Mbowe awekewa pingamizi CHADEMA

Mbowe awekewa pingamizi CHADEMA

Small minds discuss people, average minds discuss events, and great minds discuss ideas! Kansa Mabrouk has a very small mind, SHAME!!!!!
 
Hakika Mbowe ni Jabari katika siasa, wamwache atufikishe tunakotaka.
 
MACCM yanaweweseka nyuma ya mgongo wa Mbaruku,

Hivi wewe Mbaruku nani kakuroga ww siku hizi? Hujui unatuaibisha wanaMboka wenzako?
Acha ujinga huo mara moja unatufanya tuone aibu kwani wanaMboka hatuna ujinga kama huo.
 
Hueleweki. Umeshakunywa viroba vingapi?

Sasa ndugu yangu usipoelewa hapo sijui nikusadieje. OK, Hebu nenda chooni kwanza hafu kasome tena ulipopaquote. Kaaaazi kelikweli! ujue compyuta nayo inanizingua
 
bado jaji mutungi hajaja ns rungu lake

nyie wapambe ndio nuksi

Huyo ni mlevi wa madaraka katiba kaiweka kapuni ili aendeleze sacos yake na vijana wa bavicha wamepewa kidogo ili wampigie debe kweli akili ni nywele.

Naona mnajitekenya huku mkicheka wenyewe ebu naomba mnijibu maswali yangu yafuatayo
1. Katika kipengere uchaguzi ngazi ya Mwenyekiti Taifa ndani ya Katiba ya CCM kimeandikwa kuwa nafasi hiyo haitagombewa na mtu zaidi ya Mmoja? maana tangu chama kimeanza nafasi hiyo haijawahi kushindaniwa na mgombea zaidi ya mmoja na yule ambae uleta chokochoko za kutaka kugombea uzimwa na kupewa onyo kali.

2. Vipi kuhusu katiba za CUF, UDP na TLP zinasemaje kuhusu hicho mnachokishabikia CHADEMA? kwani tumeshuhudia vyama vya UDP na TLP wenyeviti ni Cheyo na Mlema, Makatibu wakuu ni Cheyo na Mlema, Makatibu wenezi ni Cheyo na Mlema, makamu wenyeviti ni Cheyo na Mlema pia ni hao hao ndio wabunge wanaowakilisha vyama vyao. Je huyo Msajili wa vyama hajayaona mapungufu katika vyama hivyo ambayo ni makubwa kuliko hayo anayojifanya kuyakomalia huku CHADEMA.
 
Huyo Mbaruku Kichwa na Tumbo vyote vipo CCM/ACT hapo CHADEMA amebakiza hivyo vimiguu vyake tu anachokifanya ni kujihangaisha bure kwani mambo yake yote yanajulikana watu wanamstahi na kumuangalia tu kwani hawezi kupata uwenyekiti na pia hata kuwa mwanachama wa CHADEMA siku zake zinahesabika.
 
Wewe acha umbulula wako. I said majina yako kwenye database na Mbowe ha-manage database. Sasa hayo mapenzi na Mbowe yako wapi?

Usihangaike na mashabiki wa Buku 7. Huyo Mbarouk hajui kuwa CDM wanajua the motive behind his petition? Mbinu chafu za Wasira na Mwigulu kupitia vipandikizi kama Mbarouk hata CCM wenyewe wanajua hazita zaa matunda.
 
Kwa nini mnaituhumu CCM wakati pingamizi limewekwa na mgombea wa CDM?

Kama hujui ni kwa nini,ni vyema ukalala kidogo na kumbukumbu zitakujilia tu na kuelewa ni kwa nini!!

Ukiona maumivu yamezidi na kumbukumbu haikurudii, rudi hapa utuulize,hatuna hiyana tutakusaidia ili na wewe uingie kwenye mapambano kupambana na hili duduwasha hatari linaloitwa CCM!!.

Kwa heri kwa sasa.
 
demokrasia lazima iwe na ukomo, lakini kwa siasa za Tanzania hawachelewi kukuita msalliti, umetumwa na ccm, wewe uko upnde wa fulani, jamani ifike hatua na mbowe ajichunguze upya, ni kweli amekifanyia chama mambo makubwa sana lakini tunapokuja kwenye swala la demokrasia lazima kuwe ukomo wa uongozi, pili lazima aruhusu mawazo mapya na hoja kinzani, na siyo anayejitokeza kumupinga anaitwa msaliti jamani demokrasia ina ukomo na pia demokrasia lazima kuwe na hoja kinzani kwa ajiiri ya kujenga.
 
jamani hivi kosa la mbarouk liko wapi, yeye kachukua fomu ya kugombea uenyekiti, jamani acheni demokrasia ifanye kazi yake then wapiga kura wataamua, hivi mbowe amekuwa nabii mpaka asipate mpinzani, na ndiyo maana wakaita uchaguzi, pili hata huyu jamaa kija na tuhuma juu ya mbowe hiyo ni lobbing lakini wapiga kura watachuja
 
"Mbowe alibadilisha majina ya Chiku Abwao na Susan Kiwanga huku akiwapachika Susan Lyimo na Lucy Uwenya. Baadaye Mbowe alikiri kosa na kuomba msamaha katika kikao cha Kamati Kuu,”alisema.
Alisema hayo yote yanadhihirisha pasipo shaka kwamba mwenyekiti huyo amekosa uaminifu hivyo anapaswa kunyang’anywa nafasi hiyo ya uenyekiti."

Alisema baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 chama kilipata nafasi tano za kuteua nafasi wabunge wa viti maalumu kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano, ambapo Kamati Kuu kilipitisha majina ya Suzan Kiwanga, Chiku Abwao, Halima Mdee, Mhonga Ruhanywa na Grace Kiwelu lakini Mbowe alibadilisha majina hayo.


source; magazetini leo.

My take; Je ni halali kutumia madaraka yako vibaya kuchakachua haki za wengine na kuweka ndugu zako?

JE CHIKU ABWAO ni MBUNGE WA JIMBO GANI ? NA JE UTARARATIBU UKOJE ? ' UKIVUTA SIGARA MPAKA KWENYE KISHUNGI UTAKUWA UMEVUTA TUMBAKU NA ILE RANGI YA MAANDISHI ' UMEELEWA ?
 
Huwa nikimuona mbowe namdhatau sana hasa mbele ya zitto jamfikii kwa lolote japo kampita umri tu.

pathetic....
hata andika yako ni shida, lakini sio kosa lako ni elimu uchwara ulio ipata, kajifunze kwanza kuandika.
 
Bavicha badala ya kumsupport Mbasrouk, mmekazania kulaumu CCM. Hivi Mbourouk ni CCM au kila anayempinga Mbowe ni CCM. Hii saccos inatupeleka wapi, haina hata mwongozo kila mtu ni kambale. Nadhani hii ni njaa, maana njaa mbaya!!!! Sasa hivi Mbarouk atafukuzwa cdm na ataambiwa msaliti na bavicha watashangilia kwa shilingi tatu tatu maana njaa mbaya.
 
Mnamo mwaka 2010 #chadema waliwatangazia wananchi kuwa hawamtambui rais dr jakaya kikwete, swali: ni lini chadema wametangaza au walitangaza kuwa wanamtambua rais??? Swali la pili; chadema mwaka 2010 walitangaza kuwa hawatachukua magari ya kifahari, je ni lini chadema walitangaza kwa wananchi kuwa wamechukua hayo magari? Na pia chadema walitangaza mwaka 2010 kuwa hatachukua posho za bungeni, swali je ni lini chadema walitutangazia wananchi kuwa wamechukua hizo posho????

#tutaheshimiana
 
Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo, CHADEMA mh Freeman Mbowe, amewekewa pingamizi kugombea nafasi ya uenyekiti Taifa kutokana na madai kuwa, amekiuka katiba ya chama hicho pamoja na maagizo ya msajili wa vyama nchini.

Freeman-Mbowe.jpg

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe


MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amewekewa pingamizi la kutogombea nafasi hiyo kwa awamu ya tatu kwa madai ya kukiuka katiba ya chama hicho na maagizo ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.

Pingamizi hilo limewekwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Tabora, Kansa Mbarouk, ambaye pia ni mgombea wa nafasi hiyo.

Barua ya Mbarouk yenye kumbukumbu namba Mbarouk/UCH/14 kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chadema na Msajili wa Vyama vya Siasa, iliyoandikwa Septemba tano, inasema kufikia Septemba 14 siku ya uchaguzi mkuu wa chama hicho, Mbowe atakuwa ametumikia vipindi viwili katika nafasi ya mwenyekiti wa taifa.

Barua ya Mbarouk inasema kwa mujibu wa katiba ya Chadema, kama ilivyothibitishwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, hakuna mwanachama anayeruhusiwa kuchaguliwa kuongoza kwa zaidi ya vipindi viwili katika cheo kimoja kwa ngazi moja.

“Msajili wa Vyama alikuwa ametoa maelekezo kwamba chama kiitishe Baraza Kuu na Mkutano Mkuu Maalumu kwa lengo la kubadilisha kipengele kinachoweka ukomo wa uongozi kama litaona kuna haja hiyo kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu. Hata hivyo hadi naandika barua hii hakuna dalili zozote kwamba mkutano mkuu maalumu utaitishwa na maandalizi ya uchaguzi yanaendelea bila kujali agizo la msajili wa vyama,”alisema Mbarouk katika barua hiyo.

Alisema katika kipindi chake cha uongozi Mbowe alisimamia vikao vya chama vilivyofanya maamuzi ya kuvunja katiba waziwazi.

“Mfano Novemba 2013, Mbowe alisimamia kikao cha kamati kuu kilichomvua nafasi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama, Zitto Kabwe na wenzake bila kuzingatia mamlaka ya kikao hicho. Kwa mujibu wa Sura ya Sita ibara ya 6.3.6(b) ya katiba ya Chadema toleo la mwaka 2006 ‘kiongozi aliyeteuliwa na vikao vya uongozi ataweza kusimamishwa au kuachishwa uongozi na kikao kilichomteua’,”alisema.

Alisema baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 chama kilipata nafasi tano za kuteua nafasi wabunge wa viti maalumu kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano, ambapo Kamati Kuu kilipitisha majina ya Suzan Kiwanga, Chiku Abwao, Halima Mdee, Mhonga Ruhanywa na Grace Kiwelu lakini Mbowe alibadilisha majina hayo.

“Mbowe alibadilisha majina ya Chiku Abwao na Susan Kiwanga huku akiwapachika Susan Lyimo na Lucy Uwenya. Baadaye Mbowe alikiri kosa na kuomba msamaha katika kikao cha Kamati Kuu,”alisema.

Alisema hayo yote yanadhihirisha pasipo shaka kwamba mwenyekiti huyo amekosa uaminifu hivyo anapaswa kunyang’anywa nafasi hiyo ya uenyekiti.

“Ninatambua kuwa kwa mujibu wa katiba ya chama Sura ya Saba ibara ya 7.3.1, uchaguzi ngazi ya taifa unapaswa kusimamiwa na wazee wastaafu wa chama hata hivyo hadi naandika barua hii sina taarifa kuhusu kuteuliwa kwa kamati hii. Hivyo basi nimelazimika kuandika barua yangu ya pingamizi kwako nikiamini kwamba utaifikisha katika chombo husika kinachoshughulikia uchaguzi,”alisema Mbarouka.

Alipotafutwa na gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani kuzungumzia barua hiyo, Mbarouk alisema ni kweli ameandika barua hiyo na kwamba aliikabidhi juzi Septemba 6 katika ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama.

“Ni kweli nimeiandika mimi na nilikabidhi jana (juzi) katika ofisi ya katibu mkuu wa chama,”alisema Mbarouk.

Kwa upande wake Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alipoulizwa na gazeti hili endapo ni kweli barua hiyo imewafikia, alimwambia mwandishi wa habari hizi kuwa atampigia baadaye.

Hata hivyo baada ya Makene kumpigia simu mwandishi alimtaka amtajie lengo la Mbarouk kumpinga Mbowe, baada ya mwandishi kufanya hivyo aliahidi angepiga tena simu, lakini hadi gazeti linakwenda mtamboni hakupiga simu.



CHANZO: Mtanzania
Big up. Tokomeza ukabila
 
Back
Top Bottom