Mbowe haondoki kwenye Uenyekiti mpaka tupate Katiba Mpya na Tume huru

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,410
74,048
Nakazia tu alichokisema mtu humu JF, kama Kitila na Zitto Kabwe wangelifanikwa kumng'oa Mbowe kwenye uenyekiti, CHADEMA lingekuwa Tawi la CCM. Rabbon

Kwa muktadha huo, Mbowe haondoki kwenye uenyekiti mpaka tupate katiba Mpya na Tume huru!

Take Note: Wenye uwezo CHADEMA ni wengi. Lissu, Heche, Lema, Msigwa and many others, lakini ngoja awepo awepo kukamilisha safari aliyoianzisha ya demokrasi at national level government.
Erythrocyte
 
Tafuteni katiba na tume huru kwenye chama chenuuu chadema ili uchaguzi uwe wa demokrasia ndani ya chama chenuu. Wewe mwenyekiti wa chama hana ukomoo? Jamaaniii.

Katiba ya wananchi itatafutwa na wananchi wenyeweee wasio na mlengo wa chama chochote
 
Hapana. Cha muhimu uchaguzi wa kumpata mwenyekiti ufanyike. Watu tofauti wagombee akiwemo na Mbowe mwenyewe. Mbowe akishinda kinyang'anyiro aendelee lkn akishindwa asepe.

Siyo suala lenye afya kwa demokrasia kuamini kuwa mtu fulani akiondoka ktk chama basi chama kitakufa.

Ni jukumu la chama kujenga mifumo imara ya kuachiana kijiti huku chama kikiendelea kuwa imara.

Kinyume na hapo tutajenga ufalme, udikteta na umilikaji wa chama pasipo kujua.
 
Hapana. Cha muhimu uchaguzi wa kumpata mwenyekiti ufanyike. Watu tofauti wagombee akiwemo na Mbowe mwenyewe. Mbowe akishinda kinyang'anyiro aendelee lkn akishindwa asepe...
Uchaguzi wa Chadema ni mfano bora wa kuigwa wa kidemokrasia
 
Nakazia tu alichokisema mtu humu JF, kama Kitila na Zitto Kabwe wangelifanikwa kumng'oa Mbowe kwenye uenyekiti, CHADEMA lingekuwa Tawi la CCM....
Mwalimu wa Siasa

JamiiForums77508547.jpg
JamiiForums1267461471_387x387.jpg
 
Tafuteni katiba na tume huru kwenye chama chenuuu chadema ili uchaguzi uwe wa demokrasia ndani ya chama chenuu. Wewe mwenyekiti wa chama hana ukomoo? Jamaaniii.

Katiba ya wananchi itatafutwa na wananchi wenyeweee wasio na mlengo wa chama chochote
Kila kitu lazima kiwe na kiongozi imara. Uoga wa watanzania, mi mi na wewe kuogopa risasi, kufungwa jela, kifo etc hatuwezi kutoboa bila kuwa na watu shupavu, wasio woga kama Mbowe..
 
Madikteta wote husema ngoja nikamilishe hiki. Ngoja ni kamilishe kile. Mwisho hutawala maisha. Mbowe alitamka kuwa mwaka 2023 anaachia kiti. Kama CDM ni wapinzani wa maana tunataka kuona hilo.
 
Chadema huwa mnachekesha kweli, mnataka katiba mpya halafu muda huo huo katiba ya chama mnaisigina, chadema ikishika dola rais wake atafia kwenye kiti, mbowe uenyekiti tu wa chama kakaa miaka 50 je akipewa nchi sasa?
 
Hiyo katiba tunaipata kwa kwenda kupitia nyuma ya ikulu?, Hapo hamna katiba mpya wote ni walewale danganya Toto.
 
Kwani zinakuwaga za siri?
Demokrasia ndani ya chaguzi za chadema bado sana. Kumbuka matukio yafiatayo:-
1. Zitto, Mwambe na Kitila kufukuzwa chamani kwa kujiandaa kupambana na mwenyekiti ktk chaguzi.

2. Kumpokea Lowasa na kumpa kijiti cha kugombea urais kupitia chadema huku waliokuwa wakivujja jasho wakituowa kama toilet paper.

3. Tunakumbuka namna vigogo wa chama wanavyochangia kuteua marafiki zao kugombea ubunge. Yaani kura za maoni huwa ni gelesha tu. Ilitokea 2015 ktk majimbo mengi ya Mbeya, Kilimanjaro, Arusha na Mbeya
 
Japo Mbowe bado anaonekana ana nguvu, mvuto, na kuaminiwa na wengi, hasa baada ya kufuta zile kelele za amelamba asali kwa kumtandika Samia na kitu kizito kichwani mpaka CCM wote wakaanza kulia...

Lakini kwa upande mwingine naona akiwepo mwenyekiti mpya aongoze Chadema mambo hayataharibika pia, anaweza kuja na ari mpya itakayokisukuma chama kusonga mbele zaidi, option zote mbili kwangu naziona sawa tu.
 
Demokrasia ndani ya chaguzi za chadema bado sana. Kumbuka matukio yafiatayo:-
1. Zitto, Mwambe na Kitila kufukuzwa chamani kwa kujiandaa kupambana na mwenyekiti ktk chaguzi.

2. Kumpokea Lowasa na kumpa kijiti cha kugombea urais kupitia chadema huku waliokuwa wakivujja jasho wakituowa kama toilet paper.

3. Tunakumbuka namna vigogo wa chama wanavyochangia kuteua marafiki zao kugombea ubunge. Yaani kura za maoni huwa ni gelesha tu. Ilitokea 2015 ktk majimbo mengi ya Mbeya, Kilimanjaro, Arusha na Mbeya
Nikujibu;

1. Zitto, Mwambe na Kitila kufukuzwa Chadema ilikuwa sahihi, wale wahuni waliandaa mapinduzi, hawakuonewa.

2. Lowassa kupokelewa Chadema ilikuwa ni haki yake kikatiba, na kupewa ridhaa ya kugombea nafasi ya Urais ulikuwa uamuzi wa KK, ndio maana siku akikaribishwa chamani, wajumbe karibia wote wa KK walikuwepo eneo husika.

3. Tuambie, hao marafiki wa vigogo wanateuliwa kwa njia gani? usitake kupotosha ionekane kuna udikteta ambapo wanaoteuliwa majimboni hupatikana bila kupigiwa kura, kama hupatikana kwa kupigiwa kura na kushinda, sioni mantiki ya hoja yako.
 
Back
Top Bottom