BREAKING NEWS: Shamba la Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye lililopo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam limevamiwa na vijana wasiojulikana na kugawana eneo lote.
Taarifa kutoka Bunju zinasema vijana hao walianza zoezi hilo jana majira ya asubuhi ambapo kila mmoja alisimama kwenye eneo analotaka na kukatiwa ambapo wengine walianza maandalizi ya ujenzi.
Vijana hao walisikika wakisema wamechoka kuangalia maeneo makubwa wanayomiliki viongozi yakikaa bila kuendelezwa wakati wao hawana aridhi.
Kama hili lina ukweli na Serikali ikakaa kimya Vigogo wa Lumumba na magogoni wajiandaa na Pesha!
Kama siasa za majukwaani zimewashinda na sasa wamefikia kiasi cha kuwatumia green guards kuvamia mashamba ya watu-ubaguzi huo hautaishia kwa Sumaye tu.