Prof Haliyamtu
Member
- Oct 16, 2015
- 28
- 2
Sema kweli, wametoa wapi huo utajiri chap chap hivyo? Au ndiyo dil zao zimetick
CHADEMA imekwisha. Inakula matapishi yake.
Sema kweli, wametoa wapi huo utajiri chap chap hivyo? Au ndiyo dil zao zimetick
hatuwezi kuchagua rais dhaifu ambaye hawezi kuhutubu kwa zaidi ya dk 10. Mpiga dili, mzembe. Kura ni kwa magufulially linje tumchague maghufuli aturundikie zigo la madeni, tusipumue??
Hapa tulipo tunadaiwa tayari billion 900/" zenye liba ya kila mwezi billion 150/"madeni ya makandarasi wa barabara hawajalipwa!!
Ahadi zake zimeisha zidi trillion 67/" !! Zimezidi za aliyemtangulia,
magufuli anaongea na kutoa ahadi kama amepagawa, sijui hizo fedha atazitoa wapi??
Tulipe madeni tuachwe utupu kama mashimo ya kahama mine buzwagi!!
Achana na mihemuko chagua rais mwenye busara na hekima lowasa
ukawa mabadiliko!!
Magazeti ya leo yameandika jamaa wapiga dili wanafanya miamala ya kufa mtu kupitia hongkong na dubai. Kweli kura ni mali.
View attachment 300421
View attachment 300420
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekashangwazwa na tuhuma za uongo na uzushi zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari dhidi ya Mwenyekiti wa chama hicho Freman Mbowe za kuhamisha fedha katika akaunti za nje. Anandika Faki Sosi (endelea).Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene ameeleza kuwa hakuna sheria inayomkataza mtu kutofanya biashara na kuhamisha fedha zake binafsi.Akitaja vyombo hivyo amesema kuwa ni Magezeti ya Jambo Leo, Uhuru na Raia Tanzania ambayo yanaonaonekana kuwa na maslahi ya kisiasa kwani habari hiyo imeonekana kuhaririwa na mhariri mmoja kutokana na kutokuwa na uthibitisho wala ushahidi wa upande wa pili.
Mimi ni mwandishi mwenzenu, naifahamu taaluma hii, ukisoma habari hiyo utaona inafanana kwa kila mstari, nukta hadi koma, inaelekea iliandikwa na mwandishi mmoja na kusambazwa kimaslahi kwa magazeti yote matatu na wahariri wakapachika alisema Makene.
Amesema kuwa mwenyekiti huyo ni mfanyabiahara wa kimataifa ambaye anafanya biashara zake halali nje na ndani ya nchi zinazojulikana na serikali, aidha magazeti hayo yanaandika ili kuwaondoa wananchi kwenye ajenda kubwa ya Uchaguzi sababu chama cha Mapinduzi kimeelemewa.
Leo Magazeti matatu yaliandika kuwa Freeman Mbowe, anatuhumiwa kuhongwa ili kumpitisha Edward Lowassa, kuwa mgombea urais wa chama hicho, yakimtuhumu kufanya uhamisho wa mabilioni ya fedha kwenye akaunti yake hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Uhuru, Jambo Leo na Raia Tanzania yaliandika kuwa zilikuwa ni njama za Mbowe, kufanya uamuzi wake wa kumpitisha Lowassa kuwania urais pasipo kushindanishwa na mtu ndani ya chama chake na ndani ya muda mfupi, uamuzi unaodaiwa kukigawa chama hicho,
Hata hivyo gazeti la Mawio limenukuliwa mara kadhaa likiweka wazi kuwa hakuna mgawanyiko kwenye Chadema isipokuwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk Willbrod Slaa ndiye aliyenunuliwa kupitia mke wake Josephine Mushumbusi, na baada ya hapo wamekuwa wakifanya juhudi kubwa kukisaidia CCM ili kudhoofisha Chadema.
Magazeti hayo kwa pamoja yaliandika kuwa Mbowe anahamisha hela hizo wakati wagombea kupitia chama chake hawana hela, hata hivyo Makene alifafanua kuwa hakuna sera ya Chadema kutumia pesa za mtu binafsi na biashara zake kwa ajili ya kusaidia wagombea, isipokuwa hela zinazopatikana kutokana na ruzuku hutumika kwa shughuli za chama na hesabu zake zinajulikana.
Source: Mwanahalisi online
mkuu sio kila anayecoment ni CCM wengine hawana chama lakin wana tanzania , escrow tulipiga kelele , tukawajua walau wezi wetu wachache japo kuna wengine stabinc hatujawajua hadi sasa . si vibaya tukapiga kelele pia kwa haya mengine ya ulaghai .ni mpumbavu pekee ndiye atakayepinga kuwa mbowe alipewa hela na ED ILI apewe hiyo nafasi ya juu
Asante mkuu kwa taarifa.
Wanajisumbua tu hao, lile eneo mimi nalifahamu lipo maeneo ya Kinondo Bunju A.
Kuna mwaka mimi mwenyewe nilikuwa mmoja wa watu ambao tulivamia lile shamba na kujikatia viwanja, lakini walikuka Polisi toka Wazo na kamanda Rwambo wa Oysterday na kusitisha zoezi letu. Lile shamba huwezi kulichukua kwa mpango huo kwani lina hati ya ardhi.
baada ya uchaguzi,mbowe ndo atakua tajiri namba moja tanzania,akifuatiwa na mbatia......
Serikali dhaifu sana hii,yaani mtu anahamisha fedha nyingi kiasi hicho hakamatwi na kuhojiwa! Ndio maana tunataka mabadiliko.
weka picha ya hizo transactions.
Tuendelee kupiga Deal WanaUKAWA zamu yetu sasa kuitafuna nchi! CCM walishaitafuna, sasa tukombe kabisaaa!