Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ni baada ya 2025

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Najua hamtaniamini lakini kwa jinsi Mambo yanavyokwenda NAWAAPIA Suala la Kupata KATIBA MPYA na TUME HURU ya UCHAGUZI litaanza Baada ya UCHAGUZI MKUU 2025 .

Wenye AKILI KUBWA tulilijua Mapema kutokana na Danadana za Viongozi ikiwa ni pamoja na kutaka Mchakato uanze UPYA wakati Tayari TUME ya JAJI WARIOBA ilishafanya KAZI KUBWA ya Kukusanya MAONI na MAPENDEKEZO ya MAMILIONI ya WANANCHI na pia FEDHA nyingi ilikwisha Tumika na kuliwa na WAJUMBE wa Bunge la Katiba bila kutupatia KATIBA MPYA.

Najiuliza kwanini SERIKALI haitaki kuendelea lilipoishia BUNGE la KATIBA?

Najiuliza kwanini SERIKALI inataka kuanza UPYA?

Jibu ni KUCHELEWESHA UPATIKANAJI wa KATIBA MPYA na TUME HURU ya UCHAGUZI na Dalili zake zinaonekana.

WATAWALA walianza kuunda VIKOSI KAZI na kutoa Mapendekezo ambayo mpaka leo SIJUI YAMEFIKIA WAPI.

Mara tukasikia Waziri Wa Sheria anatangaza kuanza MCHAKATO wa KATIBA MPYA nao umekuwa KIMYA huku Muda unakimbia.

Suala la kuendelea KUTEUA Wajumbe Mbalimbali wa TUME ya Uchaguzi wakati Hata maandalizi ya Kuunda UPYA TUME HURU ya UCHAGUZI ni Ushahidi tosha kuwa Watawala bado wanataka TUME iliyopo iendelee kufanya kazi na Madhara yake wote tunajua ikiwemo ya WABUNGE FAKE 19 ,UCHAGUZI wa SERIKALI za MITAA 2019 na UCHAGUZI MKUU 2020 Yaliyotokea Yatatokea tena 2025.

Mnazidi kuwakumbusha WATANZANIA Utawala uliokataa KATIBA MPYA 2015 ndio huu huu ULIOPO na MSITARAJIE KATIBA MPYA Au TUME HURU ya UCHAGUZI kabla ya 2025 vyote mtavipata Baada ya Watawala kuwa MADARAKANI 2025.

Mtasubiri SANA.
 
Nami naamini kabisa kuwa Rais Samia hana dhamira ya kutaka katiba mpya na tume huru ya uchaguzi vipatikane. Bila ya kuwepo nguvu ya kumlazimisha, hata hiyo baada ya 2025, hakuna chochote kitakachofanyika kuhusiana na kupatikana kwa katiba mpya.

Lini katiba mpya na tume huru ya uchaguzi vipatikane, itategemea maamuzi ya wananchi, siyo maamuzi ya Rais.

Hizi danadana, dhamira yake siyo tu kuchelewesha bali ni kuhakikisha katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, havipatikani. Zile hadithi za mara nimechagua wajumbe, sijui vikao vya vyama vya siasa, lengo lake ilikuwa ni kuua vuguvugu la wananchi kulazimisha katiba mpya kupatikana. Wanataka kukifanyika jitihada za wananchi kulazimisha, waseme kuwa hawa wanaleta vurugu, mbona mchakato umekwishaanza. Lakini ukweli ni kwamba hakuna dhamira yoyote. Kinachofanyika ni hadaa tupu.
 
Kwa bunge hili ni vizuri katiba mpya iwe baada ya uchaguzi, tuwaondowe kwanza hawa wabunge wa Magufuli na spika wa kupachikwa halafu tuingize wabunge wa kuchaguliwa na wananchi ndio kutakuwa na bunge la katiba litakalowakilisha wananchi siyo hawa wahuni aliowaweka Magufuli rubber stamp ya DP.
 
Viongozi wa CCM wanatambua fika kuwa salama yao ni kupitia kubebwa na vyombo vya dola. Wanatambua fika kuwa uchaguzi ukiwa huru na pia wa haki, basi ni lazima watalazimika kutundika daluga.

Hawana nia njema wala dhamira ya dhati kuhusu kuridhia suala la katiba mpya wala muundo mpya wa tume ya uchaguzi. Wamezoea vya kunyonga, vya kuchinja wataviwezea wapi!
 
Katiba na tume ya uchaguzi sindiyo ilimpa nguvu ya kuwaweka hao unaoita wabunge wa JPM?Huoni uwezekano ni mkubwa wa wote kushinda bila kupingwa au kutangazwa tu hatakama utapiga kura?
Hii nchi ina watu wa ajabu sana.
 
Najua hamtaniamini lakini kwa jinsi Mambo yanavyokwenda NAWAAPIA Suala la Kupata KATIBA MPYA na TUME HURU ya UCHAGUZI litaanza Baada ya UCHAGUZI MKUU 2025 .

Wenye AKILI KUBWA tulilijua Mapema kutokana na Danadana za Viongozi ikiwa ni pamoja na kutaka Mchakato uanze UPYA wakati Tayari TUME ya JAJI WARIOBA ilishafanya KAZI KUBWA ya Kukusanya MAONI na MAPENDEKEZO ya MAMILIONI ya WANANCHI na pia FEDHA nyingi ilikwisha Tumika na kuliwa na WAJUMBE wa Bunge la Katiba bila kutupatia KATIBA MPYA.

Najiuliza kwanini SERIKALI haitaki kuendelea lilipoishia BUNGE la KATIBA?

Najiuliza kwanini SERIKALI inataka kuanza UPYA?

Jibu ni KUCHELEWESHA UPATIKANAJI wa KATIBA MPYA na TUME HURU ya UCHAGUZI na Dalili zake zinaonekana.

WATAWALA walianza kuunda VIKOSI KAZI na kutoa Mapendekezo ambayo mpaka leo SIJUI YAMEFIKIA WAPI.

Mara tukasikia Waziri Wa Sheria anatangaza kuanza MCHAKATO wa KATIBA MPYA nao umekuwa KIMYA huku Muda unakimbia.

Suala la kuendelea KUTEUA Wajumbe Mbalimbali wa TUME ya Uchaguzi wakati Hata maandalizi ya Kuunda UPYA TUME HURU ya UCHAGUZI ni Ushahidi tosha kuwa Watawala bado wanataka TUME iliyopo iendelee kufanya kazi na Madhara yake wote tunajua ikiwemo ya WABUNGE FAKE 19 ,UCHAGUZI wa SERIKALI za MITAA 2019 na UCHAGUZI MKUU 2020 Yaliyotokea Yatatokea tena 2025.

Mnazidi kuwakumbusha WATANZANIA Utawala uliokataa KATIBA MPYA 2015 ndio huu huu ULIOPO na MSITARAJIE KATIBA MPYA Au TUME HURU ya UCHAGUZI kabla ya 2025 vyote mtavipata Baada ya Watawala kuwa MADARAKANI 2025.

Mtasubiri SANA.
Wasema ukweli kabisa. Kielelezo kingine cha kuashiria kukosekana kwa katiba mpya ni teuzi za wajumbe wa tume ya uchaguzi alioufanya jana. Kama mchakato ungekuweko angeendelea na waliokuwepo mpaka waje wapya.
 
Back
Top Bottom