Mbowe awekewa pingamizi CHADEMA

Mbowe awekewa pingamizi CHADEMA

KWA NINI CHADEMA TU? kwa mfano baba wa taifa alikuwa mwekiti awamu ngapi ? mbona sisi tunaoshabikia hatukuhoji ? pro. Lipumba ana awamu ngapi .mbona hatuhoji? cheo, mrema? why CDM ,why mbowe? Ninachokiona baadhi yetu tunaona cdm inapaa. hivyo tunaomba siku moja kiharibikiwe. lakini tukumbuke ni mungu tu ndiye anaweza eidha kuipaisha cdm au kuishuka lakini siyo midomo ya watu. tutatumia nguvu kubwa sana, pesa na wasaliti kama siyo mpango wa mungu watu wataaibika. watatumika tu lakini hawatafaulu.CDM FOREVER.
Kwa nini ruzuku ilikwe na mtu mmoja miaka yote?
 
KWA NINI CHADEMA TU? kwa mfano baba wa taifa alikuwa mwekiti awamu ngapi ? mbona sisi tunaoshabikia hatukuhoji ? pro. Lipumba ana awamu ngapi .mbona hatuhoji? cheo, mrema? why CDM ,why mbowe? Ninachokiona baadhi yetu tunaona cdm inapaa. hivyo tunaomba siku moja kiharibikiwe. lakini tukumbuke ni mungu tu ndiye anaweza eidha kuipaisha cdm au kuishuka lakini siyo midomo ya watu. tutatumia nguvu kubwa sana, pesa na wasaliti kama siyo mpango wa mungu watu wataaibika. watatumika tu lakini hawatafaulu.CDM FOREVER.

Chadema wakikamilisha uchaguzi wao na Mbowe kuwa mwenyekiti kwa awamu nyingine tena ccm itasambaratika!
 
Kwa nini mnaituhumu CCM wakati pingamizi limewekwa na mgombea wa CDM?

Hawana njia nyingine ya kufichia maovu na udhaifu wao zaidi ya kujifunika koti la ccm hivo usishangae wanayoyafanya sie tunawaelewa.

Unaweza kuwadanganya baadhi ya watu wakati wote,lakini huwezi kuwadanganya watu wote wakati wote.
 
Tumuache ahangaike na pingamizi hilo,labda na yeye atapata kaumaarufu kidogo.lakini atambue kuwa wana chadema bado tunamuhitaji sana mbowe kwa wakati huu,ambapo mabadiliko yana hitaji kiongozi jcli kama mbowe,bila hivyo tutakuwa salama,tutauzwa mchana kweupe.
 
Ndoo maana tunashindwaa sanaa siasa za upinzani eti wanasemaa kwa kipindi hichii mbowee ana mbadalaa jaman huu c ujingaa inaana chadema nzima akuna mtuu kama mbowe au mwenye uwezo zaidi ya mbowe ebuu tubadilike na tuachee urohoo wa madaraka wanginee nao wapewee fursaa sio kila cku mbowe kwa mfano mbowee akifaa leo chadema ndoo inakufaa?
 
viongozi wa Afrika ugonjwa wao mmoja tu kuogopa kung'oka madarakani

Yaah usemayo ndo ukwel wenyewe. Tamaa na Uroho wa madaraka ni sheeedaaah sana kwa waafrika. Nafikiri hawa viongozi ndo kipimo cha akili za wananchi wao.
 
"Mbowe alibadilisha majina ya Chiku Abwao na Susan Kiwanga huku akiwapachika Susan Lyimo na Lucy Uwenya. Baadaye Mbowe alikiri kosa na kuomba msamaha katika kikao cha Kamati Kuu,"alisema.
Alisema hayo yote yanadhihirisha pasipo shaka kwamba mwenyekiti huyo amekosa uaminifu hivyo anapaswa kunyang'anywa nafasi hiyo ya uenyekiti."

Alisema baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 chama kilipata nafasi tano za kuteua nafasi wabunge wa viti maalumu kuingia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano, ambapo Kamati Kuu kilipitisha majina ya Suzan Kiwanga, Chiku Abwao, Halima Mdee, Mhonga Ruhanywa na Grace Kiwelu lakini Mbowe alibadilisha majina hayo.


source; magazetini leo.

My take; Je ni halali kutumia madaraka yako vibaya kuchakachua haki za wengine na kuweka ndugu zako?
 
Chadema mlikuwa mnahangaika na Zitto sasa hivi limeingia jembe lingine Kansas Mbaruku..teh teh
 
Ingekuwa China mtu kama Mbowe adhabu yake ni kunyongwa.
 
Ndoo maana tunashindwaa sanaa siasa za upinzani eti wanasemaa kwa kipindi hichii mbowee ana mbadalaa jaman huu c ujingaa inaana chadema nzima akuna mtuu kama mbowe au mwenye uwezo zaidi ya mbowe ebuu tubadilike na tuachee urohoo wa madaraka wanginee nao wapewee fursaa sio kila cku mbowe kwa mfano mbowee akifaa leo chadema ndoo inakufaa?

Wapiga kura wanamhitaji Mbowe sasa ninyi nini kinawauma? Achana na Chadema wachague mwenyekiti wao kama wanaridhika naye.
 
Hawana njia nyingine ya kufichia maovu na udhaifu wao zaidi ya kujifunika koti la ccm hivo usishangae wanayoyafanya sie tunawaelewa.

Unaweza kuwadanganya baadhi ya watu wakati wote,lakini huwezi kuwadanganya watu wote wakati wote.

Yaani wewe ndio huelewi kitu, Hakuna njia nyingine zaidi ya uwatumia wasaliti.Hivi ni nani asiyejua kua Mbarouk ana kadi ya ACT?Kazi ya hiyo kadi ni nini?Hizo m.3 alizopewa zilikua na kazi gain?
 
Atakuwa ni mtu mjinga tu ndio anaweza kuto kujua nini kinafuata nyuma baada ya Kansa Mbarouk kupata air time ya hizi propaganda kwenye Mtanzania, Jambo leo, Uhuru na Habari leo.

Kwa nini?

1. Kansa Mbarouk anaye jitokeza na sababu za ukomo wa madaraka yeye mwenyewe anajua kwenye katiba ya chama kuna kipengele (6.3.2 (c), kinasema "kiongozi aliye maliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi"

Kupitia kipengele hichohicho mtu huyohuyo Kansa Mbarouk amekuwa mwenyekiti wa mkoa wa Tabora kwa vipindi zaidi ya viwili. Amekuwa mwenyekiti kwa vipindi vitatu mfululizo yaani amekuwa mwenyekiti wa Tabora kwa miaka 15. Leo hii aliye kuwa mwenyekiti wa mkoa, aliye kuwa miongoni mwa wajumbe wa Baraza kuu waliopitisha katiba yenye kipengele hicho anaweka pingamizi! Ana tofauti gani na Samson Mwigamba aliyetumia hoja hizo hizo huku naye akiwa miongoni mwa waliopitisha kifungu hicho?!

2. Kama yeye katiba ilimruhusu kugombea kwa vipindi vitatu mfululilo nini leo kinamkuna kuipinga katiba hiyo hiyo ambayo yeye ilimuwezesha kugombea vipindi vitatu na akawa mwenyekiti wa mkoa wa Tabora?!

Kama unawaza mambo kwa 3D na kuhusisha milango 6 ya fahamu utajua kuna mazingira yanaandaliwa. Mazingira yapi?

1. Kansa Mbarouk na Athuman Balozi yule aliye ongoza maandamano fake kwenda kwa msajili na CAG akishirikiana na Yona ni mtu na mjomba wake, kipindi cha mwezi juni wakati wa hekaheka za Athumani Balozi ambaye nae alikuwa kaimu katibu wa Tabora walikuwa wote hapa Dar es salaam, Athuman akitoa matamko ya kukikashifu chama na miongoni mwa hoja ikiwa ni hii hii ya mjomba wake na baadae akajiunga na ACT.

2. Kansa Mbarouk mara kadhaa amelalamikiwa kuwa amekuwa anatumia ofisi za chama kule Tabora kufanya shughuri za ACT hakuwahi kukanusha, alipoitwa kwenye kikao ajieleze alikuwa yuko Dar es salaam kwa madai anauguliwa lakini wakati huohuo akiwa DSM na watu ACT. Baadae mtu huyohuyo anachukua fomu ya uwenyekiti wa chama (ni haki yake) halafu anatangaza kuwasamehe na kuwarejesha chamani watu walio anzisha chama kingine (ACT).

3. Kuna juhudi tunazozijua za kutaka kuvuruga uchaguzi mkuu wa Taifa, tunajua role ya wapinzani wa chama wanao fadhiriwa na watu ambao tuna majina yao. Kansa Mbarouku amesha anza kazi hii na analipwa, na kuna mlolongo wa magazeti yameanza kuandika leo, si kosa lao kuandika; Cha kujiuliza mbona magazeti hayohayo hayaja hoji uhalali wa yeye kuwa mwenyekiti wa mkoa kwa miaka mitatu na iwe nogwa kwa Mbowe wakati kifungu cha katiba ni kile kile?!

KAMA ULIKUWA HUJUI.

Kansa Mbarouk anatafuta kick ya kwenda ACT lakini walau anataka aonyeshe kuwa amepambana, na hapo atakuja na viroja na uzishi kama aliokuja nao mjomba wake Athumani Balozi wa kuandaa maandamano kwenda kwa msajili na CAG kukituhumu chama kwa propaganda zilezile halafu wiki moja baadae akajiunga na muungano wa usaliti wa waziwazi (ACT).

Tutaona na kusikia mengi.

Haya ni maneno mfa maji,ni lini mmetangaza kumvua madaraka huyu Kansa?!
 
Back
Top Bottom