande zote mbili zimemaliza mazungumzo yao kwa ahadi ya kushirikiana huku mkurugenzi wa Clouds akiahidi kuwa CloudsFM itakuwa fair na yeye mwenyewe atahudhuria mkutano wa Chadema utakaofanyika Jangwani DSM tarehe 26/05/2012

Tafsiri yangu, Clouds wamegundua kuwa Chadema kwa sasa ndiyo iliyo na ushawishi na inakubalika kwa wananchi hasa vijana ambao ni walengwa wakuu wa CloudsFM. Pia wanatarajia kuwa na mahusiano na chama kinachotarajiwa kushika dola, pengine kwa maslahi ya kibiashara
 
Namsikia Mbowe anaongea Clouds, maneno mawili kingereza cha ujanja ujanja.

Wewe mbona una raise issue za kipuuzi sana? kiingereza wewe unakifahamu sana au? na pia kiingereza sio lugha yetu ni ya wageni na kujua kiingereza sio ufahari wala kujua mambo! wapo wataalam waliobobea wa urusi, ujeruman, japan, israel hawajui kiingereza! cha maana kama anaeleweka anachoeleza inatosha hata hao waingereza unawaabudu kama basi na ma genius walete hapa waambie waongee kisukuma au kipare si hawajui sasa utawacheka hawajui? uwezo wako mdogo sana wewe ni mzigo hapa JF!!
 
WENJE anasemaje kuhusu SHIBUDA????? "Its not a minor issue hata Mbowe hajui afanyeje" tehe tehe tehe kimewang'ang'ania hakibanduki hicho....!
Mling'ang'ania issue ya shibuda mkidhani italeta mvurugano ndani ya CDM, Chama makini kinajua namna ya ku handle mambo ya wapumbavu wanaotumwa na ccm wakitumia mbinu za kizamani ambazo kwa sasa hazifui dafu, MKOME!
 
Back
Top Bottom