Wanajamvi!
Kumekuwa na tabia ya CCM kila wanapoona wanabanwa na vyama vingine vya siasa, wao wanakuja na mbinu ya kupandikiza mamluki. Hali hii imeendelea miaka nenda rudi sasa!
Kipindi hiki wamegonga mwamba kwa kukutana na mwamba wa kaskazini Mh. Mbowe asiyekuwa na bei katika ununuliwaji wa viongozi wa vyama vya siasa unaofanywa na CCM.
Baada ya CCM katika kuona kuwa plan A ya kutaka kibalaka wao Zitto awe mwenyekiti wa CHADEMA kugonga mwamba wakaja na plan B ya kuunda chama cha siasa cha ACT Tanzania huku kikiwa na viongozi bila ya waongozwa. Wengi wa viongozi hao ni wasaliti waliofukuzwa CHADEMA.
Plan B nayo imeonekana kushindwa, ili kutimiza kauli ya Wassira kuwa CHADEMA haifiki 2014 wamekuja na plan C ya kumpachika Kansa Mbaruku (Mzimu wa Zitto) kwenye kinyanganyiro cha kugombea nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA Taifa. (hapa ndipo ninapojikita katika mada hii)
Siku chache kabla ya Kansa Mbaruku kutangaza kuchkua fomu ya kuomba uenyekiti wa CHADEMA Taifa akaunti yake ilikuwa Dormant lakini siku tatu baadae akaunti hiyo ilionekana kuwa na shilingi milioni tatu (3,000,000/=) huku wachambuzi wakijiuliza amezitoa wapi ili hali Mbaruku hana kazi ya kumuingizia kipato na anaishi kwa kulishwa na mkewe ambaye mfanyakazi wa CCM ofisi ya mkoa.
Katika kuonesha na kutekeleza masharti ya mdhamini wake (CCM) Mbaruku alikwenda kwenye kituo cha redio kinachomilikiwa na Msomali wa CCM Aden Rage kilichpo Tabora na kuanza kuporomosha matusi na vijembe dhidi ya CHADEMA na Viongozi wake. Pia alitangaza kujiuzulu nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA ngazi ya mkoa.
Moja ya sababu alizozisema kuwa zimemchosha na anataka azidhibiti pindi atakapo kuwa mwenyekiti wa Taifa ni kuondoa udini, kuwekana kidungu na kiongozi kukaa madarakani kwa muda mrefu bila ya kuleta mafaniko katika chama.
Kansa Mbaruku (mzimu wa Zitto) kama alivyotambulishwa na baadhi ya magazeti ya tare 31/08/2014 amekuwa ni kikwazo cha kuingia kwa wanachama wengine kujiunga na chama. Huyu huyu Mbaruku alimkaimisha ukatibu ndugu yake Athuman Balozi na kumpa umwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) ndugu Halima Katundu pia kumpa Uenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA) ndugu yake Hussein Kundecha na pia kumuweka ndugu yake mwingine kuwa mpiga mashine (PS) wa ofisi ya mkoa ndugu Reheme Ulaya. Ambao wote wametangulia ACT kwa sasa na yeye atafuata baada ya mbinu zake chafu kushindikana.
Katika kuzamilia kukamilisha plan C, Kansa Mbaruku alikuja na pingamizi la kutaka Mh. Mbowe asigombee uenyekiti kwa lengo kutimiza matakwa ya mdhamini wake (CCM). Jana magazeti ya UHURU, JAMBO LEO na MTANZANIA ambayo ni mali ya CCM na vigogo wake yaliandika kuwa MBOWE awekewa pingamizi. Leo tena katika kuashiria kuwa wasaliti na CCM jumlisha na MCHEPUKO wake wameonekana kushindwa katika hatua yao baada ya mapitio ya magazeti kutangaza kuwa pingamizi lao limetupiliwa mbali hivyo kumfanya Mh. Mbowe kuwa mgombea halali wa uenyekiti ndani ya CHADEMA.
Nimefuatilia ili kujua katika mfumo wanaoufuata wanachama wa CHADEMA hivi sasa wa CHADEMA NI MSINGI, huyu Kansa Mbaruku anatokea Msingi gani, Tawi gani na ni Kata gani. Nilichoambulia ni kuwa Kansa Mbaruku anatokea kata ya Ipuli na anakaa kwenye nyumba zilizoibwa na wanaCCM zilizopo jirani na Bohari ya Madawa au Kituo cha Gari moshi (Station) zinazoitwa URBAN QUARTER.
Kwa sasa Kansa Mbaruku yupo Dar es Salaam tokea siku aliporudisha fomu ya kugombea nafasi ya uenyekiti CHADEMA ngazi ya Taifa huku akiwa na wahuni wabeba mizigo wa standi ya mabasi ya mikoani almaarufu UBUNGO. Ambapo wahuni hao waliishia getini bila ya kuingia ndani ya ofisi ya CHADEMA makao makuu.
Mwisho itoshe kusema kuwa KANSA MBARUKU ndiye mtunza vifaa vya uenezi (kadi, bendera na vipeperushi) vya ACT - Tanzania kwa mkoa wa Tabora.
Tusubiri plan D! inayosukwa na vijana wa CCM wakiongozwa na Msalani na Vijana wa ACT wenye ofisi mitandaoni wakiongozwa na Mwl. Kaijage