Maigizo majukwaani, kamwe hayawezi kuwa mbadala wa KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,109
22,562
Salaam,Shalom.

Matatizo ya Wananchi ni ya kimfumo, hivyo chama Cha MAPINDUZI CCM kisipoteze muda kujaribu kuhadaa wananchi kuwa kinaweza kutatua kero za wananchi katika ziara majukwaani kana kwamba hakuna watumishi maofisini.

Suluhu ya matatizo ya Wananchi ni kuhakikisha tunapata Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote.

Andrew Nyerere: "Nitamsifia vipi kiongozi kuwa anaupiga mwingi Kwa kufanikisha ujenzi wa barabara ya lami, wakati Mimi Mwananchi Sina hata baiskeli ya kupita juu ya barabara hiyo?"

1. Karipio la Katibu Mwenezi kuwa anaweza kumpiga makofi waziri wa viwanda, kamwe haliwezi kupunguza ugumu wa maisha ya wananchi wa kawaida Walio wengi.

2. Kumpa bima mtoto mmoja aliyelawitiwa, wakati huo huo Serikali ya CCM ikiondoa bima Kwa watoto chini ya miaka 5, iliyokuwa Bure Nchi nzima, ni upofu wa fikra na Roho mbaya.

3. Kumpa Mzee mmoja mstaafu laki tatu jukwaani huku mfumo ukifumbia macho dhulma ya wafanyakazi walioajiriwa sekta binafsi ni sawa na kufumba macho na kutembea barabara ya mwendokasi.

Tutakutana kwenye Sanduku la kura baada ya kupatikana Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi,itakayopatikana Kwa maandamano barabarani na mikutanoni Viwanjani.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni.🙏
 
Back
Top Bottom